- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
Vijana
kutoka Arusha maarufu kwa ngoma zao kama kimbaumbau na digidigi wanaojulikana
kama Mamongóo (vijana washamba), wamesema kuwa jamii ya sasa hivi inawatisha
kutangaza mishe zao wanazofanya nje ya muziki.
Mamong’oo
wiki hii wakiwa katika ziara yao kikazi Dar es salaam, wamesema kuwa wao
wanajihusisha na biashara nyingi ikiwemo kilimo na ufugaji kama zilivyo jamii
nyingi mkoani Arusha. Lakini mtangazaji
DJ Tee wa kipindi cha vijana cha Shujaaz alipotaka kufahamu mishe
zingine wanazofanya wasanii hao walisema hawawezi kumwaga mchele maana siku
hizi wanga ni wengi.
“Sisi
pesa zetu hatujahifadhi benki ila tumeziweka sehemu ambayo tunajua zina
mzunguko wa kuzalisha, na tumewekeza kwa vijana wenzetu” alisema chalii Jambo
kutoka kundi hilo. Hata hivyo, walipoulizwa ikiwa kijana amepata pesa anatakiwa
kuwekeza kwenye kitu gani kwanza kati ya shamba, nyumba au ardhi, walisema
kwamba ardhi ndio kitu ambacho kinafaa kwa kijana kuwekeza kabla ya kununua
gari au hata nyumba maana ardhi inaweza kuleta nyumba na gari.
Wasanii
wengi siku hizi wamekuwa na kasumba ya kutumia mishe zao wanazofanya pembeni ya
sanaa sio kwa kujiongezea kipato pekee bali kujipatia heshima miongoni mwa fans
wao. Mfano mzuri ni msanii Masanja Mkandamizaji ambaye kwa sasa amekuwa
akitengeneza mamilioni ya pesa kutokana na biashara ya #KilimoPesa ambapo yeye
analima mpunga pamoja na kumiliki mgahawa wa kuuza wali nyama pamoja na
biashara zingine tusizozifahamu.
Kipindi
cha vijana cha Shujaaz huruka hewani kila Jumamosi saa nne kamili asubuhi
kupitia Abood FM ya Morogoro, kisha safari huendelea saa tisa alasiri kupitia
East Africa Radio, TBC FM na Chuchu FM ya Zanzibar kwa wakati mmoja, huku
KingsFM ya Njombe ikijiunga saa kumi jioni.
Comments
Post a Comment