- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Unknown
on
- Get link
- X
- Other Apps
Na Binagi Media Group
Mchekeshaji maarufu nchini Tanzania Emmanuel Mathias (MC Pilipili) amelazwa katika hospitali ya Rufaa ya Bugando Jijini Mwanza kwa ajili ya matibabu baada ya kupata ajali mbaya ya gari mkoani Shinyanga.
Kamanda wa polisi mkoani Shinyanga, Simon Haule amesema ajali hiyo ilitokea jana majira ya saa kumi alasiri katika Kijiji cha Mwanishoni, Kata ya Bubiki wilayani Kishapu katika barabara ya Mwanza-Shinyanga.
Amesema ajali hiyo ilihusisha gari binafsi lenye nambari T.362 BAE Toyota Prado iliyokuwa na abiria watatu ikiendeshwa na dereva Said Hassan (28) mkazi wa Dar es salaam, ikitokea Mwanza kwenda Dar es salaam.
Kamanda Haule amesema chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi na kwamba majeruhi wanaendelea kupatiwa matibabu.
Afisa Uhusiano hospitali ya Rufaa Bugando, Lucy Joseph amekiri kupokelewa Mc Pilipili hospitalini hapo kwa ajili ya matibabu na kwamba hali yake inaendelea kuimarika. Dr.Hans Klaudi kutoka idara ya upasuaji hospitali ya Kanda Bugando Jijini Mwanza ambaye ni mmoja wa madaktari wanaomtibu Mc Pilipili, amezungumza na BMG na kueleza hali yake.
Inaelezwa kwamba ajali hiyo ilitokea wakati dereva akijaribu kumkwepa mwendesha baiskeli na hivyo kupinduka.

Mchekeshaji na Mshereheshaji Mc Pilipili

Comments
Post a Comment