- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
Mkurugenzi wa Maendeleo Bank, Ibrahim Mwangalaba akizungumza hii leo Jijini Mwanza, nje ya ukumbi wa mafunzo ya mjadala kati ya sekta ya umma na sekta binafsi. Mafunzo hayo yameandaliwa na Chemba ya wafanyabiashara wenye viwanda na kilimo nchini TCCIA pamoja na Best Dialogue (Mpango wa kuboresha mazingira ya biashara Tanzania).
Binagi Media Group
Wananchi
mkoani Mwanza wametakiwa kuchangamkia fursa ya ununuaji wa hisa za Maendeleo
Bank ambazo zimeanza kuuzwa tangu Septemba 18 hadi Novemba 03 mwaka huu.
Mkurugenzi
wa benki hiyo, Ibrahim Mwangalaba ametoa rai hiyo hii leo Jijini Mwanza kwenye
mafunzo ya mjadala baina ya sekta ya umma na sekta binafsi yaliyoandaliwa na
Chemba ya wafanyabiashara wenye viwanda na kilimo TCCIA pamoja na pamoja na
Best Dialogue (Mpango wa kuboresha mazingira ya biashara Tanzania).
Mwangalaba
amesema hisa za benki hiyo zinauzwa kwa thamani ya shilingi 600 na kwamba
kiwango cha chini ya ununuzi ni hisa 100 zenye thamani ya shilingi 60,000 hivyo
wananchi wakiwemo wachangamkie fursa hiyo.
“Tunauza
hisa katika soko la hisa na hisa hizi zinauzwa kwenye matawi yote ya benki ya CRDB
ambapo tunaunga mkono juhudi za Rais wetu anayesema uchumi wa Tanzania
umilikiwe na watanzania wenyewe na njia mojawapo ya kuwajumuisha watanzania
wengi ni uuzaji wa hisa sokoni”. Amesisitiza Mwangalaba na kuongeza kwamba hisa
hizo pia zinapatikana ofisi za TCCIA.
Naye Mshauri
wa Hisa, Richard Manamba amesema ununuzi wa hisa una faida nyingi ikiwemo
wanunuzi kupata gawio la faida ambalo benki hulipata na kwamba hisa hizo
huongezeka thamani kulingana na nguvu ya soko.
Maendeleo
Bank yenye mtaji wa shilingi bilioni 10 sokoni inaendelea kuongeza mtaji wake
hadi kufikia shilingi bilioni 17 ambapo inatarajiwa kufungua matawi yake katika
mikoa mbalimbali nchini ikiwemo Mwanza.
Mkurugenzi wa Maendeleo Bank, Ibrahim Mwangalaba akielezea umuhimu wa kununua hisa za benki hiyo hii leo Jijini Mwanza ambapo mafunzo ya mjadala kati ya sekta ya umma na sekta binafsi yanafanyika.
Washiriki wa mafunzo hayo wakimsikiliza Mkurugenzi wa Maendeleo Bank, Ibrahim Mwangalaba wakati akielezea umuhimu wa kununua hisa za benki hiyo.
Mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Magu Mhe.Khadija Nyembo akifungua mafunzo hayo kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhe.John Mongella.
Mwenyekiti wa Chemba ya Wafanyabiashara wenye viwanda na kilimo TCCIA mkoani Mwanza, Elibariki Mmari akizungumza kwenye mafunzo hayo.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo akiwemo Mkurugenzi wa "Maendeleo Bank", Ibrahim Mwangalaba (kulia), wakifutahia mada kwenye mafunzo hayo.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo akiwemo Mkurugenzi wa "Maendeleo Bank", Ibrahim Mwangalaba (kulia), wakifuatilia mada.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo
Washiriki wa mafunzo hayo wakiwa kwenye majadiliano ya makundi
Majadiliano yakiendelea
Washiriki wa mafunzo hayo wakiwa kwenye majadiliano ya makundi
Washiriki wa mafunzo hayo wakiwa kwenye majadiliano ya makundi
Washiriki wa mafunzo hayo pamoja na viongozi mbalimbali wakiwa kwenye picha ya pamoja na mgeni rasmi, Mkuu wa Wilaya ya Magu Mhe.Khadija Nyembo (wa tatu) ambaye alimwakilisha Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhe.John Mongella.
Washiriki wa mafunzo hayo pamoja na viongozi mbalimbali wakiwa kwenye picha ya pamoja na mgeni rasmi, Mkuu wa Wilaya ya Magu Mhe.Khadija Nyembo (wa tatu) ambaye alimwakilisha Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhe.John Mongella.
Comments
Post a Comment