- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Unknown
on
- Get link
- X
- Other Apps
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akipitia mkataba wa
makubaliano katika mkutano wa kwanza wa Mawaziri wa usafirishaji na uchukuzi mkoani
Kigoma,kuhusu kushirikiana katika miradi ya maendeleo ya pamoja kati ya nchi ya
Tanzania, Burundi, Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akisaini mkataba wa
makubaliano mkoani Kigoma, kuhusu kushirikiana katika miradi ya maendeleo ya
pamoja kati ya nchi ya Tanzania, Burundi, Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Kongo (DRC).
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akizungumza na
waandishi wa habari mkoani Kigoma, katika mkutano wa kwanza uliohusisha Mawaziri
wa uchukuzi kutoka nchi ya Tanzania, Burundi, Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia
ya Kongo (DRC). Mkutano huo umejadili ushirikiano katika miradi
ya maendeleo ya pamoja baina ya nchi hizo.
Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa amesaini mkataba wa ushirikiano
katika miradi ya pamoja inayohusu masuala ya usafirishaji na uchukuzi, lengo
likiwa ni kuleta maendeleo na kukuza uchumi katika nchi wanachama.
Akizungumza mara baada
ya kusaini mkataba huo mkoani Kigoma, Waziri Mbarawa amesema kuwa mkataba huo ambao
unahusisha nchi ya Tanzania, Uganda, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Kongo (DRC), unalenga kuhuisha fursa za kiuchumi katika Ukanda wa Ziwa
Tanganyika.
Amesema pamoja na
mambo mengine, Mawaziri wa Muungano wa Uchukuzi na Usafirishaji wa Nchi za
Ukanda wa Ziwa Tanganyika (LTITS), wamepokea ripoti ya wataalam inayooelekeza
utekelezaji wa miradi kwa nchi wananchama ili kufikia malengo yanayotarajiwa.
“Tumeelekeza Sekretarieti
ya ukanda huu kuunganisha pamoja rasilimali kutoka nchi wanachama, sekta
binafsi na wadau wa maendeleo ili miradi inayotekelezwa kwa pamoja iweze
kukabiliana na changamoto za usafirishaji zilizopo katika ukanda wa Ziwa
Tanganyika”, amesema Profesa Mbarawa.
Mawaziri hao Bagiire
Aggrey Henry kutoka Uganda, Eng. Jean Bosco Ntunzwenimana kutoka Burundi na
Katibu wa Sekretarieti wa Ukanda huo Capt. Dieudonne Dukundane kwa pamoja wamepongeza juhudi zinazofanywa na Serikali ya
Tanzania hususan katika ujenzi wa Reli ya Kati kwa kiwango cha kisasa (Standard
Gauge), na uboreshaji wa huduma katika Mamlaka ya Bandari Tanzania ambavyo kwa
pamoja vitaunganisha Ukanda huo.
“Kukamilika kwa reli
ya Kati ya kisasa hadi Uvinza- Msongati kutawezesha reli hiyo kuunganisha
vizuri nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Burundi na hivyo
kuchochea maendeleo katika Ukanda wa Ziwa Tanganyika”, amesisitiza Waziri wa
Uchukuzi wa Burundi, Eng. Jean Bosco Ntunzwenimana.
Mawaziri hao
wameelezea umuhimu wa uboreshaji wa huduma za uchukuzi katika Bandari ya Ziwa
Tanganyika ili iwe na viwango vya kimataifa na kuunganisha vizuri ukanda huo.
Mkutano huo ni mkakati
wa nchi za Ukanda wa Ziwa Tanganyika wenye lengo la kuboresha huduma za
usafirishaji na uchukuzi katika nchi hizo ili kukuza uchumi na kurahisisha
huduma za usafirishaji wa abiria na mizigo.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
Comments
Post a Comment