- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Unknown
on
- Get link
- X
- Other Apps
Na Fadhil Paulo
Mayai ni moja ya
vyakula vichache ambavyo naweza kuviweka katika kundi la vyakula ‘bora zaidi’
kuliko vyote.
Mayai yamejaa
viinilishe mhimu na vingi kati ya hivyo viinilishe havipatikani kirahisi katika
vyakula vingi vya kisasa.
Zifuatazo ni faida 10
za kiafya zitokanazo na kula mayai kama zilivyothibitishwa katika tafiti nyingi
duniani:
1. Mayai yana virutubisho vya
kushangaza
Mayai ni moja ya
vyakula vyenye virutubisho vizuri zaidi katika sayari dunia.
Yai moja zima lina
viinilishe vyote vinavyohitajika kuibadili seli moja kuwa kifaranga cha kuku.
Yai moja kubwa
lililochemshwa lina:
Vitamin A: 6%
Folate: 5%
Vitamin B5: 7%
Vitamin B12: 9%
Vitamin B2: 15%
Phosphorus: 9%
Selenium: 22% o
Mayai pia yana kiasi cha kutosha cha Vitamini D, Vitamini E, Vitamini K, Vitamini B6, kalsiamu na Zinki.
Folate: 5%
Vitamin B5: 7%
Vitamin B12: 9%
Vitamin B2: 15%
Phosphorus: 9%
Selenium: 22% o
Mayai pia yana kiasi cha kutosha cha Vitamini D, Vitamini E, Vitamini K, Vitamini B6, kalsiamu na Zinki.
Yai moja pia linakuja
na kalori au nishati 77, gramu 6 za protini na gramu 5 za mafuta yenye afya au
mafuta safi kwa ajili ya mwili (healthy fats).
Mayai pia yana
viinilishe vingine vidogo vidogo (trace nutrients) ambavyo ni mhimu kwa afya
bora.
Hakika… mayai ni
chakula ambacho ni karibu kimejikamilisha, mayai yana karibu kila aina ya
kiinilishe mhimu tunachokihitaji kila siku.
2. Mayai huwa na kolesto nyingi lakini
hayaathiri kolesto katika damu
Ni kweli kwamba mayai
yana kolesto nyingi.
Ukweli ni kuwa, yai
moja tu huwa na kolesto mg 212, ambayo ni zaidi ya nusu ya kiasi cha kolesto
ambacho imependekezwa ule kwa siku ambacho ni mg 300.
Hata hivyo…ni mhimu
kuelewa kuwa kolesto katika mlo huwa si lazima ipandishe kolesto ya kwenye damu.
Kwa kawaida Ini peke
yake huzalisha kiasi kingi cha kolesto kila siku. Wakati tunapokuwa tumekula
mayai zaidi, Ini lenyewe huzalisha kiasi kidogo zaidi cha kolesto ili
kusawazisha hiyo tofauti.
Matokeo ya ulaji wa
mayai hutofautiana toka kwa mtu mmoja hadi mwingine:
. Asilimia 70 ya
walaji wa mayai hawapati kabisa kuongezeka kwa kolesto .
. Asilimia 30 ya walaji wanaripotiwa kuwa wanatokewa kuongezeka kwa kolesto
. Asilimia 30 ya walaji wanaripotiwa kuwa wanatokewa kuongezeka kwa kolesto
3. Mayai huuongeza Msongamano wa juu wa
lipoprotini kolesteroli (rehemu nzuri)
Mayai huuongeza
Msongamano wa juu wa lipoprotini kolesto ijulikanayo kwa kiingereza kama ‘High
Density Lipoprotein’ (HDL). Ambayo hujulikana kama ni kolesto nzuri, maana kuna
kolesto nzuri na kolesto mbaya.
Watu wenye msongamano
wa juu wa lipoprotini kolesto kwa kawaida huwa na uwezekano mdogo wa kupatwa na
maradhi kama kama ugonjwa wa moyo, stroke na matatizo mengine mengi ya kiafya.
Kula mayai ni njia
nzuri ya kuongeza msongamano wa juu wa lipoprotini kolesto.
Katika moja ya
majaribio; kula mayai 2 kwa siku kwa wiki 6 kuliwezesha kuongezeka asilimia 10
ya msongamano wa juu wa lipoprotini kolesto.
4. Mayai yana kiinilishe mhimu sana
kiitwacho ‘Choline’
Choline ndicho
kiinilishe mhimu kabisa ambacho watu wanakikosa na watu wengine hawana habari
kabisa juu ya uwepo wake.
Ndiyo, ni kiinilishe
mhimu zaidi na mara nyingi hupangwa pamoja na vitamin za kundi B.
Hiki ni kiinilishe
kinachopatikana katika mayai ambacho kazi yake kuu mwilini ni kutengeneza ukuta
wa seli na kinacho kazi pia ya kutengeneza molekuli za hisia katika ubongo na
kazi zingine nyingi.
Tafiti zinaonyesha
zaidi ya asilimia 90 ya watu wanapata kiasi kidogo cha choline kati ya kile
ambacho kimependekezwa kila mmoja ale kwa siku.
Yai zima, lote, ni
chanzo kizuri cha choline. Yai moja huwa na zaidi ya mg 100 za kiinilishe hiki
mhimu ambacho watu wengi hawakijuwi.
5. Mayai hubadili msongamano wa chini
wa lipoprotini kolesto
Msongamano wa chini
wa lipoprotini kolesto au kwa kiingereza ‘Low Density Lipoprotine’ (LDL) ndio
ambao hujulikana kama ni kolesto mbaya.
Inajulikana wazi
kuwa, kuwa na msongamano wa chini wa lipoprotini kolesto huleta uwezekano wa
hatari ya kupatwa na ugonjwa wa moyo.
Lakini kile watu
wengi hawakifahamu ni kuwa huu msongamano wa chini wa lipoprotini kolesto
umegawanyika tena katika matawi madogo ambayo yanafanya jumla ya chembe chembe
za msongamano wa chini wa lipoprotini kolesto.
Kuna msongamano wa
chini wa lipoprotini kolesto mdogo, kuna msongamano wa chini wa lipoprotini
kolesto wa kati na kuna msongamano wa chini wa lipoprotini kolesto mkubwa zaidi
katika hizo chembe chembe zinazounda msongamano wa chini wa lipoprotini
kolesto.
Tafiti nyingi
zimeonyesha kuwa watu wenye msongamano wa chini wa lipoprotini kolesto mdogo
kwa muda mrefu, na msongamano wa chini wa lipoprotini kolesto wa kati ndio
ambao huwa na hatari kubwa zaidi ya kupatwa na ugonjwa wa moyo kuliko watu
wenye chembe chembe nyingi za msongamano wa chini wa lipoprotini kolesto mkubwa
zaidi.
Hata kama mayai huwa
na uwezo kidogo wa kuongeza kiasi cha msongamano wa chini wa lipoprotini
kolesto katika baadhi ya watu, tafiti zinaonyesha kwamba chembe chembe hizo
hubadilika toka katika usawa mdogo hadi katika usawa wa kati hadi kuja kuwa
katika usawa mkubwa ambao ni jambo zuri.
6. Mayai huondoa sumu na kusaidia
kuongeza nuru ya macho
Moja ya matokeo ya
kuzeeka ni macho kupoteza uwezo wake wa kuona vizuri.
Kuna viinilishe
kadhaa ambavyo vinaweza kusaidia macho yetu kubaki na nuru na uwezo mzuri zaidi
kwa miaka mingi hata uzeeni. Moja ya viinilishe viwili mhimu zaidi katika
kufanya kazi hiyo ni hivi vijulikanavyo kama Lutein na Zeaxanthin vipatikanavyo
katika mayai, ambavyo ni viuaji sumu vyenye nguvu au vyenye kazi ya kuondoa
sumu ambavyo hujijenga katika retina ya jicho.
Tafiti zinasema
matumizi ya kutosha ya viinilishe hivi viwili yanaweza kupunguza kwa kiasi
kikubwa hatari ya kupatwa na ugonjwa wa mtoto wa jicho (cataract).
Kwa ujumla kiini cha
yai kina kiasi kingi kabisa cha Lutein na Zeaxanthin.
Katika moja ya
jaribio, ulaji wa 1.3 wa kiini cha mayai kwa siku kwa wiki 4 ulionyesha kuongezeka
kwa kiasi cha usawa wa Lutein kwa asilimia 28 hadi 50 na Zeaxanthin kwa
asilimia 114 hadi 142.
Mayai pia yana kiasi
kingi cha vitamin A. Upungufu wa vitamin A ndicho chanzo kikuu cha upofu katika
sehemu nyingi duniani.
7. Mayai yenye kiasi kingi cha Omega-3
husaidia kupunguza mafuta yapatikanayo katika damu (triglycerides);
Kwa hakika,
haijalishi ni chakula gani tunakula … tunaangalia pia ni vyakula gani ambavyo
tunakula na tumekula.
Katika hili, ni kuwa
siyo mayai yote ya kuku yapo sawa na ni mazuri. Viinilishe vilivyomo kwenye yai
vinategemea ni kwa namna gani kuku waliotaga hayo mayai walikuwa wakilishwa
nini na wamekua katika mazingira gani.
Mayai toka kwa kuku
ambao wanafugwa vizuri na wanapewa vyakula vyenye Omega-3 hutokea kuwa na asidi
mafuta mhimu zijulikanazo kama ‘Omega-3 fatty acids’.
Asidi mafuta Omega-3
zinajulikana katika kupunguza usawa wa mafuta yapatikanayo katika damu
(triglycerides), ambayo yanahusika sana na ugonjwa wa moyo.
Tafiti zinaonyesha
kwamba ulaji wa mayai yenye asidi mafuta Omega-3 ni njia nzuri zaidi katika
kupunguza mafuta yapatikanayo katika damu. Katika moja ya majaribio, ulaji wa
mayai matno tu yenye asidi mafuta Omega-3 kwa wiki kwa muda wa wiki tatu
kulipunguza mafuta yapatikanayo katika damu (triglycerides) kwa asilimia 16
hadi 18.
8. Mayai yana protini yenye ubora wa
hali ya juu na amino asidi mhimu kwa uwiano mzuri
Protini ndiyo
matofali mhimu zaidi katika ujenzi wa mwili wa binadamu.
Protini hutumika
kutengeneza aina zote za tishu na molekuli ambazo ni mhimu katika ujenzi na
ufanyaji kazi wa mwili.
Kupata kiasi cha
kutosha cha protini katika mlo wako ni mhimu sana na tafiti zinaonyesha kiasi
cha protini ambacho kimependekezwa kuwa ndicho unachopaswa kula kila siku
chaweza kuwa ni kidogo sana.
Ndiyo… mayai ni
chanzo kizuri kabisa cha protini, huku yai moja likiwa na gramu 6 za protini.
Mayai yana amino
aside zote mhimu zaidi kwa usawa mzuri na hivyo mwili wetu unakuwa
umehakikishiwa utumikaji wa protini hiyo ipatikanayo katika mayai.
Kula kiasi cha
kutosha cha protini kunaweza kuwa msaada katika kupunguza uzito, kuongeza
uwingi wa mishipa, kupunguza shinikizo la juu la damu na kuimarisha afya ya
mifupa, kwa kuyataja machache kati ya mengi ya faida ya ulaji wa kutosha wa
protini.
9. Mayai hayaleti ugonjwa wa moyo na
yanaweza kupunguza hatari ya kupatwa na Stroke
Kwa karne nyingi au
kwa miaka mingi sasa mayai yamekuwa yakisemwa vibaya sana bila sababu yoyote
yenye ukweli.
Imekuwa ikiaminiwa
kwamba kwa sababu mayai yana kiasi fulani cha kolesto ndani yake basi lazima
yatakuwa ni mabaya kwa afya ya moyo!
Tafiti nyingi
zilizofanywa katika miaka ya karibuni zimejaribu kuangalia uhusiano uliopo kati
ya ulaji wa mayai na hatari ya kupatwa na ugonjwa wa moyo.
Katika uchunguzi
mmoja ukihusisha tafiti 17 katika jumla ya watu 263,938, hakuna uhusiano wowote
ulioonekana kuwepo baina ya ulaji wa mayai na ugonjwa wa moyo.
Tafiti nyingi zaidi
na zaidi zimeendelea kutoa hitimisho hili moja linalofanana.
Ingawa… baadhi ya
tafiti zimeweza kuonyesha kuwa watu wenye kisukari hasa wenye kisukari cha aina
ya pili wanaokula zaidi mayai wanakuwa na hatari ya kupatwa na ugonjwa wa moyo.
Iwe ni kweli kwamba
mayai yanasababisha kuongezeka kwa hatari ya kupatwa na ugonjwa wa moyo bado
hili halijulikani, sababu tafiti za namna hii huwa zinaonyesha tu uhusiano wa
kitakwimu, tafiti hizo huwa haziwezi kuthibitisha kwamba ni mayai ndiyo
yamesababisha chochote.
Inawezekana kwamba
baadhi ya wagonjwa wa kisuakri wana uelewa mdogo juu ya mambo mhimu kuhusu afya
zao.
Katika mlo ambao inahimizwa
kuepuka vyakula vya wanga, mlo ambao ndiyo watu wenye kisukari hushauriwa
kuishi hivyo, ulaji wa mayai ungeweza kuwa ni msaada katika kuepuka hatari za
kupatwa na ugonjwa wa moyo.
10. Mayai humtosheleza mlaji kwa haraka
na hivyo kusaidia kupunguza uzito
Kwa hakika mayai ni
matamu sana!
Ni chakula chenye
protini ya kutosha… na kwa hakika protini ndiyo sehemu mhimu zaidi katika
lishe.
Mayai yanashikilia
alama ya juu kabisa katika kipimo kijulikanacho kama ‘Satiety Index’, ambacho
kinapima uwezo wa chakula katika kumtosheleza na kumlidhisha mlaji huku
yakiepusha ulaji wa kuzidi wa kalori.
Katika utafiti mmoja
uliohusisha wanawake 30 wenye uzito uliozidi, kitendo cha kula mayai asubuhi
badala ya mkate kiliwaongezea hisia za kujisikia kutosheka na hivyo moja kwa
moja (automatically) wakafanikiwa kuwa wanakula chakula kiasi kwa masaa 36
yaliyofuata.
Katika jaribio
linguine, kitendo cha kubadili kula mayai badala ya mkate katika mlo wa asubuhi
kilisababisha kupungua uzito kwa haraka ndani ya kipindi cha majuma 8 tu.
Namna ya kujuwa iwapo
mayai ni freshi au la
Utajuwaje kama haya
mayai ni freshi au ni mapya kwamba yatakuwa hayaharibika ndani yake? Fanya
hivi; weka maji ndani ya kindoo kidogo au hata katika bakuli kubwa, tumbukiza
yai, ikiwa yai litakwenda moja kwa moja chini hilo ni yai zuri, ikiwa linaelea
katikati ya maji hilo ni zuri lakini linatakiwa litumike haraka na ikiwa
linaelea tu hapo juu ya maji hilo ni la kutupwa tu tayari limeshakuwa bovu.
Ujumbe mhimu kuhusu ulaji mayai
Tafiti zinaonyesha
ulaji wa mayai hadi matatu kwa siku ni salama kabisa kwa afya.
Hakuna ushahidi
kwamba kula kwa kiasi hicho ni vibaya. Mimi binafsi ninakula wastani wa mayai 3
hadi 6 kwa siku na afya yangu ipo safi kabisa.
Ndiyo … mayai ni
chakula cha asili ambacho ni safi kabisa.
Zaidi ya yote, mayai
pia yanauzwa bei rahisi, ni rahisi kuyapika na yanaweza kulika karibu na kila
chakula na yana ladha ya kipekee yawapo mdomoni.
Comments
Post a Comment