- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
ALIYEKUWA
Mwenyekiti wa Simba, Hassani Dalali akizungumza na
wapenzi, wanachama na wakereketwa wa tawi la Simba Cream la Jijini Tanga wakati
alipolitembelea ikiwemo kuhimiza umoja na mshikamano ili kuiwezesha
timu hiyo kuchukua ubingwa msimu huu.
ALIYEKUWA
Mwenyekiti wa Simba, Hassani Dalali akizungumza na
wapenzi,wanachama na wakereketwa wa tawi la Simba Cream
la Jijini Tanga wakati alipolitembelea ikiwemo kuhimiza umoja na mshikamano ili kuiwezesha timu hiyo
kuchukua ubingwa msimu huu kushoto ni Mwenyekiti wa
Tawi
hilo John Bukuku kulia ni Katibu akifuatiwa na katibu Msaidizi na
Mwekahazina wa Tawi hilo Edgar Mdime
Katibu Msaidizi na Mwekahazina wa
Tawi la Simba Cream la Jijini Tanga Edgar Mdime akisoma risala fupi
katika ziara ya Aliyekuwa Mwenyekiti wa Simba Hassani Dalali iliyokuwa
na lengo la kuhimiza umoja na mshikamano ili kuiwezesha timu hiyo
kuchukua ubingwa msimu huu
Katibu Mkuu wa Tawi hilo
akizungumza machache
Sehemu ya
wapenzi,wakereketwa na wanachama wa klabu ya Simba wakimsikiliza
Dalali
Mmoja wa wanachama wa
Simba kutoka Tawi la Simba Cream Chongowe akiuliza swali
Katibu Msaidizi na
Mwekahazina wa Tawi la Simba Cream la Jijini Tanga Edgar Mdime akiteta
jambo na mwanachama wa tawi hilo
Sehemu ya
wapenzi,wakereketwa na wanachama wa klabu ya Simba wakimsikiliza
Dalali
Sehemu ya wapenzi,wakereketwa na wanachama wa klabu ya Simba wakimsikiliza Dalali |
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Simba
Hassani Dalali katika akiwa kwenye picha ya pamoja na wapenzi,wanachama
na wakereketwa wa Simba Jijini Tanga
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Simba
Hassani Dalali akiwa kwenye picha na Katibu Msaidizi wa Tawi la Simba
Cream la Jijini Tanga Edgar Mdime ambaye pia ni Mweka Hazina wa Tawi
hilo
ALIYEKUWA Mwenyekiti wa Simba,
Hassani Dalali amelitaka tawi la Simba Cream la Jijini Tanga kuanzisha timu ya vijana chini ya umri
wa miaka 17 ili iweze kuwa
hazina kubwa ya wachezaji kwa siku za mbeleni.
Licha ya hivyo lakini pia inasaidia kuweza kuinua vipaji vya
wachezaji wachanga ambao
wanaweza kuonekana thamani yao siku zinazokuja kwani mkoa wa Tanga una vipaji vya soka
vingi.
Dalali aliyesema hayo juzi akizungumza na wanachama wa Simba
ikiwemo kuhimiza umoja na mshikamano ili
kuiwezesha timu hiyo kuchukua ubingwa msimu
huukatika tawi
la Simba Cream la Tanga mjini ambalo lilianzishwa mwaka 2013
na kuzinduliwa na aliyekuwa
Rais wa Simba Evans Aveva.
Alisema uanzishwaji wa timu hiyo utakuwa na faida kubwa kwa kusaidia timu hiyo kuwa na hazina ya wachezaji ambao wanaweza kuwatumia kwa miaka ijayo ili kuendelea kuwika kama ilivyokuwa miaka ya nyuma hapa nchini.
“Kwani timu hiyo inapoanzishwa na kuweza kuwa imara itatuwezesha tunapotaka wachezaji tunakuja kuchukua mkoani Tanga kwa sababu tutakuwa tumewekeza mtaji mkubwa wa vijana”Alisema.
Hata hivyo alisema tawi la Simba la Kinondoni kwa miaka ya nyuma ndio ambalo liliwasaidia kuwapelekea mchezaji Uhuru Selemani na baadae yeye kumpeleka kwenye klabu ya Coastal Unon .
Comments
Post a Comment