Mbunge wa Pangani
Jumaa Hamidu Awesso aliyevaa shati la bluu akiwa na baadhi ya viongozi
wa simba mapema leo wakati alipowatembelea vijana wake wanaofanyiwa
majaribio na klabu hiyo.
Kijana
Abdallah Hamisi Abeid maarufu kam Jr kutokea Pangani
aliyechaguliwa kujiunga na klabu ya Simba B
Kijana
Abdallah Hamisi Abeid akiwa na wenzake waliofanyiwa majaribio na Simba
B
Na Mohammed Hammie
Mbunge wa
jimbo la Pangani Jumaa Hamidu
Awesso hatimae amefanikisha ndoto za kijana Abdallah Hamisi
Abeid maarufu kama Jr kutokea Pangani Mjini kwa kuchaguliwa kuchezea
klabu ya Simba B baada ya kupenya katika mchujo.
Akizungumza na
waandishi wa habari jijini Dar es salaam leo, Mheshimiwa Awesso amesema
kuwa, kufanikiwa kwa kijana huyo ndio mwanzo wa kuibua vijana wengine
wenye vipaji vya soka katika jimbo lake la Pangani.
Awali mbunge
huyo kijana aliandaa vijana wanne kwa ajili kuwapeleka kwenye klabu hiyo
kongwe kwa ajili ya kufanyiwa majaribio, kwa lengo la kufanikisha ndoto
zao za kuchezea klabu kubwa hapa nchini.
"Nilichukua vijana
wanne na kuwaleta hapa Dar es salaam kwenye klabu ya Simba ambao ni
Abdallah Hamisi aliyepata nafasi, wengine ni Bakari Mohammed, Gasper
Anthony na Sueli Salum ambao kwa sasa naendelea kuwafanyia mpango wa
kufanya majaribio kwenye klabu nyengine" amesema Mheshimiwa Awesso.
Kijana
Abdallah Hamisi au Jr ambaye wengi humfananisha na Mbwana Samatta,
anatokea katika klabu ya Blackburn ya Pangani Mjini ambayo imekuwa na
mashabiki wengi kutokana na kujaa vijana wengi wenye vipaji vya kusukuma
kabumbu.
"Kabla sijajiunga na Black Burn nilitokea klabu
nyengine ya Pangani United, kwa hiyo sina uzoefu mkubwa sana lakini nina
uwezo wa kipekee na ndio maana nimechaguliwa kujiunga na Simba B"
anasema Jr.
"Pia namshukuru sana Mbunge wangu Jumaa Awesso kwa
jitihada zake za kutukusanya sisi vijana wenye vipaji na kuhakikisha
tunafikia ndoto zake, kwa kweli ni mbunge pekee ambaye anaonyesha
mapenzi ya dhati kwa wananchi wake, sio tu katika soka hata katika mambo
mengine ya kimaendeleo" amesema Jr.
Jr amewataka pia vijana
wengine wilayani Pangani na Tanzania kwa ujumla kuwa na uthubutu na
kujiamini pindi wanapopatiwa fursa ya kuonyesha vipaji vyao mahala
ambapo pana uwezekano wa kutoka kimaisha.
Pia amewataka vijana
wenzake ambao hawakupata nafasi hiyo, kutokata tamaa na badala yake
waendelee kufanya majaribio kwenye vilabu vyengine vikubwa hapa
nchini.
Mbunge
Jumaa Awesso ameahidi kuendelea kuibua vijana wengine wenye vipaji
kutokea Pangani pasipo kujali itikadi, ili vijana hao wawe chachu ya
kuitangaza wilaya hiyo na kuiletea heshima hata ikibidi katika anga za
kimataifa.
Mohammed Hammie Rajab
PR Manager/Radio
Editor
Uzikwasa/Pangani Fm
Radio
P.o Box 1,
Pangani
Comments
Post a Comment