- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetangaza
‘kuzipiga mnada’ Kata 43 katika Halmashauri 36 nchini, zikiwemo kata
zilizoachwa na madiwani wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)
waliokimbilia Chama cha Mapinduzi (CCM).
Uchaguzi mdogo wa madiwani katika
kata hizo 43 utafanyika Novemba 26, 2017, huku Chadema wakiendelea kulia na ‘mchezo
mchafu’ unaodaiwa kufanywa na madiwani wao watano mkoani Arusha.
Mwenyekiti wa NEC, Jaji Semistocles Kaijage,
amesema uchaguzi huo unafanyika kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo baadhi ya
madiwani kufariki dunia, kujiuzulu, kutohudhuria vikao na wengine ushindi wao
kutenguliwa na Mahakama.
Jaji Kaijage amesema tume imetangaza
kufanyika kwa uchaguzi huo mdogo, baada ya waziri mwenye dhamana ya serikali za
mitaa kuitaarifu tume uwepo wa nafasi wazi za madiwani katika kata hizo 43
zilizoko katika halmashauri mbalimbali 36 na mikoa 19 ya Tanzania Bara.
Jaji Kaijage ameainisha kwamba
kifungu cha 13 (1) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya 292
kinampa mamlaka waziri mwenye dhamana ya Serikali za Mitaa kuitaarifu Tume
kuhusu kuwepo kwa uchaguzi huo mdogo wa madiwani.
Amefafanua kuwa baada ya kupokea
taarifa hiyo na kwa kuzingatia masharti ya kifungu cha 13(3) cha Sheria ya
Uchaguzi ya Serikali za Mitaa; Sura ya 292, Tume ya taifa ya uchaguzi ina
wajibu wa kuitisha na kuendesha Uchaguzi mdogo katika Kata hizo.
“Hivyo, ninapenda kuchukua nafasi hii
kutoa taarifa kuwa tume imepanga kuendesha uchaguzi mdogo katika Kata 43 tarehe
26 Novemba, 2017,” alisema Jaji Kaijage.
Amesema ratiba ya mchakato wa
uchaguzi huo itaanza Oktoba 26 ambapo kutafanyika uteuzi wa wagombea udiwani na
kampeni za uchaguzi huo mdogo zitaanza Oktoba 27 na kumalizika Novemba 25.
Jaji Kaijage amesema Vyama vya Siasa,
Wadau wote wa Uchaguzi na Wananchi wanakaribishwa kwa ajili ya kushiriki kwenye
uchaguzi huo utakaozingatia ratiba iliyoainishwa hapo juu.
Ametoa mwito kwa vyama vya Siasa na
Wadau wote wa Uchaguzi kuzingatia matakwa ya Katiba, Sheria ya Uchaguzi ya
Serikali za Mitaa, Kanuni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa (Madiwani) za mwaka
2015, Maadili ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ya mwaka 2015 pamoja na
maelekezo yote yaliyotolewa au yatakayotolewa na Tume wakati wote wa Uchaguzi
mdogo.
Chadema na Ukawa
Chadema ndicho
chama pekee kati ya vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa)
kilichopoteza viti vingi kwa ama ushindi wa madiwani wake kutenguliwa na
Mahakama au madiwani hao kuhamia CCM.
Katika Mkoa
wa Arusha, Juni 2017 Chadema ilipoteza madiwani nane ambao ni Credo Kifukwe
(Muriet), Anderson Sikawa (Leguruki), Emmanuel Mollel (Makiba), Greyson Isangya
(Maroroni) na Josephine Mshiu (Viti Maalumu).
Kabla hilo
halijapoa, Julai 25, 2017 madiwani watatu wa Chadema katika Halmashauri ya
Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro walitimkia CCM.
Madiwani hao
ni Goodluck Kimaro (Machame Magharibi), Abdallah Chiwili (Weruweru) na Everist
Peter Kimath (Mnadani).
Aidha,
Agosti 23, 2017 Chadema ilipoteza madiwani watatu katika Manispaa ya Iringa
ambao ni Baraka Kimata (Kata ya Kitwiru), na wawili wa Viti Maalum ambao ni Husna
Ngasi na Leah Mlelewa.
Mnamo Februari
2017, Chadema ilipoteza madiwani wawili katika Manispaa ya Shinyanga ambao ni Sebastian
Peter (Kata ya Ngokolo) na Zacharia Mfuko (Kata ya Masekolo) ambao aliamua
kuachia nyadhifa zao kwa kile walichoeleza kuwa ni migogoro isiyokwisha.
Machi
2016, Chadema ilimpoteza Diwani wa Kata ya Siuyu katika Halmashauri ya Wilaya
ya Ikungi, Jared Mahami Jastn (35) amaye alihukumiwa kwenda jela miezi sita baada
ya kutiwa hatiani kwa kosa la kuikosesha serikali mapato.
Ilidaiwa
mahakamani hapo kwamba mnamo Februari mbili mwaka huu saa tatu asubuhi huko
katika mnada wa kijiji cha njiapanda wilaya ya Singida, mshitakiwa kwa makusudi
alimzuia afisa mwidhiniwa Amina Abdallah wa kampuni ya Abada Care Investment,
kufanya kazi ya kukusanya ushuru wa halmashauri ya wilaya ya Ikungi.
Mapema
ilidaiwa katika Mahakama hiyo iliyokuwa chini ya hakimu Simon Jiwawa Kayinga,
kuwa katika siku ya tukio, alitenda makosa mawili ikiwa ni kumuzuia afisa Amina
kufanya kazi yake ya kukusanya mapato ya halmashauri kitendo ambacho ni kinyume
na kifungu cha 12 para ya (e) sheria ndogo ndogo ya halmashauri ya Ikungi.
Kata ambazo zitashiriki kwenye uchaguzi huo ni kama ilivyoanishwa kwenye jedwali hapa chini:
Zifuatazo ni Kata 43 zitazohusika katika Uchaguzi Mdogo wa Madiwani:
Na
|
MKOA
|
HALMASHAURI
|
KATA
|
1.
|
ARUSHA
|
Halmashauri ya Wilaya ya Arusha
|
Musa
|
Halmashauri ya Jiji la Arusha
|
Muriet
| ||
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
|
Ambureni
| ||
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
|
Ngabobo
| ||
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
|
Maroroni
| ||
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
|
Leguruki
| ||
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
|
Makiba
| ||
Halmashauri ya Wilaya ya Monduli
|
Moita
| ||
2. 2
|
DAR ES SALAAM
|
Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni
|
Mbweni
|
Halmashauri ya Manispaa ya Temeke
|
Kijichi
| ||
Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo
|
Saranga
| ||
3.
|
DODOMA
|
Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa
|
Chipogolo
|
4.
|
GEITA
|
Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’wale
|
Bukwimba
|
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
|
Senga
| ||
5.
|
IRINGA
|
Halmashauri ya Manispaa ya Iringa
|
Kitwiru
|
Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo
|
Kimala
| ||
6.
|
KILIMANJARO
|
Halmashauri ya Manispaa ya Moshi
|
Bomambuzi
|
Halmashauri ya Wilaya ya Hai
|
Mnadani
| ||
Halmashauri ya Wilaya ya Hai
|
Machame Magharibi
| ||
Halmashauri ya Wilaya ya Hai
|
Weruweru
| ||
7.
|
LINDI
|
Halmashauri ya Manispaa ya Lindi
|
Chikonji
|
Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa
|
Mnacho
| ||
8.
|
MANYARA
|
Halmashauri ya Wilaya ya Hanang’
|
Nangwa
|
9.
|
MBEYA
|
Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe
|
Ibighi
|
10.
|
MOROGORO
|
Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro
|
Kiloka
|
Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
|
Sofi
| ||
11.
|
MTWARA
|
Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba
|
Milongodi
|
Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara Mikindani
|
Reli
| ||
Halmashauri ya Mji wa Masasi
|
Chanikanguo
| ||
12.
|
MWANZA
|
Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi
|
Kijima
|
Halmashauri ya Jiji la Mwanza
|
Mhandu
| ||
13.
|
RUKWA
|
Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga
|
Sumbawanga
|
14. 14
|
RUVUMA
|
Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
|
Lukumbule
|
Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
|
Kalulu
| ||
Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
|
Muongozi
| ||
15.
|
SINGIDA
|
Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
|
Siuyu
|
16.
|
SIMIYU
|
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
|
Nyabubinza
|
17.
|
SONGWE
|
Halmashauri ya Wilaya ya Momba
|
Ndalambo
|
18.
|
TABORA
|
Halmashauri ya Wilaya ya Nzega
|
Nata
|
Halmashauri ya Wilaya ya Urambo
|
Muungano
| ||
19.
|
TANGA
|
Halmashauri ya Mji wa Korogwe
|
Majengo
|
Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto
|
Lukuza
| ||
Halmashauri ya Wilaya ya Bumbuli
|
Mamba
|
Imetolewa leo tarehe 04 Oktoba, 2017.
Jaji (R) Semistocles S. Kaijage
MWENYEKITI
TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI

Comments
Post a Comment