Mwakilishi wa Kamishna wa Ardhi
Msaidizi Kanda ya
Kaskazini, Ardhi Mwandamizi Thadeus Riziki akizungumza na
waandishi wa habari kuhusu Baraza
la Ardhi Mkoani Tanga kupokea
mashauri 18 yenye thamani ya Bilon 1.1 ambayo yamefikishwa
kutokana wamiliki wa nyumba
,makazi na viwanda kushindwa kulipa kodi ya ardhi kwa wakati.
Afisa Ardhi
Mteule Halmashauri ya
jiji la Tanga Straton Thobias akielezra mkakati wa mwaka wa fedha wa 2016/7
halmashauri imeweka lengo la kukusanya
kodi ya ardhi kiasi cha shilingi bilioni 2.5 ambapo hadi sasaimefanikiwa
kukusanya shilingi bilioni 2.3
 |
Mwanasheria wa Ofisi ya Kamishina wa Ardhi Kanda ya Kaskazini Rosemery Mshana akiwataka wamiliki wa ardhi
wanatakiwa kilipa kodi bila shuruti na kwamba kinyume chake watafikishwa
mahakamani mujibu wa kifungu cha 50 cha sheria
ardhi namba nne(4 |
Mashauri 18 ya madai ya kodi ya
ardhi yenye thamani ya shilingi bilioni 1.1 yamewasilishwa katika
Baraza la ardhi na nyumba wilaya ya Tanga ikiwa ni mkakati
wa Serikali
wa kuwabana wamiliki wa viwanja wanao kwepa kulipa kodi.
Akizungumza
mara baada ya kuwasilishwa kwa mashuari hayo mwakilishi wa afisa ardhi
msaidizi kanda ya kazikazini Thadeus Riziki amesema hatua ya kuwafikisha
mahakamani wamiliki wa viwanja hivyo ni kupata kibali kitakacho
wezesha wizara kulipwa makusanyo ya madeni.
Amesema baada ya
halmashauri kuwapelekea wamiliki hati ya madai na kushindwa kulipa hatua
inayofuata ni kuwafikisha mahakamani ili kupata ridhaa ya kisheria ya
kukamata mali za wadaiwa.
Kwa upande wake afisa ardhi mteule
Halmashauri ya jiji la Tanga Straton Thobias amesema katika mwaka wa
fedha wa 2016/7 halmashauri imeweka lengo la kukusanya kodi ya ardhi
kiasi cha shilingi bilioni 2.5 ambapo hadi sasaimefanikiwa kukusanya
shilingi bilioni 2.3
Akizungumzia zoezi hilo mwanasheria ofisi ya
kamishina wa ardhi Rosemery Mshana amesema wamiliki wa ardhi
wanatakiwa kilipa kodi bila shuruti na kwamba kinyume chake watafikishwa
mahakamani mujibu wa kifungu cha 50 cha sheria
ardhi namba nne(4)
habari kwa hisani ya blog ya
Kijamii ya Tanga Raha.
Comments
Post a Comment