- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
Na ELIZABETH HOMBO-DAR ES SALAAM
BAADA ya
kuishi nchini Canada kwa zaidi miaka miwili sasa, aliyekuwa Katibu Mkuu wa
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willbrod Slaa amesema anakuna
kichwa ili kupima mazingira yaliyomfanya aondoke nchini na familia yake kama
yapo au laa.
Septemba,2015
wakati wa Uchaguzi Mkuu Dk. Slaa alijiweka kando na siasa, kwa kile
alichokieleza kutofautiana na chama chake juu ya masharti ya kumpokea aliyekuwa
mgombea urais wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa),Edward Lowassa.
Hata hivyo
Dk. Slaa ambaye amekuwa mbunge wa Karatu kwa vipindi vitatu mfululizo, hakuweza
kuainisha mazingira yaliyomfanya aondokea nchini na kwenda kuishi ughaibuni.
“Sina
tabia ya kuyumbishwa…sina chuki na mtu yeyote, sipendi siasa za udanganyifu na
propaganda. Nimeachana na siasa tangu Julai 28,2015, baada ya kuona misingi ya
chama nilichoshiriki kukijenga imepotoshwa,”alisema Dk. Slaa siku alipotangaza
kuachana na siasa.
Pamoja na
mambo mengine, alisema sharti la kwanza ambalo alitaka Chadema izingatie ni
kiongozi huyo wa zamani ndani ya serikali ya CCM, kujisafisha dhidi ya tuhuma
ya kashfa ya sakata la Kampuni ya Kufua Umeme ya Richmond aliyohusishwa nayo
akiwa Waziri Mkuu.
Kurudi nchini
Akizungumza
na MTANZANIA akiwa nchini Canada jana, Dk. Slaa alisema amemaliza masomo yake
na baada ya kufanya tafakari atarejea nchini wakati wowote.
“Ni kweli
nimemaliza masomo yangu. Bado napima mazingira yaliyonifanya niondoke na
familia yangu. Baada ya hapo tutaangalia uwezekano wa kurejea,”alisema.
Alisema
kuhusu matarajio yake ya kisiasa, watu wameshindwa kumwelewa siku ambayo
alitangaza kustaafu siasa za vyama.
Alisema
alichomaanisha ni kwamba, pamoja na kuachana na siasa za vyama,atakuwa tayari
kupiga kelele pale anapoona masilahi ya Taifa yanaumia.
“Hadi sasa
sijapiga kelele kwa kuwa sijaona masilahi ya Taifa yakiangamizwa, hatua
mbalimbali zinazochukuliwa ni kweli zinawaumiza wasiohusika.
“Ndio
maana nilitumia katika makala mojawapo mtego wa panya huwakamata wanaohusika na
wasiohusika. Hivyo, makosa madogo mimi hayanisumbui kwa kuwa hakuna binadamu
kamilifu ,”alisema.
Rais Magufuli
Akizungumzia
utendaji wa Rais Dk. John Magufuli, alisema watu waelewe hakuna nchi hata moja
ambapo kiongozi atakubalika na watu wote kwa asilimia 100.
Alisema
wako watu ambao masilahi yao yataguswa kwa namna moja au nyingine hivyo lazima
watapiga kelele.
Kutokana
hilo, alisema Rais Dk. Magufuli katika kundi ambalo halihitaji fedha
ameyatekeleza yote kwa asilimia 99.9, ikiwa ni pamoja na uwajibikaji
serikalini, kuchukua hatua kali dhidi ya rushwa, uwizi wa mali za umma,
uwindaji haramu na kudhibiti dawa za kulevya.
“Hatua
zote zimechukuliwa,zinapaswa kuwa endelevu. Kwa bahati mbaya mchwa wengine
waliopenya mpaka ndani ya Ikulu na Serikali na huwezi kufagia Serikali nzima
kwa siku mmoja.
“Kwa jinsi
Rais ambavyo hayumbi na wala hayumbishwi, nina hakika atafikia malengo na
kurudisha Taifa kwenye misingi ya tunu za Taifa ya uwazi, ukweli, uadilifu,
kuheshimiana na kuthaminiana na hasa kujali utu.
“Hii ndiyo
hali ambayo JPM kila siku anaiita ‘Transition’ (kipindi cha mpito). Tutafika
tu, tunatakiwa kuwa wavumilivu na wenye uzalendo wa kweli ana nia njema ya
kufikisha Taifa mahali pazuri. Hii inahitaji kuweka pembeni maslahi yetu
binafsi kama mtu mmoja mmoja, viongozi wa Serikali au hata wa kisiasa,”alisema
Dk. Slaa.
Upinzani
Kuhusu
mwenendo huo endapo utasaidia upinzani kuingia Ikulu 2020, Dk. Slaa alisema
wakija na ajenda mbadala na makini yenye kuwalenga wananchi moja kwa moja
itawasaidia.
Dk. Slaa
ambaye pia alipata kugombea urais kupitia Chadema mwaka 2010, alisema endapo
wataendelea kurukia kauli za Rais, basi upinzani utafutika kabla ya 2020.
“Kama
nilivyorejea mara kadhaa, upinzani makini utaingia Ikulu kwa ajenda mbadala.
Ajenda makini yenye kuwalenga wananchi moja kwa moja katika kuwatoa kwenye kero
zao mbalimbali.
“Hadi sasa
ninachoona ni ‘kurukia’ kauli za JPM, lakini kauli si ajenda na hatupeani maksi
kwa kuzungumzia usahihi wa lugha. Wako wanaotazama usahihi wa lugha na mahali
pa kutazama usahihi huo. Kimsingi hayo ni masuala ya darasani au kwenye uandishi
wa vitabu.
“Aidha
kumtuhumu JPM kukiuka Katiba na sheria nayo haina tija. Wote wanaomtuhumu
wanajua kuwa wakiambiwa waonyeshe kifungu mahususi alichokiuka yeye mwenyewe
katika utendaji wake hawana majibu ya kuridhisha.
“Hivyo
mimi sijaona mwenendo wa JPM unaosaidia kuingiza upinzani Ikulu. Isitoshe kama
hawatakuja na ajenda makini na mkakati ulioandaliwa unaowatoa wananchi hapa
walipo kwenda kwenye raha, upinzani unaweza kufutika kabla ya 2020,”alisema Dk.
Slaa.
CHANZO: MTANZANIA
Comments
Post a Comment