Featured Post

WAKUTANA KUPANGA MKAKATI WA KUPAMBANA NA USAFIRISHAJI HARAMU WA BINADAMU

Katibu wa Kamati ya Kuzuia Usafirishaji Haramu wa Binadamu, Seperatus Fella, akizungumza na  wadau kutoka taasisi  zinazojihusisha na kupambana na biashara hiyo waliokutana katika jijini Dar es Salaam leo, ili kujadili mikakati ya kutokomeza biashaara hiyo nchini. Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Picha na  Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.


Afisa uchunguzi Sekretarieti ya Kuzuia na Kupambana na Biashara Haramu ya Usafirishaji Binadamu, Ahmed Mwendadi, akifafanua jambo kwa wadau kutoka Taasisi  zinazopambana  na biashara hiyo waliokutana  jijini Dar es Salaam, ili kujadili mikakati ya kutokomeza biashaara hiyo. Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Picha na  Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 

Mkurugenzi Mtendaji wa ANPPCAN Tanzania, Wilbert Muchunguzi, akieleza jambo juu ya shughuli wanazofanya katika kupambana na Biashara Haramu ya Kuzuia Usafirishaji Binadamu nchini. Kushoto ni Katibu wa Kamati ya Kuzuia Usafirishaji Haramu wa Binadamu, Seperatus Fella. Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Picha na  Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Mkurugenzi wa kituo cha C-sema, Michael Kehongoh, akieleza jambo juu ya shughuli wanazofanya katika kituo hicho kuunga mkono harakati za kupambana na Biashara Haramu ya Kuzuia Usafirishaji Binadamu nchini. Kushoto ni Katibu wa Kamati ya Kuzuia Usafirishaji Haramu wa Binadamu , Seperatus Fella. Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Picha na  Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.


Comments