- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF)
Alhaj Mussa Mbaruku kushoto
akimkabidhi viatu Mweka Hazina wa timu ya African Sports, Sad Juma kwa ajili ya kujiandaa na michuano ya Ligi Daraja
la pili makabidhiano hayo
yalifanyika uwanja wa CCM Mkwakwani mjini Tanga.
Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF)
Alhaj Mussa Mbaruku kushoto
akimkabidhi viatu Mweka Hazina wa timu ya African Sports,Sad Juma kwa ajili ya kujiandaa na
michuano ya Ligi Daraja la
pili makabidhiano hayo yalifanyika uwanja wa CCM mkwakwani mjini
Tanga
Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF)
Alhaj Mussa
Mbaruku akisalimiana na wachezaji wa timu ya Jang'ombe ya Zanzibar
ambao wameweka kambi mkoani Tanga wakati alipokwenda kukabidhi vifaa kwa
timu ya African Sports.Vifaa hivyo ambavyo ni seti ya viatu vilitolewa juzi na Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaj Mussa Mbaruku katika halfa iliyofanyika kwenye viwanja wa CCM Mkwakwani mjini Tanga
Akizungumza mara baada ya kukabidhi vifaa hivyo,Mbunge Mussa alisema ameamua kutoa vifaa hivyo ili kuweza kuihamasisha kufanya vizuri katika mashindano hayo na hatimaye kuweza kurudi ilipotoka.
Alisema licha ya timu hiyo kushuka daraja hivi sasa wanapaswa
kujiimarisha na kucheza kwa umakini mkubwa ili kuweza kucheza michuano ya ngazi za juu.
“Mimi ni Mbunge lakini pia ni mwana michezo hivyo nitahakikisha nazisapoti timu za mkoa huu kwa lengo la kurejea kwenye makali yao ya zamani kwani michezo ni ajira “Alisema.
Nay kwa upande wake,Mweka Hazina wa timu hiyo,Sad Juma alimshukuru mbunge huyo kwa kutoa vifaa hivyo ambavyo vitasaidia timu hiyo kuondokana na uhaba uliokuwepo.
“Kama unavyojua sisi tulikuwa na uhaba wa vifaa vya michezo hususani viatu na nyenginevyo hivyo alichotupa mbunge tunamshukuru lakini tutakuwa nawe bega kwa bega “Alisema.
Hata hivyo alisema hivi sasa wanaendelea na maandalizi kwa ajili ya kujiwinda na mashindano hayo wakiwa na kikosi imara ambacho kimedhamiria kupata mafanikio.
Habari kwa hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha.
Comments
Post a Comment