- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
KATIBU WA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) WILAYA YA MUFINDI JIMSON MHAGAMA AJITOSA UBUNGE WA AFRIKA MASHARIKI
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
Katibu wa Chama cha
Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Mufindi, Jimson Mhagama, akiwa kwenye mmoja ya mikutano ya kampeni kumtafuta Diwani wa Kata ya Igombavanu wilayani Mufindi akikitumikia chama.
Katibu wa Chama cha
Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Mufindi, Jimson Mhagama, akiwa kwenye mmoja ya mikutano ya kampeni akimwombea kura Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli mwaka 2015 katika uwanjwa wa Wambi mjini Mafinga.
Katibu wa Chama cha
Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Mufindi, Jimson Mhagama, akipeana mkono na Waziri Mkuu mstaafu wa awamu ya nne Mh. Mizengo Pinda kwenye moja ya majukumu ya kukitumikia chama.
Katibu wa Chama cha
Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Mufindi, Jimson Mhagama, akipeana mkono na Rais mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na kubadilishana maneno ya hapa na pale.
Na Fredy Mgunda, Mufindi
KATIBU wa Chama cha
Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Mufindi, Jimson Mhagama, ametangaza nia ya kugombea
nafsi ya kuchaguliwa kuwa mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki kwa kuiwakirisha
Tanzania.
Akizungumza kwa njia ya simu Mhagama
alisema kuwa atahakikisha lugha ya Kiswahili inatumika barani Afrika kama lugha
mama kwa kuwa ndiyo lugha iliyosambaa zaidi barani humo.
“Nimetembelea nchi nyingi hapa
Afrika nimekutana na watu wengi wanazungumza Kiswahili hivyo hoja yangu itakuwa
kuhakikisha natimiza kitu alichotuachia hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius
Kambarage Nyerere,” alisema Mhagama.
Mhagama alisema kuwa
atalazimika kuwatetea wakulima kwa kuwa asilimia kubwa ya Watanzania wengi ni
wakulima na uchumi wao bado unategemea kilimo hivyo ni lazima kuwekeza nguvu
kwenye kilimo chenye tija na kuinua mazao yanayozalishwa hapa nchi
na kukuza uchumi.
“Tanzania tumebatika kuwa na
ardhi nzuri na kubwa ambayo kwa asilimia kubwa bado haijatumika kwa mjibu wa
wataalam wa kilimo hivyo ni lazima kutafuta njia mbadala ya kuwainua wakulima
hawa ili kuviwezesha viwanda vyetu kupata malighafi nyingi na za kutosha ili
kuinua kipato cha kila sekta hapa nchini,” alisema Mhagama.
Aidha, Mhagama amewataka Watanzania kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli kwa kazi anazozifanya kwa kutafuta njia bora ya kuinua uchumi wa
wananchi wake kutoka hapa ulipo hadi kufikia uchumi wa viwanda kama sera yake
alivyoielekeza kwenye Tanzania ya Viwanda.
“Angalia sasa tunapata
wawekezaji wengi kwenye sekta ya viwanda, hii ni dalili nzuri ya kuukaribia
uchumi wa viwanda, hivyo nikiwa mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki nitaendelea
kuunga mkono juhudi za Rais kwa kutafuta njia za kuwainua wawekezaji wazawa ili waboreshe
na kuanzisha viwanda vyao,” alisema Mhagama.
Mhagama aliwaomba Watanzania
kwa ujumla kumuombea ashinde kiti hicho ili aweze kuiwakirisha vyema nchi kwa
uadilifu uliotukuka.
Comments
Post a Comment