- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Unknown
on
- Get link
- X
- Other Apps
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin
Ngonyani, akiongea na Baraza la Wawakilishi la Kamati ya Ardhi na Mawasiliano kutoka
Zanzibar na uongozi wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), (hawapo pichani),
wakati wa ziara ya kikazi ya Kamati hiyo, jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Kamati ya Ardhi na Mawasiliano kutoka Zanzibar,
Mhe. Hamza Hassan Juma, akizungumza na wajumbe na watendaji, katika ziara ya
kikazi kwenye Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) Eng.
Ladislaus Matindi (katikati) akifafanua jambo kwa wajumbe wa Baraza la Wawakilishi
la Kamati ya Ardhi na Mawasiliano kutoka Zanzibar, wakati wa ziara ya kikazi
kwenye Shirika hilo, jijini Dar es Salaam.
Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi la Kamati ya Ardhi na
Mawasiliano kutoka Zanzibar wakimsikiliza kwa makini Naibu Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano, Eng. Edwin Ngonyani (hayupo pichani), wakati wa ziara
ya kikazi katika Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi
kavu na Majini (SUMATRA), Gilliard Ngewe, akifafanua jambo kwa wajumbe wa Baraza
la Wawakilishi la Kamati ya Ardhi na Mawasiliano kutoka Zanzibar wakati wa
ziara ya kikazi katika Mamlaka hiyo, jijini Dar es Salaam.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
Serikali
imesema kuwa Shirika la Ndege nchini (ATCL), litaendelea kushirikiana na
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kuhakikisha inaboresha huduma za
usafiri wa anga katika visiwa vya Unguja na Pemba.
Akizungumza
katika kikao kilichokutanisha Baraza la Waakilishi la Kamati ya Mawasiliano na
Ardhi kutoka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na uongozi wa Shirika
hilo, Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi
Edwin Ngonyani, amesisitiza kuwa changamoto ambazo wameziwasilisha katika
kikao hicho zitafanyiwa kazi ili kuleta tija kwa pande zote mbili.
"Nawahakikishia
wajumbe wa kamati hii kuwa changamoto mlizonazo tutazifanyia kazi haraka kwani
ATCL sasa imezaliwa upya na hivyo itahakikisha inaboresha maslahi ya kuliinua
na kuliendeleza shirika ili kuweza kukidhi mahitaji ya hapa na visiwani",
amesema Naibu Waziri Ngonyani.
Aidha,
Mhandisi Ngonyani ameongeza kuwa katika kuhakikisha huduma za usafiri wa anga
visiwani humo zinaimarika, tayari Serikali imeshaanza kulipa deni lililokuwa
linadaiwa na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege la shilingi milioni 241 ambalo
shirika hilo linadaiwa kutokana na tozo ya maegesho ya ndege na Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Hamza Juma, amemwomba Naibu Waziri
Mhandisi Ngonyani kuangalia upya suala la ajira katika Shirika la ATCL ili
liweze kubeba sura ya Muungano na kuwawezesha wataalam wenye sifa kutoka
Zanzibar nao kupata nafasi hizo.
"Tunaomba
Shirika na baadhi ya Taasisi zinazofanya kazi kwa kushabihiana na masuala ya
Muungano kuzingatia utoaji wa ajira katika nafasi wanazozitangaza kwani
Zanzibar ina wataalam wenye sifa lakini hawapati fursa" amesisitiza
Mwenyekiti wa Kamati.
Naye, Mwenyekiti wa Bodi ya ATCL, Mhandisi Emmanuel Korosso, amesema kuwa Shirika hilo linaendelea kuimarika na kusambaza huduma katika viwanja mbalimbali vya ndege nchini licha ya kuwa na changamoto za uhaba wa marubani.
Naye, Mwenyekiti wa Bodi ya ATCL, Mhandisi Emmanuel Korosso, amesema kuwa Shirika hilo linaendelea kuimarika na kusambaza huduma katika viwanja mbalimbali vya ndege nchini licha ya kuwa na changamoto za uhaba wa marubani.
Katika
hatua nyingine, Kamati hiyo imetembelea Makao Makuu ya Mamlaka ya Udhibiti wa
Usafiri wa Nchi kavu na Majini (SUMATRA) na kupendekeza kwa Mamlaka hiyo kutoa
kipaumbele katika suala la ajira na vibali kwa mabaharia kutoka Zanzibar ambao
wamesajiliwa chini ya Mamlaka ya Usafiri wa Baharini Zanzibar (ZMA), kufanyika
kwa wakati.
Ziara
ya kamati hiyo imelenga kutatua, kupunguza na hatimaye kumaliza kero za
Muungano ambazo zinagusa Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano
na Usafirishaji ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
Comments
Post a Comment