- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
SAKATA la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, kuvamia kituo cha matangazo cha Clouds Media Machi 17, 2017 limemng'oa Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye.
Taarifa ya Ikulu iliyotolewa jana usiku inasema nafasi yake imechukuliwa na Dk. Harrison Mwakyembe ambaye alikuwa Waziri wa Sheria na Katiba, huku Mbunge Mteule wa Rais, Profesa Palamangamba Kabudi akiteuliwa kuwa Waziri wa Sheria na Katiba na uteuzi huo umeanza mara moja.
Wachunguzi wa masuala ya siasa na utawala, wameelezea kuondolewa kwa Nape kumetokana na hatua aliyoichukua ya kuunda kamati ya uchunguzi kuchunguza sakata la Makonda kuvamia kituo cha Clouds TV kwa nia ya kushinikiza warushe kipande cha video cha mwanamke mmoja aitwaye Grace akidai kutelekezwa na Askofu Josephat Gwajima baada ya kumzalisha mtoto.
Licha ya ukweli kwamba Rais Dk. John Magufuli alikwishalizungumzia suala hilo la kumtaka Makonda aendele kuchapa kazi, lakini Kamati ya Nape iliendelea na kazi na jana ikawasilisha ripoti yake iliyoeleza yaliyotokea siku hiyo.
Dkt. Hassan Abbas, Mkurugenzi wa Idara ya Habari – Maelezo ndiye
alimkabidhi ripoti hiyo akiwa mwenyekiti wa kamati ya watu watano walioteuliwa
na kupewa muda wa saa 24.
Kamati hiyo ya Nape iliongozwa na Dkt. Hassan Abbas, Deodatus
Balile ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF), Jesse Kwayu,
Mhariri Mtendaji wa gazeti la Nipashe, Nengida Johannes Lailumbe kutoka Upendo
Radio, na Mabel Masasi kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).
Akisoma ripoti hiyo, Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo,
Deodatus Balile, alisema kamati yao imejiridhisha kwamba Makonda alikiunga kwa
makusudu mamlaka yake pamoja na kuvunja sheria za nchi, ikiwemo Sheria Namba 3
ya Utangazaji, kwa kuingia ndani ya chumba cha matangazo bila idhini huku akiwa
na askari wenye silaha.
Wamependekeza kwamba, Makonda ni vyema aombe radhi kwa
Clouds Media na tasnia yote ya habari, lakini wakaiomba pia mamlaka ya uteuzi
kumwajibisha kwa mujibu wa taratibu za uongozi.
“Ni kweli Makonda alivamia Clouds Media, alivamia akiwa na
askari na kuwatisha wafanyakazi wa Clouds ambapo alikaa kwa saa moja, na
akawatisha kwamba kilichotokea hapo kisitokee nje, kwani angewashughulikia kwa
kuwaingiza kwenye orodha ya watuhumiwa wa dawa za kulevya.
“Kamati imeona kuwa hakuna mfanyakazi aliyepigwa lakini
wafanyakazi walilia kwa kitendo kile,” alisema Balile.
Waziri Nape alisema kwamba ataipitia ripoti hiyo na
kuiwasilisha kwa mamlaka zinazohusika kwa utekelezaji.
Rais amkingia kifua:
Hata hivyo, kuna uwezekano mdogo wa Makonda kuwajibishwa
kwani mamlaka yake ya uteuzi, ambayo ni Rais, amekwishamtetea na kumwambia
kwamba aendelee kuchapa kazi na aachane na maneno maneno ya mitandao.
Akizungumza wakati wa sherehe za kuweka jiwe la msingi
katika ujenzi wa barabara za juu (flyovers) pale Ubungo Mataa jijini Dar es
Salaam Machi 20, 2017, Rais Dkt. John Magufuli alisema hawezi kufanya uamuzi
kwa shinikizo la mitandao na akaonya kwamba, wale waliodhani kuandika hivyo
ndiko kungemfanya aamue cha kufanya wamekosea.
"Mimi ni Rais ninayejielewa. Mimi ndiye niliyemteua,
msinipangie cha kufanya. Mimi sionyeshwagi njia ya kupita. Sipangiwi na mtu
nani wa kumchagua na kumuweka wapi. Watu wafanye kazi, waache majungu. Makonda endelea
kuchapa kazi," alisema.
Ilivyokuwa
Makonda alidaiwa kuvamia kituo hicho akiwa na askari polisi
nane wenye bunduki na kuingia moja kwa moja hadi chumba cha kurushia matangazo
wakati kipindi kinaendelea na kuwashambulia watangazaji wawili wa kipindi cha
Da’Weekend Show (Shilawadu) kinachorushwa kila siku ya Ijumaa.
Habari za awali zinasema, Makonda alikuwa amechukiwa na kipindi
hicho kutorusha video ya mwanamke anayedai kuzaa na Askofu wa Kanisa la Ufufuo
na Uzima, Josephat Gwajima, katika kile kinachoonekana ‘vita baina yao’.
Waziri Nape aliiteua kamati hiyo jana, Jumatatu asubuhi,
Machi 20, 2017, na kuipa saa 24 ifanye uchunguzi ili kubaini ukweli wa
kilichotokea huku akilaani tukio hilo kwamba ni kunajisi uhuru wa habari.
"Tumezoea kuona matukio haya yanatokea kwenye nchi
ambazo zimepinduliwa kwenda kwenye vyombo vya habari na mabunduki si sawa, kwa
jambo hili tunataka kutenda haki tumsikilize Mkuu wa Mkoa ili tujue kwanini
amefanya jambo hili.
"Matukio kama haya hutokea wakati nchi inapotaka
kupinduliwa, lakini kama Rais yupo na nchi haijapinduliwa, basi kuingia ndani
ya chombo cha habari na silaha, huku ni kunajisi uhuru wa habari," alisema
Nape.
Pamoja na hayo Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Vyombo
vya Habari (MOAT), Dkt. Reginald Mengi amesema hawezi kutoa lawama kwa mtu
yoyote mpaka pale ukweli utakapofahamika japokuwa ameonekana kukerekwa.
"Kwetu sisi hili ni jambo ni la hatari sana,
linatuogopesha na linatishia maisha ya waandishi wa habari," alisema Dkt.
Mengi.
Siku Makonda
alipomshambulia Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba
mwaka 2014.
Gwajima vs Makonda:
Vita baina ya Gwajima na Makonda imeendelea kwa zaidi ya
mwezi mmoja sasa, ambapo inatokana na hatua ya mkuu huyo wa mkoa wa Dar es
Salaam kuanzisha operesheni ya kupambana na dawa za kulevya, ambapo Gwajima ni
miongoni mwa watuhumiwa walioitwa na kuwekwa mahabusu kwa madai ya kujihusisha
na biashara hiyo haramu.
Kutokana na kitendo hicho, Gwajima, akidaiwa kushirikiana na
mwanadada Mtanzania aishiye Marekani, Mange Kimambi, walifichua kwamba Makonda
siyo jina lake bali jina lake halisi ni Daudi Albert Bushite, na kwamba hata
vyeti vyake ni vya kufoji.
Jumatatu asubuhi wakati wa kipindi cha Power Breakfast,
Mkurugenzi wa vipindi na uzalishaji wa Clouds Media, Ruge Mutahaba alieleza
kusikitishwa na matumizi mabaya ya madaraka yaliyooneshwa na Mkuu huyo wa Mkoa.
Kilichotokea Machi 17, 2017:
MAKONDA AVAMIA CLOUDS KWA
MITUTU YA BUNDUKI
Jengo la Clouds Media
Group lililopo Mikocheni B jana lilishuhudia sekeseke la aina yake baada ya
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuvamia akiwa na Walinzi wenye
Bunduki.
Tukio hilo tukoea majira ya Usiku wakati kipindi SHILAWADU kikiwa hewani ambapo Makonda alivamia kwa lengo la kushinikiza Shilawadu waonyeshe mahojiano yenye lengo la kumchafua Askofu Gwajima.
Vyanzo vya uhakika vinaeleza kwamba, mwanzoni wiki 2 zilizopita, SHILAWADU walipigiwa simu na watu wasiojulikana wakieleza kwamba wana 'ubuyu' mzito wa kuhusu Askofu Gwajima na mwanamke anayedaiwa kuzaa nae. Mwanzo Shilawadu walikataa habari hiyo, lakini siku moja walikutana na Makonda akawashawishi SHILAWADU wafuatilie stori hiyo. Kama kawaida yao kupenda umbea, SHILAWADU wakiongozwa na Soudy Brown walimtafuta mwanamke anayedaiwa kuzaa na Gwajima kisha wakamhoji.
Hata hivyo, kwa kuhofia nguvu ya Gwajima katika kupambana na shutuma dhidi yake, na kwa kuzingatia maadili ya kazi, SHILAWADU waligoma kurusha habari hiyo hewani mpaka wapate kauli za upande wa pili ( upande wa Gwajima ). Baada ya kuhangaika huku na kule , SHILAWADU walishindwa kupata upande wa pili wa habari ( walishindwa kubalance story ).
Kutokana na hilo, na kujua kwamba Gwajima asingewaacha salama kwa kutoa story ya uongo dhidi yake, #SHILAWADU na wasimamizi wa vipindi wa Clouds Tv waliamua kuachana kabisa na story hiyo.
MAKONDA ANAINGIAJE? : Imefahamika kwamba watu ambao walipiga simu kwa Shilawadu kuhusu uwepo wa Mwanamke huyo ni watu wa Makonda. Makonda alitaka story hiyo itolewe kupitia #SHILAWADU ambao wana kawaida ya kuripoti matukio ya Watoto/wanawake waliokataliwa. Kwa kuwa Makonda ana marafiki wengi pale Clouds, aliamini kwamba story hiyo lazima ingetolewa na hivyo kumchafua adui yake GWAJIMA (kuzima sakata la vyeti ).
Akiwa nyumbani kwake Masaki, Makonda alikaa kwenye Tv yake Ijumaa kusubiri SHILAWADU wamvue nguo Gwajima. Cha kumsikitisha, Makonda alipata habari kwamba SHILAWADU wamegoma kupeleka habari hiyo. Hata viongozi akiwemo swahiba wake Ruge walikaataa kabisa kupeleka habari ambayo haiko 'balanced' na mbaya zaidi inawaingiza kwenye vita na mtu wa aina ya Gwajima.
Kama kawaida yake, Makonda aliamua kutumia ubabe. Kwa kuwa amezoea kuingia Clouds, Makonda alifahamu kuwa muda huo viongozi hawapo na watu waliopo anawamudu. Hivyo aliamua kwenda Clouds kuhakikisha Shilawadu wanaonyesha habari hiyo ya kumchafua Gwajima. Hivyo alibeba wanaume zaidi ya 8 wakiwa wamebeba silaha za moto.
Alipofika Clouds, walinzi wa Getini walimruhusu kupita yeye na gari iliyokuwa nyumba yake akisema ni rafiki zake wamekuja mara mara moja kwenye SOSOO FRESH kwani Adamu Mchomvu amewaalika. Lakini alipofika Reception, Mlinzi wa zamu alisitia baada ya kuona Makonda amekuja na watu wengi. NA HAPO NDIPO KASHESHE ILIANZA.
Walinzi wa Makonda walitoa Bunduki, walimtishia Mlinzi wakampiga sana na wakatumia nguvu kubwa hadi walifanikiwa kuingia ndani. Walipofika na Bunduki zao, Makonda aliamuru kila mtu kukaa alipo huku akilazimisha habari ya Gwajima iende. Kwisa kama kiongozi wa kipindi ndiye ambaye alipingwa mitama na ngumi za kutosha.
Kwa walioangalia kipindi wanajua kwamba kipindi hakikuisha, hiyo ni kutokana na kwamba Makonda na waligawa kipigo cha maana kwa Shilawadu kisha wakawabeba kwenda nao nje akisema wanaenda Cental.
Pia alitumia Bunduki kuwalazimisha Shilawadu wampe Video ya Mama anayedaiwa kuzaaa na Gwajima (alipewa). Makonda aliwaambia wapambe wake kama Shilawadu wamekataa kuonyesha habari hiyo baasi yeye atahakikisha inasambaa kupitia mitandao ya kijamii.
Hivi sasa Shilawadu hawako sawa kisaikolojia huku Suod Brown akiwa hana amani kwani alipigwa picha na Makonda alimuambia kama anaogopa kumdhalilisha Gwajima baasi yeye atadhalilishwa kwani Sura yake itawekwa hadharani kila mtu afahamu.
Baadae Makonda aliondoka baada ya kupigiwa simu ambayo haijulikani nani alipiga lakini Makonda alipoondoka Ruge alingia Clouds akiwa na watu huku na yeye amebeba bastola. Inaaminika ile simu ilipigwa kumuambia aondoke maana Ruge anakuja.

CV YA PAUL MAKONDA
1. Alizaliwa tar.15/02/1981 katika kijiji
cha Koromije, wilaya ya Misungwi, mkoa wa Mwanza.
2. Majina yake halisi ni Daudi Albert
Bushite
3. Alianza darasa la kwanza mwaka 1988 katika
shule ya msingi Koromije akitumia majina ya Daudi Albert Bushite. Mwaka 1991
alifeli darasa la 4, akarudia.
4. Mwaka 1992 alifeli tena na hivyo akahamishiwa
Mwanza mjini, ili aweze kusoma na kupata masomo ya jioni (tuition).
5. Mwaka 1996 alihitimu darasa la 7 lakini
hakuchaguliwa kuendelea na elimu ya sekondari katika shule ya serikali.
6. Mwaka 1997 akajiunga na kidato cha
kwanza shule ya sekondari ya Pamba.
7. Mwaka 2000 akahitimu kidato cha 4 na kupata
daraja sifuri (division zero).
8. Mwaka 2001 akatumia cheti cha Ndg.Paul
Christian Muyenge (chenye div.3 ya points 25) kujiunga na chuo cha uvuvi
Nyegezi (Nyegezi Fisheries Training Institute) kwa masomo ya Certificate
akahitimu mwaka 2002.
9. Mwaka huohuo 2002 akitumia cheti cha
Ndg.Paul Christian Muyenge, alijiunga na Chuo cha uvuvi Mbegani Bagamoyo kwa
masomo ya Diploma ya uvuvi (ORDINARY DIPLOMA IN MASTER FISHERMAN, NTA LEV.6),
na kuhitimu mwaka 2005.
10. Mwaka 2003 alikutana na Ndg.Benjamin
Sitta (mtoto wa Marehemu Samwel Sitta, ambaye ni Mayor Kinondoni kwa sasa).
Wakawa marafiki.
11. Mwaka 2005 baada ya kuhitimu Stashahada
yake ya uvuvi, aliomba admission Chuo cha Kilimo Sokoine kusoma shahada lakini
akakosa nafasi.
12. Baada ya kukosa nafasi alienda kuishi
nyumbani kwa Marehemu Sitta akiwa kama rafiki wa Ben (mtoto wa Sitta). Kwakuwa
alitoka familia duni, Sitta aliahidi kumsomesha elimu ya juu.
13. Mwaka 2006, alipata udahili Chuo cha
ushirika na biashara Moshi (wakati huo kikiwa chuo kikuu kishiriki cha SUA),
kwa kutumia vyeti vyake vya certificate (ya Nyegezi) na diploma (ya Mbegani).
14. Alidahiliwa kwa course ya BA in Cooperate
Management & Accounting. Mwaka 2007 alimaliza first year lakini akashindwa
kuendelea na 2nd year baada ya kupata Suplementary 6 kati ya Course 8 alizokua
akisoma (akawa discontinued).
15. Mwaka huohuo 2007 akaomba Admission
upya. Akamaliza first year akiwa na carriers 3 ambazo alienda nazo 2nd year.
Mwaka 2008 akiwa 2nd year akapata supplementary 4 kati ya course 8 alizokua
akisoma. Akawa na mzigo wa carry over na supplementary. Akaamua kuacha chuo.
16. Mwaka 2008 akaenda kujaribu kuomba udahili
chuo kikuu SUA kwa mara nyingine lakini akakosa.
17. Mwaka 2009 akarudi tena MUCcoBS kwa udahili
mpya. Akaachana na CMA akachagua Community &Economic Development (CED).
18. Mwaka 2012 akahitimu shahada ya kwanza
ya Community &Economic Development kwa jina la Paul C Makonda badala ya
majina yake halisi ya Daudi A Bushite.
19. Jina Makonda analitumia baada ya kula
kiapo mahakamani kubadili jina. Cheti cha Form four kinasomeka Paul C Muyenge lakini
vyeti vya elimu ya juu vinasomeka Paul C Makonda baada ya kuapa mahakamani.
20. Ndugu Daudi Albert Bushite ameoa (tangu
mwaka 2009) lakini hajabahatika kupata mtoto. Na ndiye mkuu wa mkoa wa Dar es
Salaam kwa sasa.
Comments
Post a Comment