- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Unknown
on
- Get link
- X
- Other Apps
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA
NCHI
JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI
OFISI YA KAMISHNA
JENERALI
JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI
S. L. P. 5821,
DAR ES
SALAAM.
|
|
Simu Nambari: +255-22-2181093
Telefax: + 255-22-2184569
Barua
Pepe: fire.rescue@frf.go.tz
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Tanzania Bara, Thobias Andengenye
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Kamishna Jenerali wa
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Tanzania Bara, Thobias Andengenye, amefanya
mabadiliko ya baadhi ya Makamanda wa Mikoa na Wakuu wa Vitengo wa Jeshi hilo.
Katika
mabadiliko hayo, aliyekuwa Kamanda wa Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Arusha
Kamishna Msaidizi (ACF) Bakari Mrisho, amekuwa Mkuu wa Chuo na Mafunzo, nafasi
yake inachukuliwa na Mrakibu (SF) Kennedy Komba, ambaye alikuwa Kamanda wa
Zimamoto Mkoa wa Iringa na nafasi yake inachukiliwa na Mrakibu Msaidizi (ASF)
James John toka Makao Makuu.
Kamanda
wa Mkoa wa Kilimanjaro Kamishna Msaidizi (ACF) Gilbert Mvungi, amekuwa Kamanda
wa Zimamoto Mkoa wa Kigoma, nafasi yake inachukuliwa na Kamishna Msaidizi (ACF)
Baraza Mvano ambaye alikuwa Kamanda wa Zimamoto Mkoa wa Kigoma.
Kamanda
wa Viwanja vya Ndege Nchini, Kamishna
Msaidizi (ACF) Juma Kwiyamba amehamishiwa Makao Makuu, nafasi yake inachukuliwa
na Kamishna Msaidizi (ACF) Christom Manyologa.
Kamishna
Msaidizi (ACF) Fikiri Salla amekuwa Kamanda wa Mkoa wa Mbeya, anajaza nafasi
iliyokuwa wazi baada ya Kamanda wa Zimamoto Mkoa wa Mbeya kuteuliwa na Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na
Usalama Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kuwa Kamishna wa Usalama dhidi ya Moto.
Kamanda
wa Zimamoto Mkoa wa Pwani, Mrakibu Msaidizi (ASF) Goodluck Zelote amekuwa
Kamanda wa Zimamoto Mkoa wa Tanga, nafasi yake inachukuliwa na Mrakibu Msaidizi
(ASF) Happy Shirima toka Makao Makuu.
Mrakibu
Msaidizi (ASF) Fatma Ngenya amekuwa Kamanda wa Zimamoto Mkoa wa Manyara,
anachukua nafasi ya Mkaguzi Msaidizi (A/INSP) Heriel Kimaro ambaye amehamishiwa Makao Makuu.
Uhamisho
huo ni Mabadiliko ya kawaida yanayotokea ndani ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji,
katika kuongeza ufanisi wa utendaji kazi.
Imetolewa na;
KITENGO CHA HABARI NA ELIMU KWA UMMA,
MAKAO MAKUU.
16 AGOSTI, 2017.
Comments
Post a Comment