- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto,
Ummy Mwalimu katikati akiteta jambo na wachezaji wa timu ya African
Sports kabla ya kuwakabidhi hundi milioni 2.1.
WAZIRI
wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto,
Ummy Mwalimu kulia akimkabidhi nahodha wa timu ya African Sports hundi
ya milioni 2.1 leo wanaoshuhudia ni viongozi wa timu hyo na wachezaji
|
WAZIRI
wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto,
Ummy Mwalimu katika akiwa kwenye picha ya pamoja na wachezaji wa timu ya
African Sports mapema leo mara baada ya makabidhiano
hayo
Mmoja kati ya viongozi wa
timu ya African Sports wakimshukuru Waziri Ummy kwa msaada huo
WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia
Wazee na Watoto,
Ummy Mwalimu akizungumza mara baada ya kukabidhi msaada huo.
WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia
Wazee na Watoto,
Ummy Mwalimu amewakabidhi timu ya African Sports “Wana kimanu manu”fedha
milioni 2.1 kwa ajili ya posho za wachezaji wa timu hiyo inayoshiriki Ligi
daraja la pili Tanzania.
Licha ya kukabidhi fedha hizo lakini pia
aliwalipia
kwenye shirikisho la soka Tanzania (TFF)Laki tano (500,000) kwa ajili ya leseni
za wachezaji na ada ya ushiriki wa timu hizo.
Akizungumza wakati akikabidhi msaada
huo,Waziri Ummy
alisema ameamua kutoa msaada huo ili kuiwezesha tmu hiyo kuweza kutimiza
malengo yake ikiwemo kupanda daraja na kufikia hatua ya kucheza Ligi kuu soka
Tanzania Bara.
“Kwani iwapo timu hiyo itarejea Ligi kuu
soka Tanzania
Bara itasaidia kukua kwa fursa mbalimbali za kiuchumi katika
Jiji la Tanga.
“Sambamba na hilo lakini pia tumepokea
mchango wa milioni
3 kutoka Kampuni ya GBP Oil ya Tanga ambao umeweza kuipa hamasa timu hiyo
kufanya vizuri katika mashindano wanayowakabili
“Alisema.
Aidha pia Waziri Ummy aliitaka timu hiyo
wahakikishe
wanafanya vizuri katika michuano hiyo ili kuweza kurejesha hadhi yake ya miaka
ya nyuma ilipoweza kuwika katika medani ya soka hapa
nchini.
“Ndugu zangu wana African Sports
msituangushe hakikisheni
mnatumia misaada hii mnayoipata iweza kuwa chachu ya kufikia malengo yenu ya
kufanya vizuri “Alisema.
Hata hivyo pia Waziri Ummy aliwafungulia
akaunti ya fedha
wachezaji wote wa timu hiyo katika benki ya NMB ili iwe rahisi posho zao
kulipwa moja kwa moja kupitia benki ili kuepusha migogoro inayoweza
kujitokeza.
Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya
Tanga Raha
Comments
Post a Comment