- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
Wananchi kutoka maeneo mbalimbali
Jijini Tanga wakishuhudia ajali hiyo leo iliyotokea eneo la Kwaminchi
makutano ya reli baada ya gari ndogo aina ya Carry kufeli breki baada ya
kufika eneo la reli na kuligonga treni iliyokuwa ikitokea eneo la
Pongwe kuelekea Stesheni Jijini Tanga.
Wananchi kutoka maeneo
mbalimbali Jijini Tanga
wakishuhudia ajali hiyo leo iliyotokea eneo la Kwaminchi makutano ya
reli baada ya gari ndogo aina ya Carry kufeli breki baada ya kufika eneo
la reli na kuligonga treni iliyokuwa ikitokea eneo la Pongwe kuelekea
Stesheni Jijini Tanga
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Benedict Wakulyamba akikagua gari hiyo jana jioni. |
Kwa mujibu wa mashuhuda walieleza kuwa gari hilo baada ya kufika eneo la makutano ya reli wakati lijaribu kusimama ndipo lilipofeli breki na kuiparamia treni hiyo.
Ajali hiyo ambayo ilitokea jana eneo la makutano ya reli Kwaminchi Jijini Tanga iliacha mshangao mkubwa kutokana na mazingira ya namna ilivyotoke ambapo gari ndogo ilikuwa ikitokea eneo la kwaminchi.
Akithibitisha kutokea tukio hilo jana,Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga,Benedict Wakulyamba alisema ajali hiyo ilitokea saa kumi jioni katika eneo hilo ambapo gari hilo ilifeli breki na kuparamia mabehewa ya reli wakati ikipita katika eneo hilo.
Aliitaja gari hiyo aina ya Carry ambayo ilipata ajali hiyo kuwa ni T.343 DCQ iliacha njia na kuigonga treli iliyokuwa ikitokea eneo la Pongwe kuingia kwenye stesheni ya Tanga.
Aidha alisema majeruhi sana waliokuwepo kwenye ajali hiyo walifikishwa kwenye hospitali ya mkoa wa Tanga Bombo kwa matibabu zaidi huku Dereva wa gari hilo alitokomea kusikojulikana.
Kamanda huyo alisema kutokana na kukimbia kwa dereva huyo wataendelea kumsaka ili aweze kujibu tuhuma zinazomkabili.
Hata hivyo,Kamanda huyo alitoa wito kwa madereva kuhakikisha wanazingatia sheria za usalama barabarani kwa kuhakikisha kwenye maeneo ya kivuko cha reli wanakaa mita 50.
Awali akizungumza mmoja wa mashuhuda wa ajali hiyo,Said Kiruwasha alisema wakati wakiwa kwenye eneo hilo wakailiona gari hilo moshi likitokea eneo la Pongwe kuelekea Stesheni ndipo gari hilo lilipokuwa likipita ndipo ilipofeli breki baada ya kusikia honi ya treni hiyo.
Habari kwa Hisani ya Blog ya
Kijamii ya Tanga Raha
Comments
Post a Comment