- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
Mwakilishi wa masuala ya biashara wa Uingereza nchini Tanzania, Bw. Lord Clive Hollick (kushoto) akizungumza kuhusu ushirikiano wa kibiashara na Tanzania alipokutana na kufanya mazungumzo na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Khatibu Kazungu (hayupo pichani), katika Ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi wa masuala ya biashara wa Uingereza nchini Tanzania, Bw. Lord Clive Hollick (kushoto) akizungumza jambo aliokutana na kufanya mazungumzo na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Khatibu Kazungu (wa tatu kulia) kuhusu masuala mbalimbali ya biashara na uwekezaji, katika Ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
Kamishna wa Fedha za Nje wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. John Rubuga (kulia) na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Khatibu Kazungu (kushoto), wakimsikiliza kwa makini Mwakilishi wa masuala ya biashara wa Uingereza nchini Tanzania, Bw. Lord Clive Hollick (hayupo pichani) alipokua akizungumzia mazingira bora ya kibiashara kwa maendeleo ya Taifa, katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Khatibu Kazungu akieleza kuhusu uimara wa Serikali katika kusimamia mazingira bora ya biashara ili kusaidia kuinua Sekta binafsi nchini, katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
Kaimu Kamisha wa Sera wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Shogholo Msangi (kulia) akizungumzia masuala ya kodi katika Mkutano wa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Khatibu Kazungu na Mwakilishi wa masuala ya biashara wa Uingereza nchini Tanzania, Bw. Lord Clive Hollick (hayupo pichani), katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam, kushoto ni Kamishna wa Fedha za Nje wa Wizara hiyo Bw. John Rubuga.
Mmoja wa wajumbe walioongozana na Mwakilishi wa masuala ya biashara wa Uingereza nchini Tanzania, (katikati) akifafanua jambo wakati wa Mkutano wa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Khatibu Kazungu na Mwakilishi wa masuala ya biashara wa Uingereza Bw. Lord Clive Hollick (kushoto), mkutano huo umefanyika Ofisi za Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es Salaam.
Comments
Post a Comment