- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Unknown
on
- Get link
- X
- Other Apps
Anuani ya
Simu “MKUUPOLISI”
|
Ofisi ya
Inspekta Jenerali wa Polisi,
|
|
Simu : (022)
2110734
|
Makao Makuu
ya Polisi,
|
|
Fax Na.
(022) 21355
|
S.L.P. 9141,
|
|
DAR
ES SALAAM.
|
||
12/09/2017
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Katika
siku za karibuni kumejitokeza vitendo vya baadhi ya watu kutumia majina ama
picha za watu na kuwahusisha na matukio ya kihalifu au matukio yanayohusiana na
uhalifu kwa lengo la kujipatia umaarufu, kuwachafua watu hao au kuwakosanisha
na jamii inayowazunguka.
Mnamo
tarehe 11.09.2017 kupitia mitandao ya kijamii kulisambaa picha ya askari wa
Jeshi la Polisi akihusishwa na muendelezo wa tukio la kujeruhiwa kwa risasi kwa
Mhe. Tundu Lissu (MB) ambapo taarifa hiyo ilimtambulisha askari huyo kuwa ni
kachero wa Kitengo cha Interpol na kwamba yupo jijini Nairobi nchini Kenya
akifuatilia taarifa za Mhe. Lissu.
Jeshi
la Polisi linapenda kukanusha taarifa hizo kuwa si za kweli na ni za uongo
zenye lengo la kumchafua askari huyo na Jeshi la Polisi kwa ujumla. Askari huyo
hayupo Nairobi kama ilivyoenezwa na picha iliyotumika ilipigwa hapa nchini
tarehe 07.01.2017 kwenye sherehe ya mahafali ya mtoto wa kaka yake.
Kuhusiana
na safari ya Nairobi, askari huyo alikuwa nchini Kenya kwa kozi ya kimafunzo
kuanzia tarehe 04.09.2017 na kurejea tarehe 08.09.2017, huku Mhe. Lissu
akipatwa na mkasa wa kujeruhiwa kwa risasi Tarehe 07.09.2017 na kusafirishwa
kwenda Nairobi usiku wa kuamkia tarehe 08.09.2017.
Jeshi
la Polisi linakemea vikali kitendo hiki chenye lengo la kumharibia maisha yake
askari wetu, na linawataka wale wote waliohusika kusambaza au kutajwa katika
taarifa hizo kuripoti kwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) kwa
ajili ya mahojiano. Vilevile tunatoa onyo kwa wote wanaofikiri kuwa wanaweza
kukaa na kupika habari ili waweze kuivuta jamii iwe upande wao na kuchafua
upande wa serikali.
Suala
hili la Mhe. Lissu lipo chini ya uchunguzi ili kuwabaini wote waliohusika na
tukio hili na hatimaye kuwafikisha mahakamani. Ni vema wananchi na wanasiasa
wakaliacha Jeshi la Polisi liweze kufanya kazi yake bila kuliingilia ili kuweza
kupata ukweli wa jambo hili.
Jamii
itambue kuwa Jeshi la Polisi linafanyakazi kwa mujibu wa Sheria, kanuni na
taratibu za Nchi na kamwe halifanyi kazi kwa kuvizia. Endapo mtu yeyote
anahitaji taarifa, tunayo mifumo yetu rasmi inayotuwezesha kupata taarifa
tuzitakazo kupitia uhusiano tulionao ndani na nje ya nchi.
Jeshi
la Polisi kupitia Kitengo cha upelelezi wa makosi ya mitandao (Cyber Crime
Investigation Unit) linaendelea na uchunguzi ili kuwabaini wote waliohusika na
kusambaa kwa taarifa hizi za uongo ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao.
Jeshi
la Polisi linatoa rai kwa wananchi kuacha kutumia mitandao ya kijamii vibaya na
badala yake mitandao hii itumike kwa ajili ya kuelimisha na kuihabarisha jamii
juu ya masuala mbalimbali ya kimaendeleo.
Imetolewa na:
Barnabas David
Mwakalukwa - ACP
Msemaji wa Jeshi la Polisi
Makao Makuu ya
Polisi.
www.policeforce.go.tz www.twitter.com/tanpol www.facebook.com/tanpol www.usalama2.blogspot.com
Comments
Post a Comment