Featured Post

TAMASHA LA USALAMA BARABARANI KUFANYIKA AGOSTI 5 MWAKA HUU UWANJA WA TAIFA

Naibu Waziri  wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na Waandishi wa Habari(hawapo pichani) kuhusu Tamasha la Usalama Barabarani linalotarajiwa kufanyika mapema mwezi wa nane,mwaka huu katika Uwanja wa Taifa,jijini Dar es Salaam,ambapo Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dk. John Magufuli.Kulia ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini,Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi,Fortunatus Musilimu. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi, Fortunatus Musilimu, akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) kuhusu Tamasha la Usalama Barabarani linalotarajiwa kufanyika mapema mwezi wa nane,mwaka huu katika Uwanja wa Taifa,jijini Dar es Salaam,ambapo Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dk. John Magufuli. Kushoto ni Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani,Mhandisi Hamad Masauni. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waandishi wa  Habari wakimisikiliza Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, ambae pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni wakati wa Mkutano uliohusu Tamasha la Usalama Barabarani linalotarajiwa kufanyika mapema mwezi wa nane,mwaka huu katika Uwanja wa Taifa, Jijini  Dar es Salaam, ambapo Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dk. John Magufuli.Kushoto ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini,Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi,Fortunatus Musilimu. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI-WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

Comments