- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
MASAUNI AVIAGIZA VYOMBO VYAKE KUONGEZA KASI ZAIDI KUKAMATA WAHAMIAJI HARAMU, WAUZA DAWA ZA KULEVYA MKOANI LINDI, AKAGUA MIRADI YA MAENDELEO
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad
Masauni akizungumza na Maafisa na Askari wa vyombo vya Ulinzi na Usalama
vilivyo chini ya Wizara yake, katika Ukumbi wa Bwalo la Magereza, mjini Kilwa
mkoani Lindi. Masauni aliwataka maafisa na askari hao kuongeza nguvu zaidi
katika ukamataji wa wahamiaji haramu pamoja na wauza dawa za kulevya. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad
Masauni (katikati), akiwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, Renatha Mzinga
(kushoto) wakati Naibu Waziri huyo alipokuwa anakagua Makazi ya askari Polisi,
Mitwero mkoani humo ambapo nyumba za askari hao zimechangaa na chache kutokana
na wingi wa askari hao. Hata hivyo, Serikali hivi karibuni inatarajia kujenga
nyumba mpya katika eneo hilo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, Renatha Mzinga akimuonyesha
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni eneo la Mitwero
mkoani humo ambalo nyumba za makazi ya askari polisi zitakapojengwa. Masauni
alikagua nyumba wanazoishi askari hao kwasasa pamoja na kukagua eneo hilo
makazi mapya yatakapojengwa. Picha na
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad
Masauni (katikati), akilikagua Jengo jipya la ghorofa la Idara ya Uhamiaji Mkoa
wa Lindi ambalo linajengwa mjini humo. Kulia ni Afisa Uhamiaji mkoa huo, George
Kombe, pamoja na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, Renatha Mzinga. Masauni aliongozana
na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama vilivyo chini ya Wizara yake mkoani
humo kwa lengo la kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo. Picha na Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad
Masauni (kulia), akimpa maelekezo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, Renatha Mzinga
(wapili kushoto), wakati Naibu Waziri huyo alipokuwa anaangalia ramani ya
ujenzi wa makazi ya askari polisi eneo la Mitwero mkoani humo. Masauni yupo
mkoani humo kwa ajili ya ziara ya kikazi.
Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Comments
Post a Comment