Mwenyekiti wa Kijiji cha Kakola, wilaya ya Msalala mkoani Shinyanga, Emmanuel Bombeda, akiongoza kongamano la wananchi wa kijiji hicho lililokuwa na ajenda ya kutoka na maazimio ya kudai fidia zao kutoka mgogi wa Bulyanhulu.
Wakazi wa Kijiji cha Kakola, Kata ya Bulyanhulu, Wilaya ya Msalala
mkoani Shinyanga wameazimia kufanya maandamano yasiyo na ukomo
kushinikiza mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu kuwalipa fidia zao. Wakizungumza kwenye kongamano la Kijiji hicho lililofanyika jana juni
20,2017, wakazi hao wamepanga kupeleka kero zao Jijini Dar es salaam kwa
Rais John Pombe Magufuli pamoja na kufanya maandamano ya kufunga
barabara kushinikiza kulipwa fidia zao. "Kongamano la leo ni kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Dkt.John Pombe Magufuli kwa kugundua kwamba tulikuwa tunaibiwa
kwa muda mrefu. Tangu mwaka 1996 mpaka leo sisi tumeibiwa tu,
hatujapata haki hata moja. Hakuna huduma za jamii zinazotambulika ambazo
zimefanywa na mgodi". Alisema mchimbaji mdogo Aziz Mbaga. Mjumbe wa serikali ya Kijiji cha Bulyanhulu, Mhidini Mfwanguro alisema
maazimio ya wananchi wa Kijiji hicho ni fidia kwa wafukiwa na waathirika
wa Bulyanhulu mwaka 1996 pamoja na waathirika wengine wakiwemo
wafanyakazi waliochishwa kazi kwa kuumia kazini bila kulipwa na kwamba
watawasilisha madai hayo kwa wamiliki wa mgodi huo, kampuni ya Barrick
Gold Mine. Mwenyekiti wa kijiji cha Kakola, Emmanuel Bombeda amesema kijiji hicho
kilikuwa na vitongoji tisa lakini vitongoji vinne vilichukuliwa na mgodi
wa Bulyanhulu bila wananchi kulipwa fidia huku nyumba zao zikibomolewa. "Tunataka maandamano ya kufunga barabara tulipwe, siwezi kufanya
maandamano halafu tusambae, nataka maandamano kama tuliyofanya umeme
ukaletwa kijiji cha Kakola, maandamano kama yale ya Musoma ya kupigwa
mabomu lakini tulipwe". Alisema Bombeda.
Diwani wa Kata ya Bulyanhulu, John Kiganga alikiri wananchi wengi kukosa
stahiki zao baada ya kuondolewa kwenye maeneo yao ili kupisha uwekezaji
wa mgodi wa Bulyanhulu na kusisita kwamba wanapaswa kulipwa fidia zao
maana fomu za tathimini zipo na kwamba hata wale waliolipwa fidia,
walilipwa kinyume na tathimini ambapo mmoja wa wananchi aliyepaswa
kulipwa shilingi milioni 375 alilipwa shilingi laki tano. Wananchi wa Kijiji cha Kakola wanalalamika kutolipwa fidia zao baada ya
maeneo na makazi yao kuchukuliwa na mgodi wa Bulyanhulu, wengine ndugu
zao kufukiwa kwenye mashimo, waliokuwa wafanyakazi wa mgodi huo kutaka
stahiki zao baada ya kuumia kazini na kuachishwa kazi pamoja na kutaka
huduma bora za kijamii ikiwemo barabara za lami na vituo vya
afya/hospitali kutokana na uwepo wa mgodi.
Diwani wa Kata ya Bulyanhulu, John Kiganga, akizungumza kwenye kongamano hilo. Mkazi wa Kakola, Erasto Mapato, akizungumza kwenye kongamano hilo. Mjumbe serikali ya Kijiji cha Kakola, Jedidiah Kitundu, akizungumza kwenye kongamano hilo. Mkazi wa Kakola, John Mutemankamba, akizungumza kwenye kongamano hilo. Mchimbaji mdogo wa dhahabu, Aziz Mbaga, akizungumza kwenye kongamano hilo. Mkazi wa Kakola, Erasto Mapato, akizungumza kwenye kongamano hilo. Mkazi wa Bulyanhulu, Waziri Bakari, akizungumza kwenye kongamano hilo. Mkazi wa Bulyanhulu, akizungumza kwenye kongamano hilo. Mkazi wa Bulyanhulu akizungumza kwenye kongamano hilo. Mzee Nikodemas Mabe ambaye ni Mwenyekiti wa wachimbaji wadogo Bulyanhulu akielezea kero zao.
Magdalena Lusana akielezea kero za Bulyanhulu Mzee Geremiah Wangaluke akielezea kero za Bulyanhulu Kijana Masumbuko Kafula mkazi wa Bulyanhulu akieleza madhira waliyoyapata kutokana na wawekezaji Mama Melania Baesi akieleza juu ya wanae kupoteza maisha kwenye sakata la Bulyanhulu Wakazi wa Bulyanhulu wilayani Msalala Wakazi wa Bulyanhulu wilayani Msalala Kongamano la wananchi wa kijiji cha Kakola lililokuwa na ajenda ya kutoka na maazimio ya kudai fidia zao kutoka mgogi wa Bulyanhulu.
Comments
Post a Comment