- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
Ng'ombe anayeumwa Chambavu akiwa amelala. Picha ndogo inaonyesha kidonda kikubwa kwenye mguu kilichotokana na ugonjwa huo.
UGONJWA wa Chambavu au Black Quarter unaoshambulia ng'ombe,
kondoo na mara chache farasi.
Ugonjwa huu unasababishwa
na vijidudu aina ya Clostridium
chauvoei ambavyo hushambulia bila uwepo wa Oksijeni ya
kutosha (anaerobic) na kuzalisha sumu
kwenye mwili wa mnyama na kusababisha kifo.
KUSAMBAA
Vijidudu vya Clostridium chauvoei husambaa kwa kupitia kwenye udongo ambapo mnyama huvipata anapokula
majani.
Lakini pia ugonjwa huu huweza
kusambazwa kwa njia ya vidonda na mate kutoka kwa mnyama mwenye ugonjwa huu.
DALILI
-Homa kali
-Misuli ya miguu ya nyuma
huvimba na kuwa na joto kali, inauma ikiguswa na rangi ya sehemu hiyo ya ngozi
hubadilika
-Ukigusa sehemu
iliyoshambuliwa inatoa sauti kama ya majani makavu
-Mnyama huchechemea mguu wa
nyuma sababu ya maumivu.
UCHUNGUZI
Nyama ya ng'ombe aliyekufa kwa ugonjwa wa Chambavu ikifanyiwa uchunguzi.
Uchunguzi ufanyike na maofisa
ugani wa mifugo kwa kufuatilia dalili na historia ya sehemu husika
-Kipande cha msuli na
majimaji kutoka sehemu iliyoathiriwa kwa ajili ya uchunguzi wa kimaabara
-Uchunguzi wa mwili wa mnyama
aliyekufa (Post Mortem).
MATIBABU
-Tumia dawa za aina ya Penicilin
ambazo zinasaidia kutibu ugonjwa kama matibabu yataanza katika hatua za mwazo,
ukichelewa hutaweza kumtibu mnyama wako.
-Tumia B-Complex na dawa za
kupunguza uvimbe kama visaidizi vya tiba
-Chana sehemu iliyoathirika
ili kutoa majimaji na kuingiza hewa ili kuharibu mazingira ya vijidudu hivyo kuishi.
KINGA
-Chanjo ya mara moja kwa
mwaka kwa wanyama wakubwa.
-Wanyama wadogo wachanjwe
mara wafikishapo umri wa miezi mitatu
-Kwa sehemu ambayo kuna
mlipuko wa ugonjwa huu wanyama wote wachanjwe kisha wapigwe dozi kubwa ya penicilin (kama ugonjwa hautaibuka ndani
ya siku 14 wanyama wako watakuwa salama)
-Miili ya wanyama waliokufa
ichomwe moto na kuzikwa kwenye shimo refu sana ili kuondoa uwezekano wa
vijidudu hivyo kusambaa.
Comments
Post a Comment