- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Unknown
on
- Get link
- X
- Other Apps
Mkufunzi wa semina ya wadau mbalimbali wanaotumia Teknologia ya biogas ,pamoja na wamiliki wa mitambo hiyo pamoja na mafundi Rowah Spear akiendelea kutoa elimu katika semina hiyo inayofanyika leo jiji hapa.
wakwanza kulia ni Mratibu wa Ubunifu kutoka ECHO Harold Msanya akiwa anafafanua jambo mbele ya wakufunzi hao
baadhi ya washiriki wa semina hiyo wakiendelea kufanya kazi ya majadiliano katika makundi
Mkufunzi wa semina ya wadau mbalimbali wanaotumia Teknologia ya biogas ndugu Rowah Spear akiwa anawaelekeza baadhi ya wadau waliouthuria semina jinsi biogas inaweza kufanya kazi
wadau wakiendelea kufatilia mada ilikuwa inaendelea
Mkurugenzi wa ECHO Erwin Kinsey akiwa anaonyesha wakulima na wadau walioshiriki semina hiyo mmea aina ya gugukaroti ambalo ,alisema kuwa gugu ilo kwa asilimia 90% huku asilimia 10% ni gugu ambalo linaweza kutumika kutengeneza biogas(na woinde shizza,Arusha)
wadau wakiendelea na majadiliano katika makundi yao ikiwa ni sehemu ya kujifunza njia mbalimbali na matumizi ya biogas
Habari picha na Woinde Shizza,Arusha
Wananchi wametakiwa kutumia Gesi Bayogesi
kwani inapunguza gharama za watumiaji wa vyanzo
vingine vya nishati ,pia gesi hii
inasaida kutunza mazingira .
Hayo yamebainishwa leo na Mratibu wa Ubunifu kutoka ECHO Harold
Msanya wakati akitoa mada katika semina ya wadau mbalimbali wanaotumia Teknologia
ya biogas , wamiliki wa mitambo hiyo pamoja na mafundi wanaofunga na
kutengeneza mitambo hiyo .
Alisema kuwa gharama
za nishati ya umeme na gesi asilia ni ghali sana hasa kwa mtumiaji
atakayedhamiria kutumia jiko la umeme au jiko la gesi lakini kwa gesi hii ya
samadi mtumiaji au mabaki ya nyasi aina
mbalimbali zitamgharimu muda wake tu kujaza samadi na maji kila siku na atakuwa
hana malipo ya pesa kila mwezi kama itakavyomlazimu kulipia umeme na gesi
asilia kila mwezi, na hata kuni ambazo watumiaji wengine hununua
Alibainisha kuwa njia hii imeweza kuwasaidia na kuwapa
faida baadhi ya wananchi ambao wameanza kutumia teknoligia hii na pia wengi wao
wameshanufaika na huduma hii .
Aidha Bayogesi ambayo aghalabu hutokana na
kinyesi cha wanyama, masalia ya mimea na kinyesi cha binadamu inaweza
kuzalishwa na kutumika kupikia na hata matumizi mengine kama vile kuendeshea
mitambo mbalimbali.
“ Matumizi ya
gesi hii kwa mtu ambaye ana mifugo kama vile nguruwe, ng’ombe yanaweza kusaidia
kuondokana na gharama za kununua nishati ya kuni, mkaa, umeme na hata gesi
asilia inayochimbwa ardhini.”alisema
Msanya
Kwa upande wake mkufunzi wa Mkufunzi wa semina ya wadau mbalimbali wanaotumia
Teknologia ya biogas ,pamoja na wamiliki wa mitambo hiyo pamoja na mafundi
Rowah Spear alisemak uwa ni wajibu wa kila mtanzania kuwakikisha anakuwa na
mtambo huo kwani mtambo huo unapunguza gharama
kubwa ambazo awali walikuwa wanatumia ,na pia pale mwananchi anapotumia
mtambo huu anakuwa rafiki wa mazingira kwani kwanza kabisa akati miti ovyo na
pili yale majani ,vyakula ,na uchafu
uchafu wa aina wowote anaweza kuukusanya na kuingiza katika mashina na
ikamsaidia kupatikana kwa Biogas
Pia
alisema kuwa mbali na kupata nishati yakupikia tu pia uchafu ambao unakuwa
umetokana na mabaki haya unaweza kufanywa kama mbolea kwa mazao mbalimbali
tunayoyalima hivyo ni vyema kila mwananchi kuhakikisha nyumbani kwake anamtambo
huu
Comments
Post a Comment