- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wajumbe wa Baraza la Uwekezaji la Korea nchini Tanzania (KICoT Corporation) leo, Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan akisisitiza jambo wakati wa mazungumzo na Wajumbe wa Baraza la Uwekezaji la Korea nchini
Tanzania (KICoT Corporation) leo, Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan akiimba wimbo wa Taifa pamoja na Mshauri Mkuu wa Baraza la Uwekezaji la Korea nchini
Tanzania (KICoT Corporation), Mhe. Balozi Mstaafu wa Korea Kusini hapa nchini Kim, Young-Hoon ambaye alimwambia Mhe. Makamu wa Rais kuwa bado anaukumbuka wimbo wa Taifa la Tanzania.
.....................................................................
Watanzania
waliosoma Nchi Korea Kusini wameunga mkono jitihada za Serikali ya awamu ya
Tano ya kujenga uchumi wa viwanda kwa kuleta wawekezaji ambao wanataka kuwekeza
katika ujenzi wa viwanda vya nguo, vifaa tiba, uzalishaji wa nishati ya umeme
wa jua, kilimo na katika sekta ya Sanaa,utamaduni na michezo.
Mwenyekiti
wa Baraza la Uwekezaji kutoka Korea Kusini hapa nchini Kakono David ametoa
kauli hiyo wakati anaongoza Ujumbe wa Baraza la Uwekezaji la Korea Kusini ambao
wamekutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa Jamahuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti
huyo amesema ujenzi wa viwanda hivyo utatoa fursa kubwa katika kukuza uchumi wa
nchi na kutoa ajira nyingi kwa Watanzania na amesisitiza kuwa kwa kuanzia
wawekezaji hao wataanza kuwekeza katika wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza.
Kwa
upande wake, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu
Hassan katika mazungumzo na ujumbe huo wa Baraza la Uwekezaji Kutoka Korea
Kusini amesema amefurahishwa na ujio wa wawekezaji hao na amewahakikishia kuwa
Serikali ya awamu ya Tano inaendelea kujenga mazingira bora ya uwekezaji ili
kazi ya ujenzi wa viwanda nchini iweze kwenda kwa kasi inayotakiwa.
Makamu wa
Rais amesema ujenzi wa viwanda unaoendelea kufanywa na wawekezaji nchini
utasaidia kuongeza pato la taifa na kutoa ajira kwa Watanzania.
Amesema
Tanzania ina maeneo mengi na mazuri kwa ajili ya uwekezaji Tanzania Bara na
Zanzibar hivyo ni wakati muafaka kwa watendaji wa sekta husika kwa ushirikiano
na serikali kujiimarisha katika kuondoa ukiritimba ili kuvutia wawekezaji
kutoka mataifa mbalimbali Duniani.
Makamu
wa Raia pia amefurahishwa na mpango wa wawekezaji hao kutoka Korea Kusini ambao
wanataka kusaidia uimarishaji wa haki za wanawake hapa nchini na amekaribisha
Jumuiya ya Wanawake kutoka Korea Kusini kuja Kufanya ziara ya kikazi hapa
nchini.
Comments
Post a Comment