- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
MKUU wa
Wilaya ya Temeke jijini Dar es salaam Mhe
Felix Lyaviva akizungumza wakati wa semina
ya mamlaka ya Mawasiliano Tanzania kuhusu hali
ya sekta ya mawasiliano na utangazaji nchini
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Mhandisi James Mitayakingi Kilaba akitoa maelezo kuhusu semina
ya mamlaka ya Mawasiliano Tanzania kuhusu hali
ya sekta ya mawasiliano na utangazaji nchini
Baadhi ya washiriki wakimsikiliza Mkuu wa
Wilaya ya Temeke jijini Dar es salaam Mhe
Felix Lyaviva akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina
ya mamlaka ya Mawasiliano Tanzania kuhusu hali
ya sekta ya mawasiliano na utangazaji nchini
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akifatilia kwa makini semina
ya mamlaka ya Mawasiliano Tanzania kuhusu hali
ya sekta ya mawasiliano na utangazaji nchini
Mrakibu
msaididzi wa Polisi Makao Makuu kitengo cha Makosa ya mitandao Joshua Mwangasa Akielezea takwimu na jinsi ya kudhibiti makosa ya mitandao ya kijamii nchini.
Meya wa Manispaa ya Ubungo Ndg Boniface Jacobo (Kulia) akifatilia kwa makini semina
ya mamlaka ya Mawasiliano Tanzania kuhusu hali
ya sekta ya mawasiliano na utangazaji nchini
Katibu Tawala wa Manispaa ya Kinondoni Bi Gift Msuya akifatilia kwa makini semina
ya mamlaka ya Mawasiliano Tanzania kuhusu hali
ya sekta ya mawasiliano na utangazaji nchini
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akifatilia kwa makini semina
ya mamlaka ya Mawasiliano Tanzania kuhusu hali
ya sekta ya mawasiliano na utangazaji nchini
Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es salaam Bi Theresia Mbando akifatilia kwa makini semina
ya mamlaka ya Mawasiliano Tanzania kuhusu hali
ya sekta ya mawasiliano na utangazaji nchini
Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es salaam Mhe Isaya Mwita akitoa mtazamo wake wakati wa semina
ya mamlaka ya Mawasiliano Tanzania kuhusu hali
ya sekta ya mawasiliano na utangazaji nchini
Na Mathias Canal, Dar es salaam
MKUU
wa Wilaya ya Temeke jijini Dar es salaam Mhe
Felix Lyaviva amewaagiza Wakurugenzi wa Halmashauri za Manispaa za
Kigamboni, Ilala, Temeke, Kinondoni na Ubungo kuanzisha daftari la wakazi
katika kila Mtaa katika Jiji la dar es salaam.
Alisema kuwa ili kupunguza uhalifu katika
Mkoa wa Dar es salaam ni vyema kuwatambua wananchi wote na mahali wanapoishi
ikiwemo kubaini wageni wote wanaowasili katika Jiji hilo na mahali wanapofikia.
Ametoa agizo hilo wakati akihutubia kwa niaba
ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul Makonda katika ufunguzi wa semina ya
mamlaka ya Mawasiliano Tanzania ili kuwaelimisha watumiaji wa Intaneti wapatao
milioni 20 sambamba na watumiaji wa simu za mikononi wapatao milioni 40 kuwa na
matumizi bora ya simu za mikononi na mitandao ya kijamii.
Katika Semina hiyo wadau wamekumbushwa namna
ya kuelewa Zaidi hali ya sekta ya mawasiliano na utangazaji, Umuhimu wa anuani
za makazi na Post-kodi kwa maendeleo ya Taifa, Faida za huduma ya kumiliki na
kuhama na namba ya simu ya kiganjani na mwelekeo wa Teknolojia na huduma za
mawasiliano na utangazaji hapa nchini.
Mhe Lyaviva
alisema kuwa pamoja na faida kubwa
inayopatikana kutokana na kukua kwa sekta ya mawasiliano nchini ambayo
inawezesha ukuaji wa kasi wa sekta nyingine, kumekuwepo na watu wachache katika
jamii ambao wanatumia fursa hiyo vibaya hivyo kusababisha usumbufu kwa watu
binafsi na jamii kwa ujumla.
Alisema kuwa wapo wanaotumia simu na mitandao
ya kijamii kupanga mikakati ya uhalifu huku wengine wakitumia simu na mitandao
hiyo kukashifu na kutukana watu wengine.
Mhe Lyaviva alisema kuwa lengo la serikali ni
kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji katika sekta ya Mawasiliano na utangazaji
ili kutoa fursa za ajira na kuwezesha huduma hizo kuwafikia wananchi wote kwa
gharama nafuu.
Naye Mrakibu msaididzi wa Polisi Makao Makuu
kitengo cha Makosa ya mitandao Joshua
Mwangasa akiwasilisha mada kuhusu makosa ya mitandao ya kijamii alisema
kuwa kuna njia nyingi zinazotumiwa ili kufanya uhalifu ikiwemo mitandao ya
kijamii hivyo amewasihi watumiaji wote wa mitandao ya kijamii nchini kubadili
mara kwa mara Namba za siri (Password).
Alisema kuwa kufanya hivyo ni miongoni mwa
njia nzuri ya kuepuka kuingiliwa na wahalifu katika mawasiliano yao kwani kwa
kiasi kikubwa maisha ya binadamu yanaenda kubadilika kutokana na teknolojia
Akitoa takwimu na jinsi ya kudhibiti makosa
hayo kwa viongozi wa Mkoa wa Dar es salaam, Mwangasa alisema kuwa Mwaka 2016
makosa ya mitandao ya kijamii yameongezeka kufikia 9441 ukilinganisha na Mwaka
2015, ambapo amezitaja sababu za kuongezeka kwake kuwa ni pamoja na ongezeko la
uelewa wa wananchi na hatimaye kutoa taarifa za matukio hayo katika vituo
mbalimbali vya Polisi nchini
Comments
Post a Comment