- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
Taifa Stars ya Tanzania kesho Machi
28, 2017 saa 10:00 jioni inaingia tena Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, kucheza
na Intamba Murugamba ya Burundi katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa, kwa
mujibu wa kalenda ya wiki ya mechi za kimataifa ya FIFA.
Huu ni mchezo wa pili kwa Taifa Stars
kucheza ndani ya wiki moja baada ya ule wa awali dhidi ya The Zebras
‘Pundamilia’ wa Botswana uliofanyika Uwanja huo wa Taifa, jijini Dar es Salaam
Jumamosi iliyopita.
Katika mchezo huo wa Jumamosi, Taifa
Stars ambayo kwa sasa inanolewa na Salum Mayanga akisaidiwa na Patrick Mwangata
ambao ni makocha wapya wa kikosi hicho, walishinda kwa mabao 2-0.
Tayari Intamba Murugamba wametua nchini
tangu jana Jumapili saa 4.30 asubuhi na kufikia Hoteli ya De Mag iliyoko,
Kinondoni, Dar es Salaam na jioni yake walifanya mazoezi kwenye Uwanja wa
Karume, Ilala jijini. Leo Jumatatu, inafanya mazoezi Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam.
Ndani ya kikosi hicho wamo
washambuliaji wawili wanaotamba katika klabu za Simba na Young African za Dar
es Salaam. Nyota hao ni Amisi Tambwe wa Young Africans na Laudit Mavugo wa
Simba.
Leo Jumatatu Machi 27, 2017 saa 8.30
alasiri nyota hao wakiongozana na kocha wao watazungumza na wanahabari namna
walivyoajiandaa kucheza na Taifa Stars ambayo pia ina nyota wengi wanaocheza na
wachezaji hao wa Burundi katika klabu za Simba na Young Africans.
Wakati Mavugo ni mshambuluaji,
anatarajiwa kuwa na wakati mgumu mbele ya walinzi mahiri ambao pia wako Simba
kama vile Abdi Banda na Mohammed Hussein wakati Andrew Vicent anayetoka Young
African atakuwa kisiki kwa Tambwe wanayecheza naye timu moja kama makocha
watawapanga.
Kwa upande wake, Mayanga alifurahishwa
na ushindi wa Jumamosi iliyopita dhidi ya The Zebras ya Botswana na hivyo
amehimiza Watanzania kujitokeza kwa wingi katika mchezo wa kesho.
Katika kuunga mkono wito wa Kocha
Mayanga, TFF imebakiza viingilio vya mchezo huo kuwa sawa na vile vya Jumamosi
iliyopita kwani katika mzunguko ambao unachukua mashabiki wengi kiingilio
kitakuwa ni Sh 3,000.
Kwa upande wa VIP “A” Kiingilio
kitakuwa ni Sh 15,000 wakati VIP “B” na VIP “C” kiingilio kitakuwa ni Sh
10,000. Viingilio hivyo vimelenga kuwaalika Watanzania wengine kwenda uwanjani.
Comments
Post a Comment