- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
RAIS MHE. DKT. MAGUFULI AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA BANDARINI NA KUZUIA MAKONTENA 20 YENYE MCHANGA WA MADINI ULIOKUWA USAFIRISHWE NJE YA NCHI
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika ziara ya kushtukiza katika
Bandari ya Dar es Salaam kufatilia maagizo yake ya kudhibiti vitendo vya
udanganyifu vinavyofanywa na wafanyabiashara wanaogiza na kusafirisha mizigo
ndani na nje ya nchi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli
akihesabu makontena 20 yenye mchanga wa madini ambapo ameamuru kontena hizo
zisisafirishwe mahali popote.
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na kutoa maagizo
mbalimbali kuhusu makontena 20 (yanayoonekana nyuma) yenye mchanga wa madiniuliokuwa usafirishwe
kwenda nje ya nchi ambapo ameagiza Kontena hizo zisisafirishwe mahali popote.
Makontena 20 yenye mchanga wa madini
yakiwa yamezuiwa kusafirishwa nje ya nchi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli mara alipofanya ziara ya kushtukiza
katika bandari ya Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akikagua nyaraka mbalimbali zenye
maelezo kuhusu makontena ambayo husafirishwa nje ya nchi katika Bandari ya Dar
es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia baadhi ya magari
yalivyoingizwa nchini na Wafanyabiashara wakubwa kwa njia isiyo halali ya kudai
kuwa ni makontena ya mitumba wakati ndani yake wanaficha magari yakifahari wanayoyachanganya
na bidhaa zilizochakaa.
Moja ya kontena likiwa lina gari
ndani yake aina ya Range Rover ambapo muagizaji alidai kuwa anaagiza mitumba lakini
kumbe ndani yake anakutwa ameficha magari ya kifahari.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na IGP Ernest Mangu
mara baada ya kufanya ukaguzi Bandarini hapo. PICHA NA IKULU
Comments
Post a Comment