- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
HIVI NDIVYO ASKOFU GWAJIMA 'ALIVYOHUSIKA' KUISAMBARATISHA NDOA YA FLORA MBASHA. SOMA BARUA HII YA EMMANUEL MBASHA!
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
HII ni barua ya malalamiko aliyoiandika Emmanuel Mbasha,
aliyekuwa mume wa mwimbaji wa nyimbo za Injili, Flora au ‘Madame Flora’,
aliyoiandika mwaka 2014 na ikanaswa
na vyombo vya habari na kusambaa kupitia mitandao ya kijamii kwenda kwa Mchungaji
Josephat Gwajima wa Kanisa la Ufufuo na Uzima.
Emmanuel Mbasha na mkewe Flora wakati wa mgogoro wa ndoa yao mwaka 2014. Huyu anaomba, huyu anatafakari!
Katika barua hiyo, ambayo MaendeleoVijijini inaichapa neno
kwa neno, Mbasha alikuwa akilalamika Mchungaji (sasa Askofu???) Gwajima
kuingilia na kuivuruga ndoa yake, ambayo kwa sasa imevunjika rasmi baada ya Flora
kufungua madai ya talaka katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni na kushinda.
Mbasha, ambaye naye ni mwimbaji wa Injili, aliandika barua
hiyo baada ya mgogoro kuendelea huku tuhuma nyingi zikielekezwa kwa Gwajima,
kwamba ndiye aliyekuwa chanzo kutokana na kuwa na uhisiano wa kimapenzi na
Flora licha ya kufahamu kwamba mwanamke huyo ni mke wa mtu.
Kumbe hata ile skendo ya Mbasha kubaka shemejiye ilikuwa ni ‘muvi’
iliyoandaliwa na Flora na Gwajima, kama hii ambayo Mkuu wa Mkoa wa Dar es
Salaam alikuwa ameiandaa.
Na Mbasha anasema kwenye barua yake kwamba, kumbe waandishi
watatu wa magazeti ya udaku walilipwa fedha ili kuhakikisha habari zinaandikwa
katika ‘muvi’ hiyo na Mbasha anafungwa jela miaka 30 kwa ubakaji!
Hata suala la ‘sembe’ Mbasha amelidokeza kwenye barua yake,
hivyo yawezekana tuhuma
za sasa zilizozusha vita kati ya Gwajima na Makonda ni za muda mrefu na
madai yamekuwa yakiendelea chini kwa chini.
Sitaki kukumalizia uhondo, barua hiyo inajieleza yenyewe
hapa chini ingawa imehaririwa kwa makosa ya kisarufi tu:
"Mchungaji ... yapata
kama wiki mbili zilizopita nilihoji kupitia vyombo vya habari juu ya ‘utajiri'
wa ghafla wa mke wangu mara baada ya mgogoro kutokea kati yangu na yeye, bila
kupoteza muda mke wangu akanijibu kupitia gazeti moja la udaku kuwa amechangiwa
fedha kiasi cha milioni 9 na waumini kanisani kwako.
Mchungaji, naomba
uelewe kuwa nafahamu juu ya mipango yote mnayoipanga kuliko unavyodhani!!
Kwanza ni kweli kuwa mlipitisha harambee ya kumchangia mke wangu, lakini
kiwango kilichopatikana kilikuwa ni milioni 2 na laki tatu na si milioni tisa
kama mlivyotangaza!! Lakini mlitangaza uongo huo makusudi iwe rahisi kutimiza
malengo yenu ya kidhalimu mliyoyapanga juu yangu!!
Mnamo tarehe 3 mwezi Juni
mwaka huu (2014), mlifungua akaunti mpya kwa jina la mke wangu katika benki ya CRDB
Morogoro, na siku nne baadaye mke wangu aliingiziwa fedha kiasi cha milioni 18
kutoka akaunti ya MWANAMAPINDUZI FOUNDATION ambayo hiyo account ipo NMB Mwanza!
Ambapo asasi hii inamilikiwa na mchungaji wako msaidizi Maximilian Machumu
pamoja na Mbunge wa Viti Maalumu kutoka mikoa ya Kaskazini!
Nashukuru kama ulimpa
fedha hizi kwa nia ya kumsaidia, lakini hofu yangu ni kuwa kwanini kitendo hiki
kifanyike kwa kificho?? Kwanini mtumie njia za siri ambazo si rahisi watu kujua
kama mmempa fedha??
Pia napatwa na mashaka
zaidi kwani siku moja baada ya fedha hizi kuingizwa taarifa ya benki inaonyesha
kuwa kiasi cha milioni sita cash zilitolewa na siku hiyo hiyo wapo waandishi
watatu wa magazeti ya udaku ambao wanaonekana waliingiziwa fedha kiasi cha milioni
moja kila mtu na aliyedeposit hizo fedha ni moja ya viongozi wako hapo
kanisani!! Kuna nini hapo??
Mchungaji, naomba
tusizunguke mbuyu! Ni dhahiri shahiri kuwa umekuwa na uhusiano wenye utata na
mke wangu kwa muda mrefu sasa!
Binafsi nilianza
kupata wasiwasi mwaka jana (2013) mwezi Desemba tulipoenda katika mkutano wako
wa injili pale Morogoro! Mimi na mke wangu tulifikia hoteli ya Kingsway Msamvu
na wewe ulifikia Nashera Hotel maeneo ya Forest Hill!!
Baada ya siku tatu za
mahubiri mkutano wako ulipigwa marufuku na serikali kwa sababu ya maneno ya kichochezi
uliyokuwa unahubiri, hivyo ikatulazimu waimbaji wote turejee Dar es Salaam!!
Lakini uliniomba mke wangu
abaki na wewe kwani ulipanga uwe unawafanyia watu maombi pale kanisani kwako Kihonda
kwa muda wa siku nne!! Nilikubali na nikamuacha mke wangu nyumbani kwa dada
yako pale Mazimbu!! Lakini kesho yake dada yako alisafiri kwenda Mwanza na
ikabidi mke wangu arudi hotelini Kingsway!!
Kwa taarifa nilizonazo
na nimezithibitisha kupitia wahudumu wa pale hotelini ni kuwa mke wangu
hakuwahi kulala pale hata siku moja ingawa chumba kililipiwa kwa siku zote
zile!! Unaweza kunijibu alikuwa analala wapi?? Je, unaweza kunieleza kwanini
mke wangu alikuwa analetwa Nashera Hoteli na taxi kila siku usiku!! Sibahatishi
katika hili kwani hata namba ya dereva taxi ninayo!!
Yote haya nilivumilia,
na hapa kati kati kuna mengi sana yametokea lakini nikajifanya mjinga
nikajishusha nikavumilia kwa lengo la kulinda ndoa yangu isiharibike lakini
naona wenzangu hambadiliki wala hamjishitukii sana sana mapenzi ndio yanazidi
kuwa motomoto kati yenu!! Ulikuwa unategemea nivumilie mpaka lini, nijishushe
kiasi gani, niwe mjinga kiasi gani? Nilikuvumilia sana mchungaji lakini sasa
imefika point hapana, imetosha lazima nikuondelee uvivu Watanzania na dunia
ikufahamu jinsi ulivyo na kitendo ulichonifanyaia na unataka kuniziba mdomo kwa
kunitishia jela miaka 30!!!
Wewe ni mpuuzi na
shetani anaishi ndani yako... na nataka nikuahidi kitu kimoja kuwa
NITAKUSHINDA! Najua utanisumbua sana kutokana na hela zako but at the end, I
will be the last man standing!! Narudia tena, nitakushinda.!!
Bila kusahau naomba
niongee na wewe pia mke wangu, hivi ni nini kilichokukuta ndani ya moyo wako
How did we get here?? Je ni fedha zilizokufanya ukengeuke kiasi hicho au kuna
kingine?? Kama unanichukia mimi kiasi hiki je, uwahurumii hata watoto wetu??
Mbona tunawatengenezea mikosi wakiwa wadogo hivi?? Hivi unadhani watoto
wanajisikiaje watakaposikia kuwa baba ameenda jela kwa kosa la kubaka lakini
aliyechongesha muvi yote hiyo ni mama?? Hivi kisaikolojia hawa watoto
watakuwaje? Si watakuwa huku wanatuchukia sisi wote wawili kwa aibu na mikosi
hii tunayowatengenezea? Kwanini tunataka kuwataabisha watoto kwa dhambi ambayo
hawajaitenda?
Yes nafahamu
nimekukosea mengi and am very sorry for that, lakini basi embu kumbuka mke wangu
nimekuvumilia mambo mangapi mke wangu, kumbuka makosa mazito uliyonifanyia
lakini nikakusamehe ni sijamsimulia hata ndugu yako ama ndugu yangu ili kulinda
heshima yako!! Kumbuka jinsi tulivyopigana na changamoto mbalimbali mpaka leo
hii umefikia kuwa moja ya icons wa muziki wa injili hapa nchini?? Kumbuka
shida, manyanyaso, dhuluma, kuchekwa na kudharauliwa ambako tumepitia mpaka leo
hii tuko hapa!!!
Mke wangu, kwa miaka
yote hii nimekubali nionekane Bushoke tu huku watu hawajui kuwa mimi ndiye
ninayechora ramani ya kila ishu yako!! Mimi ndiye nimekuwa nafatilia na
kufanikisha kila kitu chako from scratch!!!
Lakini nimekubali
jamii inione Bushoke kwani nilikuwa najua nini mimi na wewe tunatengeneza kwa
maisha yetu ya sasa na baadae!!! Nini kilichokubadilisha mke wangu? Fedha au
huyo mchungaji mwanamazingaombwe?
Hivi kweli kabisa
umefikia hatua ya kulipa waandishi wa habari ili wanikandamize nionekane sifai
katika jamii? Ni nini kilichokupata mke wangu??
Naomba uelewe kuwa
binafsi siogopi kwenda jela kwa sababu ya hiyo muvi mliyonizushia, kwani ni bora
nikakae jela kuliko kuishi huru huku mkininyanyasa kiasi cha kuondoa utu wangu
kama binadamu, lakini kinachoniuma ni familia yetu!! Kwanini watoto wateseke
kwa sababu ya tamaa zetu binafsi!! Nikifikiria hilo naumia sana!
Najua kwa sasa
inaonekana kama vile ni impossible kwa mimi na wewe kurudiana tena, lakini
binafsi naamini tunaweza!! Najua haitakuwa rahisi kwani tumeharibu mno, lakini
ni heri ya kujaribu kuliko kuendelea kufanya huu upuuzi tunaoufanya sasa!!
Kumbuka hiki
tunachokifanya sasa hatujajipaka matope sisi tu pekee, bali mziki wote wa Injili
Tanzania, na tusipotubu tukajirudi Mungu atatuhukumu kwa dhambi hii!!
Kumbuka kuwa hakuna
kati yenu atakayeshinda katika hii vita, vyombo vya habari pekee ndivyo
vitakavyo nufaika lakini mimi, wewe na mchungaji wote tuta loose!!
Mwisho nimalizie na
wewe mchungaji, tulipokutana mara ya kwanza nilikuchukulia kama kaka na kama
mlezi wetu wa kiroho!! Lakini umegeuka shetani mwenye pembe saba,
umeparaganyisha familia yangu, umeleta maumivu makali kwenye ukoo!!
Nakuonya tena kwa mara
nyingine, muache mke wangu!! Huyo ni mke wangu, nilimtolea mahali mimi mwenyewe
na wazazi wake waliniamini na kunikabidhi!!! Nasema niachie mke wangu!!
Wewe ni nyoka, imefika
time Watanzania wakujue ukweli wako wewe mbwa mwitu mkali uliyevaa ngozi ya
kondoo!!!
Umedanganya watu vya
kutosha na umefarakanisha ndoa nyingi sana kwa sababu ya kiburi cha pesa zako
chafu za sembe!! Umeudhalilisha ulokole kiasi cha kutosha imefika time
tuwaeleze Watanzania ukweli na wakufahamu kuwa wewe ni nyoka!!
Sitakubali kuona
ukiendelea kuitesa familia yangu, nitapambana na nitakushinda!!! Siogopi fedha
zako wala connection ulizonazo, ni bora nife nikiwa nimesimama kuliko kuishi
nimepiga magoti!
Nitapambana na wewe
mpaka mwisho ili historia isomeke vizuri ili hata wanangu wakiwa wakubwa wajue
kuwa baba yao sikuwa lofa kiasi cha kupiga magoti na kuelekeza shingo kibla
kuruhusu mdhalimu kama wewe uichinje familia yangu, bali licha ya umasikini
wangu nilisimama kiume na kupigana kutetea familia yangu!!!
Narudia tena
mchungaji, nitapambana na nitakushinda.."
CHANZO: TAIFA
KWANZA!
Comments
Post a Comment