- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Unknown
on
- Get link
- X
- Other Apps
Kocha wa timu ya Bandari Tanga Mohamed Fazal akitoa maelekezo kwa timu hiyo wakati wa mapumzikokulia ni PRO wa Bandari ya Tanga,Moni Jarufu |
Kocha wa timu ya Bandari Tanga,Mohamed Fazal akitoa mawaidha kwa timu hiyo wakati wa mapumziko kulia ni PRO wa Bandari ya Tanga,Moni Jarufu |
Kikosi cha timu ya Mpira wa Kikapu ya Bandari Tanga. |
TIMU ya Mpira wa Kikapu ya Bandari Tanga ambayo
inashikilia Ubingwa wa Mashindano ya Kilimanjaro Cup mwaka jana inashiriki tena
Mashindano hayo kutetea ubingwa huo mwaka huu katika mashindano yanayoendelea
kwenye viwanja KCMC mjini Moshi.
Kitendo cha timu hiyo kuendelea kufanya vizuri katika
mashindano hayo kwa mara nyengine kinaonyesha namna kinavyotumia vema fursa
hiyo kuitangaza Bandari ya Tanga.
Katika kuhakikisha suala hilo linakwenda kwa vitendo
leo timu ya Bandari Tanga wameibuka na ushindi wa vikapu 64-57 dhidi ya timu ya
Baptist katika mechi iliyokuwa na upinzani mkubwa huku Bandari Tanga ikipambana
ili kuhakikisha inatetea Ubingwa wake na kuondoka na ushindi
huo.
Awali akizungumza wakati akizundua mashindano hayo,
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mgwira amezitaka timu shiriki kutumia fursa
ya mashindano hayo kutangaza utalii wa nchi ikiwemo mlima
Kilimanjaro.
“Baada ya mashindano haya timu zote shiriki
zitakwenda kupanda mlima Kilimanjaro ili kuweza kuhamasisha wanamichezo na
wananchi wengine kuweza kutalii mlima huo “Alisema Mkuu huyo wa
mkoa.
Mkuu huyo wa mkoa alitumia nafasi hiyo kuwataka
vijana kuchangia damu kwa wahitaji ambapo katika viwanja hivyo sehemu
iliyotengwa
kwa ajili ya kuchangia damu kwa hiari.
Mashindano hayo yanaendelea kwa wiki nzima katika
viwanja vya Baptist na KCMC Mkoani Kilimanjaro.
Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha
Comments
Post a Comment