- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
Na Daniel Mbega, MaendeleoVijijini Blog
UVIMBE wa uterine adenocarcinoma,
unaofanana na tezi kama uvimbe wa malignant unaotokana na tishu za ndani kutoka katika
eneo la ndani kabisa la mji wa uzazi, ni miongoni mwa visababishi vya kansa ya
kizazi kwa sungura.
Takriban asilimia 60 ya sungura majike
wenye umri wa zaidi ya miaka mitatu wanaweza kupatwa na tatizo hili.
Uvimbe huu mara nyingi hutokea katika eneo la ndani la mji
wa uzazi au katika ukingo wa mji wa uzazi.
Mara nyingi kansa ya kizazi hutokea baada ya sungura kupata
matatizo mengine ya uzazi kwenye kizazi, ikiwemo kitu kinachoitwa endometriosis, hali ya maumivu
yanayohusisha kukua kwa tishu kwenye uterus na via vya uzazi.
Umri unaonekana kuwa chanzo kikuu cha tatizo hili.
Uvimbe unaweza kuonekana pia pamoja na hali nyingine, kama
kuvimba kwa mishipa ya vena katika ukingo wa mji wa uzazi, hali ambayo pia
kitaalam huitwa venous aneurysms.
Dalili na Aina
Dalili na viashiria vya kansa ya kizazi (uterine adenocarcinoma) inatofautia
kutoka kwa sungura mmoja hadi mwingine, japokuwa sungura yeyote jike mwenye
zaidi ya miaka 3-4 anaweza kupata.
Kuonekana kwa damu katika mkojo kunaweza kuwa dalili kubwa
kwa sungura majike, lakini dalili nyingine ni pamoja na:
* Kutoka majimaji
kwenye uke yaliyochanganyika na damu
* Uvimbe kwenye tezi
za maziwa, na majimaji meupe yanayoweza kutoka kwenye matiti (lakini siyo
maziwa)
* Kubadilika kwa
tabia, ikiwemo tahayari
* Uchovu na kukosa
nguvu, kushindwa kula, utando mweupe (hasa katika hatua za mwisho za ugonjwa)
* Tungamo (mass) katika utumbo (hutokea katika
hatua za mwisho za ugonjwa)
* Kukua kwa matiti.
Chanzo
Sungura yeyote jike ambaye bado anaendelea kuzaa anaweza
kupata kansa ya kizazi.
Uchunguzi
Uchunguzi mara nyingi huanza kwa kuzitenga sababu nyingine
za dalili kama hizo, ikiwemo chanzo kikubwa cha kuwepo kwa tungamo kwenye
tumbo: yaani mimba.
Uvimbe mwingine usio wa kizazi unaweza kusababisha dalili
kama zilizoelezwa hapo juu.
Kukua sana kwa seli kunaweza pia kuendana na dalili nyingine
za uvimbe; hata hivyo, dalili ambazo zimeelezwa hapa zinatajwa kwamba ni za
uwepo wa kansa, hasa kwa sungura wenye zaidi ya umri wa miaka mitatu.
Upungufu mkubwa wa damu (Anemia)
mara nyingi unaendana na hali hii kwa sungura majike na unasaidia katika
kufanya uchunguzi.
Picha mbaya katika vipimo vya maumbo kama X-Ray na
Ultrasound pia vinaweza kusaidia kubaini tatizo, kama ilivyo kwa uvimbe usio wa
kawaida au limfu, ambao unaashiria kusambaa kwa ugonjwa.
Uchunguzi pia unaweza kufanya kwa kutumia matokeo ya biopsy kwenye
tishu ya kizazi.
Tiba
Tiba ya kansa ya kizazi (uterine
adenocarcinoma) inaweza kuhusisha kuondolewa kwa viungo ambavyo tayari
vimeathirika na kansa (complete
hysterectomy).
Kwa kawaida hii ni hatua ya awali, hususan kama kansa
haijasambaa hadi kwenye via vya uzazi.
Uchunguzi wa biopsy unaweza kufanyika kuthibitisha mabaki ya
kansa kwenye via vya uzazi, au kama imeenea nje ya via vya uzazi.
Wakati mwingine hakuna dalili za kuenea kwa kansa wakati wa
kufanya upasuaji.
Ufuatiliaji ni muhimu sana wakati wa tiba hasa kwa kupunguza
maumivu kwa sungura.
Imeandaliwa na www.maendeleovijijini.blogspot.com.
Tupigie: +255 656 331974
Comments
Post a Comment