- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
Mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu wa 2017/2018 kati ya Azam FC na Young Africans utachezwa saa 10 jioni Azam Complex Chamazi.
Mchezo huo namba 115 utachezwa Jumamosi Januari 27, 2018.
Viingilio kwenye mchezo huo ni shilingi elfu kumi(10,000) kwa Jukwaa Kuu na shilingi elfu saba (7,000) kwa majukwaa ya kawaida.
Waamuzi wa mchezo huo wote ni kutoka Dar es Salaam ambapo muamuzi wa kati ni Israel Nkongo akisaidiwa na mwamuzi msaidizi namba moja Josephat Bulali na mwamuzi msaidizi namba mbili Soud Lila, mwamuzi wa akiba Elly Sasii wakati Kamishna wa mchezo huo ni Omar Abdulkadir.
Wakati huo huo, Mchezo namba 114 kati ya Mwadui FC ya Shinyanga na Njombe Mji ya Njombe uliokuwa ufanyike Ijumaa Januari 26, 2018 imesogezwa kwa siku moja kupisha mazishi ya aliyekuwa kocha msaidizi wa Mwadui Jumanne Ntambi.

Mchezo huo sasa utachezwa Jumamosi, Januari 27, 2018.
Kocha huyo msaidizi wa Mwadui alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa shinikizo la damu kabla ya kufikwa na mauti.
Comments
Post a Comment