- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
Fuatana nami Mkufunzi wako Amani Ezekiel -
+255765366133
Wengi tunajua
kwamba vyakula vingi vya viwandani vilivyowekwa kwenye makopo na makasha ya
paketi si salama kwa 100%, na pia wengi hujua kwamba vinywaji laini na pombe
sio salama kwa 100%, pia wengi tunajua sindano na vidonge vya uzazi wa mpango
si salama kwa 100%. Pia vyakula vingi fresh vya kutoka nje ya nchi kama samaki,
na nyama na cheese sio salama 100%.
Lakini
wengi hatujui kama MAJIKO YETU si salama 100%. Mara nyingi huwa nasema
ukiletewa chakula mezani, fikiria kidogo na jiulize swali hili ‘Je chakula
nilacho kinaenda kuufanyaje mwili wangu”
ANGALIZO:
Wagonjwa
wengi wa magonjwa sugu wamekuwa wakilalamika mara kwa mara kwamba ametumia dawa
flani ya kampuni flani akapata nafuu lakini hakuweza kupona kabisa. Akinamama
kwa akinababa wengine pia walitumia mbinu mbalimbali za kupunguza uzito na
kufanikiwa lakini baada ya muda uzito ulirudi tena mara mbili zaidi.
Swali ni
kwamba nini shida. Jibu ni rahisi sana Ukishatibiwa malaria unatakiwa ulale
kwenye net sio ulale bila net, ukilala nje ya net utapata malaria tena. Ndio
hata magonjwa sugu ukishatibika/kupata nafuu basi unatakiwa uache baadhi ya
vitu vilivyopelekea wewe kupata magonjwa hayo.
DALILI KWAMBA HOMONI ZA MWANAMKE ZIMEVURUGIKA
1. Kuwa na
hedhi ya muda mrefu zaidi ya siku 7
2. Kuwa na
hedhi yenye kuambatana na maumivu Makali sana
3. Kuwa na
hedhi yenye kuambatana na kichefu chefu na kuharisha
4. Kuwa na
hedhi iliyojaa woga mkubwa sana
5. Kuwa na
hedhi ambayo haina mpangilio, Unaweza kuingia mara tatu kwa mwezi mmoja, mara
mbili au unaweza usipate kabisa hata miezi 6 hadi mwaka.
6. Kuwa na
ndevu sehemu za usoni na kifuani nyingi kupita kiasi
7. Kuwa na
kitambi cha tumbo la chini (Abdominal obesity)
8. Kukosa
mtoto kwa muda mrefu
9. Kukosa
hamu ya tendo la ndoa na kuwa na tendo la ndoa lenye kuambatana na maumivu
makali
10. Mwili
kuwa unauma sana hasa misuli bila sababu ya msingi, kuumwa sana na kichwa bila
sababu ya msingi.
HOMONI NI VITU GANI
Homoni ni
kemikali zinazotolewa na tezi za mwili na kusafiri mwilini kupitia mfumo wa
mzunguko wa damu hadi ogani za mwili. Homoni ndio zinasababisha mabadiliko
katika ogani mbalimbali za mwili. Kwa lugha nyingine zinapeleka ujumbe kwa
ogani mbalimbali za mwili ili ziweze kufanya kazi kulingana na mahitaji ya
mwili.
Homoni
ndio kemikali kuu zinazotumika kusafirisha taarifa kwenye viungo mbalimbali vya
mwili hivyo mabadiliko madogo ya homoni husababisha mabadiliko makubwa kwenye
mwili.
Mfumo wa
utengenezaji wa homoni unalingana kwa kiasi kikubwa kwa wanaume na wanawake
isipokuwa homoni zinazotengenezwa kwenye tezi zilizopo kwenye mfumo wa uzazi.
Baadhi ya Homoni na Kazi zake
1. Homoni ya Kiume – Testosteroni, homoni hii huhusika na uumbaji wa via vya uzazi tangu
mtoto akiwa tumboni, inabalehesha na pia kumpa mwanaume nguvu na hamu za tendo
la ndoa.Katika mwili wa mwanamke homoni hii ipo kidogo sana.
2. Homoni ya Kike – Oestrogen, homoni hii huhusika na uumbaji wa via vya uzazi vya
mwanamke tangu akiwa tumboni, inabalehesha na pia inahusika na mzunguko wa
hedhi na kumpa mwanamke hamu ya tendo la ndoa.
3. Homoni ya Insulini – homoni hii ipo kwa
wanaume na wanawake inahusika na kupunguza kiasi cha wanga na sukari (glucose)
katika mfumo wa damu.
NAMNA HOMONI ZINAVYOVURUGWA
Miili yetu
ikiwa katika hali ya kawaida hutengeneza homoni kwa uwiano stahiki na kufanya
ogani na tishu za mwili kufanya kazi vizuri.
Pale
homoni moja au zaidi inapoongezeka au kupungua kiwango cha kawaida
kinachohitajika na ogani/tishu ili kuweza kufanya kazi basi na homoni zingine
huongeza au kupunguza uzalishaji wake.
Baadhi ya
sababu zinazopelekea kuvurugika kwa hormone mwilini.
- mifumo
ya uzazi wa mpango wa kisasa (vidonge na vijiti)
- msongo
wa mawazo
- matumizi
makubwa yaliyopitiliza ya vipodozi.
-
ujauzito, kukoma kwa hedhi kwa wanawake kutokana na umri
-
kubale/kuvunja ungo
-
kutokufanya mazoezi
- mfumo wa
maisha, unene, na mfumo wa ulaji (kula wanga na sukari ile hali wanga huo
hauendi kutumika)
MWANAMKE: MAHUSIANO YA CHAKULA UNACHOKULA NA
UZAZI
MATOKEO YA UPIKAJI WA WANGA NA UTUMIAJI WA
SUKARI NYINGI JIKONI
1. KUONGEZEKA KIASI CHA HOMONI YA KIUME KWA
MWANAMKE:
Ulaji wa
wanga na sukari nyingi ile hali mwanamke hauko na kazi nyingi za kufanya, yaani
wewe unakuwa umekaa tuu tangu asubuhi husafishi nyumba, wala, nguo, wala
vyombo, kazini kwenyewe wewe ni bosi, hufanyi mazoezi wala kazi ngumu za
mikono, hii inapelekea mwanamke kuwa mnene na mzito hivyo kuwa na kiasi kikubwa
cha homoni ya insulin mwilini.
Homoni hii
ya insulin ikishakuwa nyingi mwilini kwa mwanamke inasababisha kuongezeka
uzalishaji wa homoni ya kiume (Kwa kawaida homoni hii ipo kiasi kidogo ndani ya
mwili wa mwanamke). Matokeo yake angalia kipengere (a) na (b) hapa chini:
(a) Ikiwa
homoni ya kiume itakuwa nyingi ndani ya mwili wa mwanamke matokeo yake ni mwili
wa mwanamke kugeuka na kuwa na tabia za kidumedume (Kuota ndevu, kuwa na sauti
neno, kuota chunusu sugu, kunenepa sana na kuwa na kitambi katika tumbo la
chini). Kuna hatari pia ya kupata kisukari aina ya II. Pia unakuta mwanamke ana
uso wenye mafuta mengi sana kupita kiasi, shingo kuwa nyeusi sana na sehemu
zingine kama kwapa na kwenye mikunjo sehemu za siri, kupata viotea shingoni
yaani “Skin Tags”.
MUHIMU TAMBUA YA KWAMBA – Ulaji wa Wanga na
Sukari uliopitiliza ile hali huna kazi za nguvu inapelekea mwanamke kushindwa
kukomaza mayai yake, hii ni kutokana na kuongezeke kwa kiwango cha insulin
mwilini ambayo inaenda kuamsha uzalishaji homoni ya kiume inayomfanya mwanamke
awe na mwili wa kidumedume.
TAKE NOTE: Si wanawake wote watapatwa na matatizo
haya hata kama wanakula wanga na sukari kwa wingi na hawana kazi za nguvu, hii
ni kwa sababu kila mwanamke ana mwili wake tofauti na mwingine (kila machine
ina ufunguo wake)
(b) KUSHINDWA KUPEVUSHA MAYAI Mwanamke huwa ana
viwanda viwili vya kuzalisha mayai kila mwezi yaani kwa lugha nyingine ni
“Ovari ya kushoto” na “Ovari ya kulia”.
Ndani ya
ovari ya mwanamke kuna mayai ambayo hayajakoma. Haya mayai hukomazwa kila mwezi
na kutupatia yai ambalo linatakiwa lipatiwe urutibishaji endapo itakutana na
mbegu ya kiume.
Sasa
inapotokea hizo mifuko ya mayai zimekomaa vizuri kwenye ovary na zinatakiwa
zipasuke zitoe mayai NA KWA BAHATI MBAYA kabisa “Kitendo hicho kinashindikana” hivyo
hizo mifuko ambazo zimeshindwa kupasuka na kutoa yai zinabaki na umbo kama
“Zabibu zilizo kwenye kikonyo chake”.
Kwa hiyo
katika mji wa uzazi kuna kuwa na alama nyingi kama za zabibu hivi zimejaa.
2. KUONGEZEKA KWA KIASI KIKUBWA CHA HOMONI YA
KIKE KWENYE MWILI WA MWANAMKE
Kiwango
cha Estrogen (homoni ya kike) huongezeka kupita kiasi
Hii
inasababishwa na insulin kuisisimua ovary kufanya kazi kwa kiwango kikubwa na
hii inapelekea kiwango cha homoni hii kuwa juu kwenye damu.
Madhara ya
homoni hii kuwa katika kiwango kikubwa katika mwili inaweza kukupelekea ukuta
wa kizazi kujengeka na kuwa mnene kupita kiasi na hatimaye unaweza kuwa
hatarini kupata kansa ya kizazi.
Na hii
ndio sababu kubwa ya kupata hedhi nzito kupita kiasi yenye mabonge ya damu
sana, kwa sababu kazi kubwa ya homoni ya kike ni kukufanya wewe uonekane
“mwanamke” na ndio homoni ambayo inajenga ukuta wa kizazi kila mwezi ili kama
mimba ikitungwa mtoto aje ajishikize kwenye ukuta imara.
Lakini
inapotokea kiwango chake ni kukubwa ukuta mnene utajengwa kila mwezi na inapokuwa
mimba haijatungwa ukuta utabomolewa na kama ukuta huu ni mnene wakati wa hedhi
ya kawaida damu nyingi sana itatoka. Ukiona dalili hizo fika hospitali maana
kuna hatari kubwa ya kuishiwa damu.
USHAURI
KAMA UNA DALILI HIZO HAPO JUU NA KISHA ULIPATA
DAWA HOSPITALINI NA HUJAPONA, mchawi wako anaweza kuwa jiko lako. Watu wengi
wanene walikokuwa katika program yetu ya kupunguza unene na vitambi wametoa
shuhuda nyingi sana za kuwa wepesi wa mwili, kupata hedhi kawaida na pia kuwa
wachangamfu wakati wa tendo la ndoa.
UNAWEZA PATA BIDHAA NA HUDUMA ZIFUATAZO TOKA
TREVO
1. Program
ya kupunguza unene, uzito na kiriba Tumbo pamoja na kurudisha hedhi
iliyovurugika (kwa muda wa miezi mitatu. Trevo, itakufikia popote ulipo ili
mradi una WhatsApp utapata program.
2. Program
ya kukontrol kisukari bila kutumia insulin injection, hii ni ndani ya siku 90
utakuwa upo vizuri na baada ya hapo utajifunza namna ya kuishi bila kutegemea
sindano. (inawahusu wanaume na wanawake), pia utaipata popote ulipo duniani.
3.
Waliokosa watoto muda mrefu nenda kapime hospitalini ijulikane shida ni nini,
je ni uvimbe, mayai machanga, mbegu hazina nguvu, ukuta wa mimba mbovu?
Suluhisho lipo.
Whatsapp +255765366133 na Massage za kawaida
Simu
tu +255 716128536
MAJI NA MAZOEZI NI MUHIMU SANA, mana wengine katika
program yetu ya kula huacha kufanya mazoezi, fanya mazoezi mepesi ya kutembea,
kukimbia taratibu (jogging), kuendesha baiskeli, sitt ups na mazoezi ya kazi
ndogondogo za mikono. Ni LAZIMA kwa mwanadamu uliye hai ili uongeze uwezo wa
mwili wako kuchakata chakula na kuchukua vitaminis, madini na nguvu pamoja na
nishati mbalimbali kwa ajii ya ujenzi wa mwili wako.
UKIKAA IDLE VITU VINGI MWILINI MWAKO VINAKUWA
IDDLE.
Credit:
Mitandao ya Kijamii
Comments
Post a Comment