- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Unknown
on
- Get link
- X
- Other Apps
New York, Marekani
KAMA ingekuwa ni Tanzania, ukifika dukani ungeuliwa: "Unataka cha Arusha, Makambako, Morogoro au Malawi?" Lakini sasa huko ni Marekani, taifa kubwa linaloongoza kwa uchumi duniani.
Na Jimbo la Colorado
nchini humo ndilo lenye uchumi unaokua kwa kasi zaidi
kuliko majimbo mengine yote 51 yaliyobakia.
Ukuaji huo unatokana na kitendo cha Serikali ya jimbo hilo kuhalalisha matumuizi
ya bangi na mimea kama hiyo Januari 2012.
Kwa sasa jimboni humo
maduka ya kuuza bangi na mimea kama mhiyo yanaingiza jumla ya dolari milioni
295 (sawa na shilingi bilioni 590 za Tanzania) huku Derikali ikipata jumla ya Dola
51 milioni (sawa na Shs. 112.2 bilioni za Tanzania) kama kodi ya mapato.
Taarifa zinasema kuwa
kutokana na hatua hiyo ya Serikali ya kuruhusu matumizi ya bangi, utalii
jimboni humo umeongezeka maradufu huku vituo vya afya vya tiba kwa wanaopata
madhara vikiongezeka pia.
Hata hivyo, pamoja na
kwamba bangi ni halali jimboni Colorado, lakini inauzwa kwa watu wenye umri
kuanzia miaka 21 na kuendelea na si chini ya umri huo.
Uangalizi makini
hufanywa kwenye maduka yanayouza bangi hiyo na yeyote anayekwenda kinyume cha
amri hiyo hujikuta akifikishwa mbele ya sheria na vyombo vya dola.
Inaelezwa kwamba watu
wengi wanapenda kutumia bangi kutokana na kwamba huwasaidia kupunguza maumivu
ya mwili na uchovu wa usingizi.
Ziko bidhaa nyingine
ambazo huwekwa unga wenye bangi kama vile mananasi, maembe, nyanya na vitu vingine
vya majimaji au mafuta ambavyo watu hupenda kutumia na hivyo kujikuta
wakiliongezea jimbo hilo pato la ajabu na kuongoza kwa uchumi nchini Marekani.
Rais wa zamani wa Marekani,
Barak Obama, katika kampeni zake za kuwania Urais wa nchi hiyo mwaka 2008,
alikiri kuwa amewahi kuvuta bangi na kusema kuwa ni bora kuliko sigara.
Hata hivyo, bangi
imepigwa marufu sehemu nyingi duniani ikiwemo Tanzania kwa madai kuwa
inahatarisha maisha ya watu.
Comments
Post a Comment