- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
RAIS DKT. MAGUFULI AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA RELI YA KISASA STANDARD GAUGE KUTOKA DAR HADI MOROGORO
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na
Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa pamoja na Mkewe Mama Janeth Magufuli akikata
utepe kuashiria uzinduzi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa Standard Gauge itakayoanzia
jijini Dar es Salaam hadi mkoani Morogoro na baadaye kuendelea hadi mikoa ya Kigoma
na Mwanza.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na
Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akiweka jiwe la msingi Ujenzi wa Reli ya
Kisasa Standard Gauge itakayoanzia jijini Dar es Salaam hadi mkoani Morogoro na
baadaye kuendelea hadi Kigoma na Mwanza.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia majina ya baadhi ya wataalamu
mbalimbali waliohusika katika mchakato wa Ujenzi huo wa Reli ya Kisasa Standard
Gauge itakayoanzia jijini Dar es Salaam hadi mkoani Morogoro na baadaye
kuendelea hadi Kigoma na Mwanza. Wakwanza kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa
kampuni hodhi ya Rasilimali za Reli (RAHCO) Masanja Kadogosa akiwa ameshika
majina hayo.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli
akichota mchanga na kuweka kama ishara ya kushiriki katika ujenzi huo wa Reli ya
Kisasa Standard Gauge itakayoanzia jijini Dar es Salaam hadi mkoani Morogoro na
baadaye kuendelea hadi Kigoma na Mwanza
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia kibao cha jiwe la msingi cha
Ujenzi wa Reli ya Kisasa Standard Gauge itakayoanzia jijini Dar es Salaam hadi
mkoani Morogoro na baadaye kuendelea hadi Kigoma na Mwanza
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na
Mawasiliano Profesa Makame Mabarawa, Mama Janeth Magufuli wakimsikiliza Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa RAHCO Masanja Kadogosa wakati akielezea kuhusu ujenzi wa
Reli ya Kisasa Standard Gauge itakayoanzia jijini Dar es Salaam hadi mkoani
Morogoro na baadaye kuendelea hadi Kigoma na Mwanza
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amechuchumaa kwenye mfano wa Reli ya
Kisasa (SGR) na Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame
Mabarawa, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa RAHCO Masanja Kadogosa, Mwenyekiti wa
Kamati ya Kudumu ya Miundombinu Profesa Norman Sigala mara baada ya kuweka jiwe
la msingi la ujenzi wa Reli hiyo, wengine katika picha ni Mke wa Rais Mama
Janeth Magufuli pamoja na Hawa Ghasia
(Mb)
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na
Mawasiliano Profesa Makame Mabarawa wakati akipita katika katika ya mfano wa
Reli hiyo itakayojengwa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wananchi waliohudhuria
sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi Ujenzi wa Reli ya Kisasa Standard Gauge
itakayoanzia jijini Dar es Salaam hadi mkoani Morogoro na baadaye kuendelea
hadi Kigoma na Mwanza.
Mfano wa Reli hiyo ya Kisasa ya
Standard Gauge SGR itakayojengwa kuanzia Dar es Salaam hadi Morogoro na baadae
kuendelea hadi mikoa ya Mwanza na Kigoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Kaimu Mtendaji Mkuu wa RAHCO
Masanja Kadogosa wakati akielekea kuweka jiwe la Msingi ujenzi wa Reli hiyo ya
Kisasa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia kabla ya kuweka jiwe la Msingi
ujenzi wa Reli hiyo ya Kisasa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Mufti Mkuu wa Tanzania
Shekhe Abubakary Zubeiry mara baada ya kuweka jiwe la Msingi katika eneo la
Pugu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akimpongeza msanii Mrisho Mpoto mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika
ujenzi huo wa Reli ya Kisasa Pugu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU
Comments
Post a Comment