- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
Makaburi ya zamani ambayo yana majeneza kadha
yaliyotengenezwa kwa mawe, na mkufu ulio na "ujumbe kutoka kuzimuni"
vimegunduliwa nchini Misri.
Ugunduzi huo umefanywa Minya, kusini mwa Cairo. Makaburi yaliyogunduliwa
ni ya zaidi ya miaka 2,000 iliyopita na shughuli ya ufukuzi inatarajiwa
kuchukua miaka takriban mitano.
Waziri wa mambo ya kale Misri Khaled al-Enany amesema
makaburi hayo yana majeneza 40, vito, vyungu na barakoa ya dhahabu.
Amesema kuna mashimo ya kuwekwa majeneza chini ya ardhi
ambayo ni ya enzi za Mafirauni hadi enzi za Wagiriki mnamo mwaka 300BC hivi.
"Huu ni mwanzo tu wa ugunduzi huu mpya,"
aliwaambia waandishi wa habari.
"Karibuni tutaanza kuongeza kivutio kingine cha mambo
ya kale Misri."
Mostafa Waziri, mkuu wa ufukuzi huo, amesema makaburi manane
yaligunduliwa katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita lakini anatarajia
mengine zaidi yagunduliwe.
"Shughuli ya ufukuzi inapangiwa kuendelea kwa miaka
mitano hivi katika jaribio la kufukua eneo lote la makaburi," amesema.
Waziri amesema mengi ya makaburi na vitu vya kale
vilivyogunduliwa ni vya makasisi wa miungu wa zamani wa Misri kwa jina Thoth.
Magudulia manne yenye vifuniko ambayo yamehifadhiwa vyema
yameundwa kuwa na muonekano wa wana wanne wa kiume wa miungu Horus pia
yaligunduliwa.
"Bado magudulia hayo yana viungo vya ndani ya mwili vya
marehemu vilivyohifadhiwa vyema ndani. Magudulia hayo yamepambwa kwa maandishi
ya kale yanayoonesha majina na vyeo vya wahusika," amesema Waziri.
Ameeleza sifa ya kugunduliwa kwa mkufu huo Mkesha wa Mwaka
Mpya ukiwa umeandikwa ujumbe "Kheri ya Mwaka Mpya" ni ya ajabu.
"Huu ni ujumbe uliotumwa kwetu kutoka kuzimuni,"
amesema.
Mapema mwezi huu, wanaakiolojia waligundua kaburi la kasisi
wa kike ambaye alizikwa miaka 4,400 iliyopita.
Kaburi hilo lilikuwa limehifadhiwa vyema na lilikuwa na
picha ya ukutani ya kasisi huyo, Hetpet, zikimuonesha akitekeleza shughuli
mbalimbali.
Comments
Post a Comment