- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
Na John Mnubi, Iringa
Wavuvi
wanaofanya shughuli za uvuvi katika Bwawa la Mtera Kijiji cha Migoli wilayani Iringa wamelalamikia vitendo vya uvuvi haramu
katika bwawa hilo.
Mvuvi,
Albert Mkeleja alizitupia lawama mamlaka husika kwa kutolivalia njuga swala la
uvuvi haramu ambalo limeshamiri sana kwa sasa katika bwawa hilo.
Aidha, Mkeleja alisema hana imani na wanao
endesha zoezi la kukamata wavuvi haramu akidai kuwa wanachelewa kurudia zoezi
hivyo watu wanatengeneza tena nyavu na
kuendelea na uvuvi haramu.
“Alikuja
hapa Mkuu wa Wilaya wakati wa uchaguzi wa wenyeviti wa vijiji tuliongea nae
kuhusu uvuvi haramu akasema tatizo hili malalamiko ni mengi, akamwambia Diwani
kazi yako hii. Halafu akasema kwamba nyinyi wavuvi ndo mnajua zaidi wanaovua
uvuvi haramu kuliko mimi, hivyo mwaweza kudhibiti uvuvi haramu ukaisha kwa
kushirikiana na uongozi wa idara ya uvuvi,” alisema Mkeleja.
Mvuvi
mwingine, Mika Weston, naye alikiri kuwepo kwa
uvuvi haramu uliokithiri katika maeneo ya Bwawa la Mtera upande wa Mkoa
wa Iringa.
“Kwa
kawaida mvuvi unapotega nyavu inabidi ukae pembeni ulinde, lakini maofisa uvuvi
wanakataza badala yake hudai wavuvi warudi forodhani wapaki mitumbwi na kurudi
wanapokaa. Ukirudi kesho unakosa nyavu zako,” alisema Weston.
Ofisa huyu akiangalia nyavu zilizochomwa moto baada ya kukamatwa kutokana na kutokuwa na kiwango kinachotakiwa katika uvuvi.
Ofisa
Mtendaji wa Kata ya Migoli, alisema kuwa kumekuwa na matukio kadhaa ya wavuvi
kuibiana nyavu na samaki kwenye maeneo ambapo wavuvi huvua kwa njia ya kutega.
“Watu na zana hukamatwa kwa mfano, hivi karibuni
kulikuwa na kesi hiyo ambapo watu walikamtwa wakiwa kwenye uvuvi haramu, na
kwasababu huku kwetu kutokana na jitihada za makusudi za uhifadhi, samaki
wanapatika mana samaki hupenda sehemu iliyotulia hivyo wavuvi toka mikoa
mingine jirani hutamani samaki wanaopatikana huku,” alisema Bosco.
Aidha
kwa pamoja Kaimu Ofisa Mtendaji wa
Kijiji cha Makatapola, Msafiri Chansi na Mwenyekiti wa kijiji hicho , Felix
Nzigilwa, waliwatupia lawama maafisa uvuvi wa mkoa wa Dodoma kwa kushindwa
kutilia mkazo swala la uvuvi haramu kama wanavyo jitahidi maafisa wa upande wa
Iringa.
“Maafisa
uvuvi wa wilaya za Dodoma pamoja na wilaya za Iringa kwa pamoja wawe na mpango
mkakati kutokomeza wimbi la uvuvi haramu usiachiwe upande mmoja,” alishauri
Mwenyekiti Nzigilwa.
Kata
ya Migoli ina asili ya ukame,wakazi wake wengi wanategemea bwawa la mtera kwa
ajili ya kujipatia chakula na kipato kingine.
Comments
Post a Comment