- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
Msichana wa
Kichina alikuwa amesimama kwenye kizingiti cha mlango wa chumba kilichotazamana
na changu. Alikuwa na umbile dogo, lakini lililojengeka vyema: nywele zake
maridadi nyeusi zilikuwa zimesukwa na kuning’inia shingoni. Alikuwa amevalia
lauzi nyeupe na sketi ya buluu nzito. Alivutia kumtazama bila kuwa mrembo.
Alikuwa akinitazama kana kwamba alikuwa akisubiri kwa muda wote kwamba
nitatokea.
“Hello, mheshimiwa,”
akasema huku tabasamu pana likiwa limechanua usoni mwake. “Naitwa Leila. Jina
lako nani?”
Nikalipenda
tabasamu lake na nikayapenda meno yake meupe.
“Nelson Ryan,” nikamwambia,
nikifunga mlango wangu. “Unaweza kuniita Nelson. Unaishi hapa?”
“Ndiyo.” Macho
yake meusi ya kirafiki yakaanza kunisawiri. “Ni wanaume wachache wa Kimarekani
wanaoishi hapa. Wewe unaishi hapa?” akaniuliza.
“Ndiyo maana
yake, umekuwepo hapa muda mrefu?”
“Miezi kumi na
nane.” Alikuwa na lafudhi ya kipekee. Ilibidi niwe makini kuweza kuelewa
alichokuwa anasema. Alinitazama kwa mtazamo ule unaomaanisha alichokimaanisha.
“Ukitaka kufanya mapenzi, utakuja kunichukua?”
Nilishtushwa kwa
muda, halafu nikafanikiwa kutabasamu.
“Nitakumbuka,
lakini usinitegemee sana.”
Mlango
ukafunguliwa mbele kabisa ya korido na mtu mmoja mfupi ambaye angeweza kuwa
Mtaliano au Mfaransa akatoka nje. Akaja haraka upande wangu, bila kunitazama.
Alifuatiwa na msichana wa Kichina. Sidhani kama alikuwa na miaka zaidi ya kumi
na sita, lakini ni vigumu kujua kwa watu hawa wenye maumbile madogo. Akanitazama
kwa mvuto wakati akinipita. Mpaka wakati huo nikatambua ni hoteli gani hiyo
niliyokuwa nimefikia.
Leila akaweka
mikono yake mizuri chini ya matiti yake madogo na kuyapandisha juu.
“Ungeweza kuja
kwangu sasa hivi?” akauliza kwa utulivu.
“Siyo wakati huu,”
nikamwambia. “Nina kazi. Pengine wakati mwingine.”
“Wanaume wa
Kimarekani kila wakati wako bize,” akasema. “Labda usiku, au?”
“Nitakwambia.”
Akakata tamaa.
“Hiyo
haimaanishi chochote, unaweza kuja au usije.”
“Ndiyo maana
yake,” nikamwambia. “Kwa sasa kuna mambo ninayafanya,” na nikaelekea kwenye
ukumbi wa mapokezi ambako karani wa mapokezi mzee wa Kichina aliketi akiwa
ametulia kama Buddha.
Nikateremka
ngazi hadi mtaani kulikojaa watu, kelele na joto kali. Kijana wa mkokoteni
akaja moja kwa moja kunifuata.
“Makao makuu ya
polisi,” nikamwambia mara tu baada ya kuingia kwenye mkokoteni wake wa abiria.
Akaondoka
akikimbia. Baada ya kuondoka umbali wa yadi mia mbili au mia tatu, nikagundua
kosa nililolifanya kuchukua usafiri wa aina ile. Magari makubwa, ya kati na
malori hayakuwathamini wenye mikokoteni. Kila sekunde nikahisi kwamba
nitagongwa na lori au kwa gari kubwa lenye kasi la Kimarekani. Nikashusha pumzi
baada ya kufika nje ya Kituo Kikuu cha Polisi cha Hong Kong, nikishangaa kwamba
bado nilikuwa katika hali salama.
Baada ya kueleza
kilichonipeleka kwa sajini aliyekuwa mapokezi, hatimaye nikaelekezwa kwenye
ofisi ndogo, safi ambako Inspekta Mkuu mwenye nywele nyeupe na sharubu za
kijeshi akanitazama kwa jicho lisilo la kirafiki wakati akinielekeza kwenye
kiti.
Nikamweleza mimi
ni nani naye akanieleza jina lake. Jina lake alikuwa MacCarthy na alizungumza
lafudhi ya Kiskochi.
“Jefferson?” Akazirudisha
nywele zake kwa nyuma kwa kuinua kichwa na kunyanyua mtemba wa Dunhill
ulioonekana kuzeeka. Wakati alipoanza kuujaza tumbaku, akaendelea, “Nini
kilichokuvutia sana? Tayari nimekwishashughulikia suala hilo hilo baada ya
kuulizwa na polisi wa Jiji la Pasadena kuhusu huyo mtu. Yeye ni nani kwako?”
Nikamwambia
nilikuwa namwakilisha Mzee J. Wilbur Jefferson.
“Ninahitaji
kupata taarifa za kutosha kuhusu mwanaye na mkewe wa Kichina kwa kadiri
itakavyowezekana,” nikamwambia. “Chochote utakachoniambia kinaweza kusaidia.”
“Ubalozi wa
Marekani unaweza kusaidia zaidi,” akasema, akiwasha mtemba wake. Akapuliza
moshi wenye harufu ya tumbaku ghali kwangu. “Sifahamu mambo mengi kumhusu.
Aliuawa kwenye ajali ya gari. Nadhani umesikia kuhusu hilo?”
“Ajali hiyo
ilitokeaje?”
Akapandisha
mabega yake.
“Alikuwa akiendesha kasi kwenye barabara yenye utelezi. Hakukuwa
na cha ziada cha kuchukua wakati tulipomkuta. Alikuwa ndani ya gari ambalo
liliungua moto baada ya kupata ajali.”
“Hakuwa na mtu
yeyote?”
“Hapana.”
“Alikuwa
anaelekea wapi?”
MacCarthy akaanza
kunitazama kwa udadisi.
“Sifahamu. Ajali
ilitokea yapata kilometa tano nje ya Kowloon katika eneo la New Territories. Pengine
alikuwa anakwenda mahali.”
“Nani
aliyemtambua?”
Akajiweka sawa,
akionyesha utulivu wa kutosha.
“Mke wake.”
“Unaweza
kunieleza kidogo historia yake? Alikuwa anapata riziki kwa kazi gani?”
“Sidhani kama
ninaweza.” Akatoa mtemba mdomoni mwake na kutazama kitezo cha majivu. “Hakuwa
mtu aliyenisumbua kwa bahati nzuri. Alijitahidi kuwa mbali nasi. Hapa
hatuwafuatilii watu shughuli zao mpaka wanapofanya makosa na Jefferson alikuwa
makini asifanye hivyo. Mara kadhaa tulikuwa tukipata taarifa zake hapa na pale.
Hakuwa raia mwema. Hakuna mashaka yoyote kwamba alikuwa akitegemea mapato
haramu ya mkewe, lakini hapa pia, hatuingilii maisha ya raia wa Marekani, kama
nitaliweka sawa hilo.”
“Taarifa zozote
kuhusu mwanamke?”
Alivuta moshi na
kuonekana kuchoshwa.
“Alikuwa kahaba,
ndio ukweli wenyewe. Hili ni tatizo tunalojitahidi kupambana nalo, lakini siyo
rahisi. Hawa wasichana wakimbizi wanaishi kwa taabu kupata fedha: ukahaba ndiyo
njia rahisi zaidi kwao. Taratibu tunasafisha mji, lakini ni kazi ngumu.”
“Najaribu
kufikiria ni kwa nini aliuawa.”
Akapandisha
mabega yake.
“Siwezi kusaidia
kwa hilo.” Akatazama rundo la karatasi zilizokuwa kwenye dawati lake. “Nimetoa
taarifa zote nilizonazo kuhusu hawa wawili kwa Luteni Retnick. Hakuna cha ziada
ninachoweza kuongeza.”
Hapa tafsiri
yake ilionekana kwamba baada ya Retnick, mimi ni mtu mwingine niliyepewa
taarifa hizo. Nikasimama.
“Sawa, asante.
Wacha ninuse mitaani. Pengine ninaweza kupata zaidi.”
“Sina uhakika.” Akazivuta
karatasi upande wake. “Kama kutakuwa na lolote ninaloweza kulifanya. . . .”
Itaendelea
kesho…
Comments
Post a Comment