- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
GAZETI LA
UWAZI: JUNI 10, 2014
MUME wa
mwimba Injili Bongo, Flora Mbasha anayedaiwa kumbaka binti wa miaka 17 ( jina
lipo), Emmanuel Mbasha ameibuka mzimamzima na kumtaka Mchungaji Kiongozi wa
Kanisa la Uzima na Ufufuo la jijini Dar, Josephat Gwajima amuachie mke wake,
yaani Flora.
Flora
Mbasha akiwa na mumewe Emmanuel Mbasha kwenye pozi la kimahaba. Akizungumza kwa
machungu kwa njia ya simu kutokea alikojihifadhi huku akionesha waziwazi hasira
juu ya hisia zake, Mbasha alisema: "Nimesika mke wangu baada ya matatizo
yetu amehamia nyumbani kwa Gwajima. Nataka mumwambie Gwajima aniachie mke
wangu, mbona ananifanyia hivyo?"
KINACHOMSHANGAZA
Mbasha
ambaye mpaka sasa hajulikani alipo, aliendelea kudai kwamba kinachomshangaza
zaidi ni kwamba, Flora amekiuka utamaduni wa Kiafrika, kwamba kama mke na mume
wamegombana kiasi cha kushindwa kuishi nyumba moja, mke anakwenda kwao lakini
hilo la Flora kukimbilia kwa Gwajima ndilo la ajabu zaidi kwake.
"Kama
kweli Flora ameshindwa kuishi nyumbani kwetu (Tabata -Kimanga) kwa nini asiende
Morogoro kwa mama yake. Au kwa nini asirudi Mwanza kwenye chimbuko la familia
ya mzee Moses Kulola?
"Yeye
badala yake amechukuliwa na Gwajima na kwenda kuishi naye nyumbani kwake. Mimi
sijapenda, sijapenda na sitapenda kamwe," alisema Mbasha. Mwimba Injili
Bongo, Flora Mbasha, wakati akiongea na Uwazi mafichoni hotelini.
ATUHUMU
MTOTO KULIPIWA ADA YA SHULE
Akiendelea
kutoa la moyoni, Mbasha alituhumu kuwa mke wake kwa sasa ana pesa nyingi licha
ya kwamba wakati matatizo ya yeye kutuhumiwa kubaka yanatokea na kuingia mitini
alimwacha hana kitu.
Anasema:
"Wakati matatizo yanatokea Flora nilimwacha mweupe. Mtoto wetu (Elizabeth)
alitakiwa kupelekwa shule, kwa hiyo ina maana hakwenda.
"Sasa
nasikia mtoto amelipiwa ada na anakwenda shule. Nani kamlipia ada mwanangu kama
si Gwajima? Mimi naumia sana, kwa nini iwe hivyo? Kama Gwajima ameamua mke
wangu kukaa kwake kwa ajili ya kumsaidia kipindi hiki cha matatizio ajue mimi
sijapenda.
"Yeye
Gwajima ana mke wake, najua hawezikusema kitu kwa sababu Gwajima ni kila kitu
lakini sijapenda."
GWAJIMA
SASA
Jumamosi
iliyopita, Uwazi lilimtafuta Mchungaji Gwajima kwa njia ya simu ambapo
alisema hataweza kuzungumza kwa sababu yupo Mikumi akielekea Dar.
Uwazi: "Sawa, lakini inadaiwa Flora yupo kwako.
Hata jijini Dar habari zimeenea kwamba yupo kwako. Mbasha mwenyewe pia amesema
mke wake yupo kwako. Unasemaje kuhusu hili?"
Gwajima: "Flora hakai kwangu na wala sijui alipo.
Hao wanaosema anaishi kwangu si wa kweli. Hata mkija kwangu hamtamkuta Flora."
UWAZI LAMSAKA FLORA
Uwazi lilianza kuingia
mitaani kumsaka mwimbaji huyo kwa kutumia vyanzo mbalimbali vya kiintelejensia.
Ilikuwa kazi kubwa sana iliyoanza saa mbili na nusu asubuhi ya Jumapili na
ilipofika saa tano, Flora alipatikana kwenye hoteli moja (jina tunalo) iliyopo
Sinza jijini Dar es Salaam. Alikuwa akijiandaa kwenda kanisani ikabidi hekima
zitumike ili aweze kutoa dakika ishirini tu za mahojiano ambapo alikubali.
KUMBE ULIANZA UGOMVI
Akizungumzia
kuhusu ugomvi katika ndoa na tuhuma ambazo mumewe anadai kuhusika nazo, Flora
alikuwa na haya ya kusema: "Mimi sina ugomvi na mume wangu Mbasha
ninampenda sana ila ninamshangaa kutoa taarifa yetu ya ndani katika vyombo vya
habari.
Mchungaji
Kiongozi wa Kanisa la Uzima na Ufufuo la jijini Dar, Josephat Gwajima.
"Nimeshtushwa
sana na kitendo hicho kwani kama ingekuwa ni ugomvi baina yake na mimi tungekaa
chini na kuyamaliza kama wanandoa. Siamini kama njia hii anayoitumia italeta suluhu,
bali itaendeleza matatizo."
KUHUSU MADAI YA UBAKAJI
"Nakumbuka
ilikuwa asubuhi ya Ijumaa ya wiki mbili zilizopita, Ima (Emmanuel ) aliniambia
nijiandae kwenda ofisini kwetu kuangalia shughuli, alinipitisha ofisini kisha
yeye akarudi nyumbani.
"Baadaye
alinipitia ofisini kurudi nyumbani. Nilimkuta binti mlalamikaji akiwa hana raha
na hali siyo nzuri, nilimuuliza tatizo ni nini hakuniambia.
"Ilipofika
Jumapili nilimwambia mume wangu twende kanisani lakini alikataa, nilimuomba
ufunguo wa gari ili mimi niende na familia, akagoma. Ndipo ugomvi ulipoanzia,
nilimuuliza umekuwaje? Mbona uko hivi? Au umechanganyikiwa? Alinijibu anataka
aondoke aniache na familia. "Baadaye akabadilika, akasema hapana
haiwezekani yeye akaondoka, bali mimi ndiyo niondoke."
ATISHIWA KUCHINJWA
"Nilimuomba
tuwaite watu wazima ili waje kutupatanisha, akaniambia nikiondoka kwenda
kutafuta watu atanichinja.
"Niliamua
kuachana naye, nilimpigia simu rafiki yangu mmoja aje anipitie na gari kwenda
kanisani, lakini huyo rafiki yangu alipita na kuniambia kuwa amepata dharura
hivyo asingenipeleka kanisani.
"Nikamrudia
mume wangu na kumwambia mbona kama umerogwa? Akasema ndiyo amerogwa, nikamwambia
twende kanisani ukaombewe, akakataa. Matokeo yake akanikaba shingoni mpaka
nikashindwa kuongea. Nikamwambia unaniua ndipo akaniachia.
"Nilichukua
gari la watu na familia yangu tukaenda kanisani. Kufika kanisani nilimweleza
Mchungaji Gwajima tatizo lililonipata, akaniambia nirudi tu nyumbani kama hali
itakuwa mbaya ataangalia cha kufanya.
"Baada
ya ibada nilimwambia mdogo wangu arudi nyumbani na watoto, mimi nikaenda kukaa
mahali nikiwaza cha kufanya."
BINTI AMPIGIA SIMU
"Ilipofika
kesho yake (Jumatatu) nikapigiwa simu na yule binti akidai anaondoka nyumbani
kwa sababu shemeji yake amemdhalilisha sana. Nilimwambia asiondoke kuna mtu
atakwenda kumchukua mchana kumleta nilipokuwa.
"Alipoletwa
nilishangaa kumkuta katika hali ambayo hawezi kutembea sawasawa. Nikamuuliza
vipi? Ndipo akanielezea jinsi mume wangu alivyomfanyia."
BINTI AENDA HOSPITALI
Flora
aliendelea kusema kuwa, binti mwenyewe aliamua kwamba anakwenda hospitali kucheki
afya. Akasindikizwa na mdogo wake Flora. Kule vipimo vilionesha kweli
aliingiliwa kimwili. Madaktari walimshauri aende polisi.
"Ndipo
akaenda polisi na kutoa maelezo na kuandikiwa faili ambapo mume wangu akawa
anatafutwa.
"Mume
wangu amekuwa akisambaza habari kwamba nina mwanaume sijui nani! Hicho kitu
hakipo. Hata mwaka jana nilikwenda Uingereza lakini tulikuwa wote. "
KUHUSU KUWA NA PESA, MTOTO KULIPIWA ADA
Kuhusu
madai kwamba mtoto amelipiwa ada, yeye hana pesa, Flora alisema: "Pale
kanisani (Ufufuo na Uzima) waumini walipojua nina matatizo na mume wangu na
sipo nyumbani, walipitisha harambee ambapo niliweza kupata shilingi milioni
tisa ndiyo maana mtoto akaenda shule na mimi nikabaki na za matumizi maana kila
kitu kuhusu akaunti ya benki anakijua mume wangu."
MBASHA AOMBA KESI IFUTWE
"Mume
wangu aliniomba msamaha baada ya haya mambo kutokea, nimemsamehe. Aliniomba
nifute kesi polisi, nikamwambia si mimi niliyepeleka kesi polisi. Mimi siwezi
kumsaliti yeye, kwanza nampenda sana Mungu kisha yeye."
AKUTWA AMEVUA PETE YA NDOA
Uwazi lilimkuta Flora akiwa
hana ile pete ya ndoa iliyozoeleka kuwepo kwenye kidole chake. Alipoulizwa
alisema hakuna uhusiano wa pete kutokuwepo kidoleni na ugomvi.
FAMILIA YACHAFUKA
Mwimbaji
huyo alikwenda mbele zaidi kwa kusema kwamba ugomvi kati yake na mume wake
umesababisha familia kuchafuka maana umekuwa gumzo katika kila kona ya mtaa.
Comments
Post a Comment