- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Sekta ya
Mifugo nchini, Dkt Maria Mashingo (mwenye
skafu) akiongea na wafugaji kuhusu upigaji chapa mifugo
kwenye Kijiji cha
Makere Mkoani Kigoma.Kipindi cha kupiga chapa kitaifa knaiisha rasmi leo
Januari 31. (Picha na Ngailo Ndatta)
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Sekta ya
Mifugo nchini, Dkt Maria Mashingo
akishiriki zoezi la Upigaji chapa mifugo katika siku ya mwisho ya zoezi hilo
leo huko Kigoma. Kipindi cha kupiga chapa kitaifa knaiisha rasmi leo Januari
31. (Picha na Ngailo Ndatta
Na John Mapepele, Dodoma
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na
Uvuvi anayeshughulikia Sekta ya Mifugo nchini, Dkt Maria Mashingo amewataka
Wakuu Wote wa Idara katika Wizara ya Mifugo na Uvuvi kuhakikisha
kwamba timu zote zilizosambaa kote nchini ziwe
zimewasili mjini Dodoma leo na kwamba ifikapo saa kumi na mbili jioni ziwe
zimewasilisha taarifa kuhusu zoezi hilo kwake ili akabidhi rasmi kwa Waziri wa
Mifugo na Uvuvi Mh.Luhaga Mpina kwa ajili ya hatua zaidi baada
ya zoezi hilo kuisha rasmi leo.
“Wakuu Wote wa Idara,Mhe Waziri
anataka Timu za Chapa zirudi Dodoma.Leo saa 12 jioni apate taarifa ya mwisho ya
upigaji chapa. Mkurugenzi wa Mipango ratibu timu ya kukamilisha taarifa ”
alisisitiza Mashingo kwenye taarifa yake aliyoitoa jana kwa Wakuu wa
Idara.
Aidha amezitaka Halmashauri zote nchini kuhakikisha
wamemaliza zoezi la kupiga chapa mifugo yao yote katika muda wa
nyongeza uliotolewa na
Serikali ambao uliamuliwa kuwa Januari 31mwaka huu.
Akizungumza katika siku za mwisho
wakati anahitimisha ukaguzi na uhamasishaji wa zoezi la kupiga chapa katika
Mkoa wa Kigoma, Dkt. Mashingo amewaonya baadhi ya wafugaji kutojiingiza katika
matatizo ya kupiga chapa mifugo ambayo inatoka nje ya
nchi ambapo amesema wakibainika watachukuliwa
hatua kali.
Aidha, Dkt. Mashingo amewataka
wafugaji wote wasio raia wa Tanzania
waliyoingia katika mikoa ya mipakani
kuondoa mifugo yao mara moja kwa kuwa haitapigwa chapa badala yake watakamatwa
na kufikishwa katika vyombo vya sheria.
Katika hatua nyingine Dkt. Mashingo
ambaye pia ni mtaalam bobezi katika eneo la malisho ya mifugo amesema
kufanikiwa kwa zoezi la kupiga chapa kutasaidia usimamizi wa Sekta ya Mifugo
hapa nchini ambapo alisema awali inakadiliwa
kwamba 30% ya malisho yote nchini
yalikuwa yakitumiwa na mifugo toka nje
ya nchi.
Ameutaka Uongozi wa Chama cha
Wafugaji Tanzania (CCWT) kutopingana na Serikali badala yake kuongeza
ushirikiano na kuwaelimisha wenzao
kufuga kisasa ili kuondoa migogoro baina ya wafugaji na watumiaji wengine wa
ardhi.
Awali Waziri wa
Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina wakati
akihitimisha zoezi la upigaji chapa mifugo kitaifa lililofanyika katika
wilayani Itilima mkoani Simiyu, Desemba 31mwaka jana aliongeza
siku 30 kwa halmashauri zote nchini ili kukamilisha zoezi la kupigaji
chapa mifugo
huku akiwavua nyadhifa maafisa wawili wa Wizara kwa kushindwa kusimamia zoezi
hilo kikamilifu na wengine wawili wakipewa onyo
kali.
Alida kuwa licha ya
kuwepo kwa baadhi ya changamoto
zilizosababisha zoezi hilo kufanyika kwa asilimia 38.5 tu kwa nchi nzima baadhi
ya watendaji wa serikali na viongozi walichangia kulikwamisha ambapo
Halimashauri ambazo
zikamilisha zoezi la chapa chini ya asilimia 10 zilipelekwa majina ya watendaji
wao kwenye Ofisi ya Waziri Mkuu.
Siku kumi na tano baada ya muda
wa nyongeza wa siku
thelathini, Mhe. Mpina alitoa tathmini mbele ya Waandishi wa Habari mjini
Dodoma, kuhusu tathmini ya utekelezaji wa zoezi la upigaji chapa mifugo ambapo
Mpina alisema hadi kufikia siku hiyo ya Januari 16 mwaka huu jumla ya ng’ombe
10,306,359 sawa na asilimia 59.3 ya lengo walishapigwa chapa ikiwa ni ongezeko
la asilimia 20 ya tathmini ya awali iliyofanywa
Desemba 31 Mwaka jana .
Aidha alisema wafugaji wote
nchini watakaoshindwa kupiga
chapa mifugo yao ndani ya muda uliowekwa hatua kali zitachukuliwa kwa mujibu wa
Sheria ya Utambuzi, Usajili na Ufuatiliaji Namba 12 ya mwaka 2010 ibara ya 4
kifungu cha 26.
Comments
Post a Comment