- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Unknown
on
- Get link
- X
- Other Apps
Kamishna
Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye, akimkabidhi
zawadi Balozi wa Kuwait nchini, Jasem Al-Najem (kushoto), baada ya mazungumzo
na Balozi huyo alipotembelea Makao Makuu ya Jeshi hilo, jjini Dar es Salaam
leo. Katika Kikao hicho Balozi huyo aliahidi kushirikiana na Jeshi
kubadilishana utaalamu katika masuala ya kukabiliana na majanga mbalimbali. Picha
na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.
Kamishna
Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye, akizungumza na Balozi
wa Kuwait nchini, Jasem Al-Najem (Wakwanza kulia) alipotembelea Makao Makuu ya
Jeshi hilo jijini Dar es Salaam leo. Katika Kikao hicho Balozi huyo aliahidi
kushirikiana na Jeshi hilo kubadilishana utaalamu katika masuala ya kukabiliana
na majanga mbalimbali. Wengine ni Maafisa Waandamizi wa Jeshi hilo. Picha na
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji
Balozi
wa Kuwait nchini, Jasem Al-Najem, akizungumza wakati wa kikao na Kamishna Jenerali
wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye (katikati) na Maafisa
Waandamizi wa Jeshi hilo, alipotembelea Makao Makuu ya Jeshi jijini Dar es Salaam leo. Katika Kikao hicho Balozi
huyo aliahidi kushirikiana na Jeshi hilo kubadilishana utaalamu katika masuala
ya kukabiliana na majanga mbalimbali.Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.
Kamishna
Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na
Uokoaji, Thobias Andengenye, akiongozana
na Balozi wa Kuwait nchini, Jasem
Al-Najem (kulia) alipowasili Makao Makuu
ya Jeshi hilo jijini Dar es Salaam leo
kwa mazungumzo yaliyohusisha ushirikiano kati ya Majeshi ya nchi hizo
kubadilishana Utaalamu katika masuala ya kukabiliana na majanga mbalimbali.Picha
na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji
Balozi
wa Kuwait nchini, Jasem Al-Najem, akisalimiana na Maafisa wa Jeshi la Zimamoto
na Uokoaji wakati alipowasili Makao Makuu ya Jeshi hilo jijini Dar es Salaam leo kwa mazungumzo na Kamishna
Jenerali wa Jeshi hilo, Thobias Andengenye(hayupo pichani). Katika Kikao hicho
Balozi huyo aliahidi kushirikiana na Jeshi hilo kubadilishana utaalamu katika
masuala ya kukabiliana na majanga mbalimbali.Picha na Jeshi la Zimamoto na
Uokoaji.
Kamishna
Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye, akiwa katika
picha ya pamoja na Balozi wa Kuwait nchini, Jasem Al-Najem (katikati) baada ya kikao
cha mazungumzo yaliyohusisha
ushirikiano kati ya Majeshi ya nchi hizo katika
kubadilishana Utaalamu katika masuala ya kukabiliana na majanga
mbalimbali.Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji
IMEANDALIWA
NA KITENGO CHA HABARI NA ELIMU KWA UMMA-MAKAO MAKUU YA JESHI LA ZIMAMOTO NA
UOKOAJI
Na Mwandishi Wetu
Jeshi la Zimamoto na
Uokoaji Nchini, liko katika mkakati wa kuingia ushirikiano na Serikali ya Kuwait
katika shughuli zake za kukabiliana na majanga ya moto ikiwa ni juhudi zake
katika kuyafikia maeneo mengi nchini.
Akizungumza
alipotembelea Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji jijini Dar es salaam,
Balozi wa Kuwait Nchini, Jasem Al-Najem, alisema serikali ya Kuwait ipo tayari
kubadilishana mafunzo na kutoa msaada wa vifaa kwa Jeshi hilo.
“Ni vema tukatengeneza
mpango ambao wataalam wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kutoka
nchini Tanzania wataweza kubadilishana uzoefu na wataalamu kutoka nchini Kuwait
kwa ajili ya kujifunza mbinu mbalimbali za kukabiliana na majanga pindi
yanapotokea, ’’ Alisema Balozi huyo.
Akizungumza wakati wa
kikao hicho, Kamishna Jenerali wa Jeshi
la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye alimshukuru kwa kumtembelea na kusema
kuwa ujio wa balozi huyo, umefungua ukurasa mpya kwa upande wa misaada na
mafunzo kwa Askari wa Jeshi hilo, kwani watapata fursa ya kubadilishana uzoefu
na kuongeza tija kwa Jeshi lake.
“Tutapata nafasi ya
kubadilishana uzoefu na kupata mafunzo kutoka Nchi ya Kuwait na kuongeza
ufanisi katika majukumu yetu ya kila siku, lengo ikiwa ni kukabiliana na
majanga mbalimbali yakiwemo ya moto,’’ alisema Kamishna Jenerali.
Katika kikao hicho
Balozi wa Kuwait, Nasem Al-Najem alipokea
taarifa ya changamoto zinazolikabili jeshi hilo ikiwemo uhaba wa
vitendea kazi huku akiahidi kuzifanyia kazi na akisisitiza mchakato wa kusaini
makubaliano ya hiari ukamilike kwani utakuwa msaada wa kutekeleza kwa haraka program
za mafunzo ya muda mfupi.
Comments
Post a Comment