Featured Post

RAIS MHE. DKT. MAGUFULI AFUTA AGIZO LA KUFUNGA NDOA KWA SHARTI LA KUWA NA CHETI CHA KUZALIWA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wanahabari Mkoani Dodoma kuhusiana na kufuta agizo lililotolewa jana na Waziri wa Katiba na Sheria kuhusu Wananchi wanaohitaji kufunga ndoa kuanzia mwezi Mei mwaka huu kuwa na vyeti vya kuzaliwa. 
Rais Mhe. Dkt. Magufuli ameagiza utaratibu wa awali uendelee kutumika kwasababu wananchi wengi wa Tanzania hawana vyeti, hivyo wangekosa haki hiyo ya kufunga ndoa. 
Kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Jordan Rugimbana. PICHA NA IKULU

Comments