 |
Mkurugenzi
Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga
(Tanga Uwasa)Mhandisi Joshua Mgeyekwa akizungumza na waandishi wa habari
mkoani Tanga kuhusu maadhimisho ya wiki ya Maji |
 |
Afisa
Uhusiano Mwandamizi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira
Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Dorra Killo akizungumza jambo wakati wa kikao
hicho leo |
Mkurugenzi Mtendaji wa
Mamlaka ya Maji Safi na
Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa)Mhandisi Joshua Mgeyekwa
akizungumza na waandishi wa habari mkoani Tanga kuhusu maadhimisho ya
wiki ya Maji
 |
Mkurugenzi
wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga
Uwasa) Mhandisi Joshua Mgeyekwa kulia akiteta jambo na Meneja Rasilimali
watu na Utawala wa Mamlaka hiyo,Haika Ndalama. |
Waandishi wa Habari Mkoani Tanga
wakifuatilia hotuba ya Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa
Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Joshua Mgeyekwa ambaye
hayupo pichani.
Waandishi wa Habari
Mkoani Tanga wakifuatilia hotuba ya Mkurugenzi wa
Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa)
Mhandisi Joshua Mgeyekwa ambaye hayupo pichani katikati mwenye hijabu
ni Amina Omari wa Gazeti la Mtanzania
Watumishi wa Mamlaka ya Maji Safi
na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga Tanga Uwasa wakiandaa baadhi ya
dondooo kuhusiana na wiku ya maji
Mwandishi wa Gazeti la Daily News
Mkoani Tanga Amina Kingazi akiuliza swali kwenye mkutano huo kulia ni
Mwandishi wa Gazeti la Mwananchi Mkoani Tanga,Raisa Saidi.
Mwandishi wa Azam TV Mkoani
Tanga,Mariam Shedaffa akifuatilia kwa umakini taarifa mbalimbali za
mamlaka ya Maji Safi na Usafiri wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga
Uwasa)
Waandishi wa Habari Mkoani Tanga
Amina Omari wa Gazeti la Mtanzania wa pili kulia wakifuatilia kwa
umakini mada mbalimbali zilizokuwa zikiwakilishwa kwenye semina hiyo
 |
Mwandishi wa Gazeti la Mtanzania,Amina
Omari akuliza swali kwenye mkutano huo |
MAMLAKA ya Majisafi na Majitaka
katika Jiji la Tanga (Tanga-Uwasa), linahitaji kiasi cha shilingi
bilioni 15 hadi 20 kwa ajili ya kutekeleza mpango wa kusafisha majitaka
yaweze kutumika kwa shughulinyingine za kibinadamu ikiwemo kilimo cha
umwagiliaji.
Akizungumza katika semina kwa
wanahabari Jijini hapa Mkurugenzi wa Tanga-Uwasa Injinia Joshua
Mgeyekwa, alisema kutokana na kuzaliza kiasi cha mita za ujazo zipatazo
2,700, wameonelea wayasafishe kwa kujenga mfumo utakaosaidia maji hayo
kutumika tena.
Mgeyekwa alisema tayari wametenga eneo la Utofu kama sehemu
itayokusanya maji taka ambayo kwa sasa kiasi cha asilimia 10 cha wateja
wao maji wanayoyazalisha kupelekwa baharini hivyo mfumo huo utasaidia
suala zima la uchafuzi wa mazingira.
“Tupo na mpango wa kuyatumia maji taka kwa shughuli nyingine kama kilimo
cha mbogamboga, unaimani kwa kufanya hivyo tutaongeza kipato cha mtu
mmoja moja…Lakini ili mpango huu uweze kutimia tunahitaji kiasi cha
shilingi bilioni 15 hadi 20 kutekelezwa,” alisema.
Mkurugenzi huyo alisema kuwa mfumo wa kutumia majitaka kwa shughuli
nyingine za kibinadamu umekuwa ukitumika katika nchi zilizoendelea kama
China, Israel na kwingineko ambako teklonojia hiyo imeanza.
Katika hatua nyingine Mamlaka hiyo imeanza mpango wa kufunga mita za
watumiaji maji wa malipo ya kabla zinazojulikana kwa jina la ‘Lipa Maji
Kadiri Unavyotumia’ (LIMAKU) ambazo tayari wamezifunga katika baadhi ya
maeneo yakiwemo vikosi vya jeshi hapa nchini.
Mkurugenzi huyo alisema hadi sasa wamefunga katika vikosi vya jeshi
vilipo mkoani hapa pamoja na shule 20 za msingi zilizopo katika Jiji la
Tanga na maendeleo yake yanaenda vizuri.
“Tumeagiza mita nyingine za Limaku zipatazo 300 hizi pia tutazifunga
katika taasisi za serikali na watu wengine hasa wateja wetu wenye madeni
makubwa,” alisema Mgeyekwa.
Habari kwa Hisani ya Blog ya
Kijamii ya Tanga Raha.
Comments
Post a Comment