- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na kumpokea mgeni wake Waziri
Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Dessalegn mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa
ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Terminal One jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na mgeni wake Waziri Mkuu wa
Ethiopia Hailemariam Dessalegn mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa ndege wa
Kimataifa wa Julius Nyerere Terminal One jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu wa Ethiopia
Hailemariam Dessalegn akipiga ngoma mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es
Salaam, Pembeni yake ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli akimpigia makofi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Waziri Mkuu wa Ethiopia
Hailemariam Dessalegn wakati nyimbo za mataifa mawili (Tanzania na Ethiopia)
zikipigwa mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius
Nyerere Terminal One jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu wa Ethiopia
Hailemariam Dessalegn akishuka kwenye jukwaa kwenda kukagua gwaride la Heshma
lililoandaliwa kwa ajili yake.
Waziri Mkuu wa Ethiopia
Hailemariam Dessalegn akikagua Gwaride la heshma lililoandaliwa kwa ajili yake.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na mgeni wake Waziri
Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Dessalegn mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar
es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wanahabari mara baada ya
kumaliza mkutano wa pamoja na Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Dessalegn
aliyeambatana na ujumbe wake Ikulu jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu wa Ethiopia
Hailemariam Dessalegn akifurahia jambo wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alipokuwa akizungumza na Wanahabari Ikulu
jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu wa Ethiopia
Hailemariam Dessalegn akizungumza na Wanahabari Ikulu jijini Dar es Salaam mara
baada ya mkutano wake na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John
Pombe Magufuli.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimtambulisha Katibu Mkuu Kiongozi Balozi
Eng. John Kijazi kwa mgeni wake Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Dessalegn
Ikulu jijini Dar es Salaam.
Shamra shamra zikiendelea wakati wa kuwasili Waziri Mkuu wa Ethiopia
Hailemariam Dessalegn katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere
Terminal 2 jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Dessalegn akikaribishwa kwa kupewa ua na mtoto Xyleen Mapunda mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Terminal One jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU
Comments
Post a Comment