Mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mhe Rukia Muwango akisisitiza umuhimu wa kufanya mazoezi.
Mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mhe Rukia Muwango akionyesha mfano wa ufanayaji mazoezi
Mkuu wa wilaya ya Nachingwea ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa Wilaya hiyo Mhe Rukia Muwango akifanya mazoezi katika uzinduzi huo
Matembezi yakiendelea vyema


Na Mathias Canal, Lindi
Mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mhe Rukia Muwango ameitaka Halmashauri ya
Wilaya hiyo irejeshe maeneo yote ya wazi yaliyo vamiwa na kutumika
kinyume cha matumizi yaliyolengwa.
Dc Muwango ametoa agizo hilo
mjini Nachingwea kwenye uzinduzi wa kampeni ya kitaifa ya kudhibiti
magonjwa yasioambukiza na yanayoweza kuzuilika kupitia mazoezi na
michezo.
Uzinduzi huo uliofanyika katika uwanja wa kumbukumbu ya
Sokoine ambapo Alisema kuwa yeye kama mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na
usalama ya wilaya hiyo anatambua na anazotaarifa za kutosha kuwa maeneo
mengi ambayo yalitengwa kwa ajili michezo na shuguli nyingine za umma
yamevamiwa na kubadilishwa matumizi.
Dc Muwango ameitaka halmashauri hiyo kurejesha haraka kutoka mikononi mwa wavamizi.
Katika hali inayoonesha kuwa mkuu huyo wa Wilaya amelivalia njuga suala
hilo, ameitaka Halmashauri hiyo ipeleke na kumkabidhi mikakati na
taarifa za utekelezaji wa agizo lake haraka iwezekanavyo.
Sambamba na agizo hilo Muwango ameitaka Halmashauri hiyo kutenga maeneo kwa ajili ya michezo.
Amebainisha kuwa bila kuwa na maeneo ya wazi itakuwa vigumu kufanikiwa
kukuza michezo na kuibua vipaji mbalimbali vya wanamichezo.
Amemuagiza Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya hiyo kuwaandikia
wakuu wa shule za sekondari na walimu wakuu wa shule za msingi ili
warejeshe mbio za mchakamchaka kwenye shule zao kwani shule nyingi
wanafunzi hawakimbii mchakamchaka.
"Jambo ambalo ni muhimu kwa
afya na akili za wanafunz ila walimu wawe na usimamizi mzuri ili
wanafunzi wasiathiriwe katika masomo na usalama wao," Alisistiza
Muwango.
Akizungumzia umuhimu wa michezo na mazoezi Dc Muwango alisema kuwa licha ya kuimarisha, umoja,undugu na mshikamano.
Lakini pia mazoezi na michezo ni kichocheo kikubwa cha maendeleo, utulivu na amani katika jamii.
Alibainisha kuwa chanzo cha baadhi ya migogoro katika baadhi ya jamii
ni magonjwa ambayo yanaweza kuepukwa kwa kufanya mazoezi ambapo Hata
hivyo jamii husika hazitambui jbo hilo Badala yake inayahusisha magonjwa
hayo na sababu zisizo na msingi Ikiwa ni pamoja na Imani potofu, uchawi
na ushirikina mambo ambayo hupelekea kunyoosheana vidole na kusababisha
migogoro.
"Lakini mtu akiwa mgonjwa hawezi kufanya shuguli za
kiuchumi na maendeleo yake mwenyewe, Taifa na hata wanaomuuguza hawawezi
kufanya kazi ambazo zingewaletea maendeleo," Aliongeza Muwango.
Mkuu huyo wa Wilaya alitoa wito kwa wananchi wilayani humo kujenga
utamaduni wa kufanya mazoezi bila kujali rika Huku akiwaasa kuunda
vikundi vya michezo na mazoezi Kwa sababu madhara ya kutofanya mazoezi
ni makubwa ambapo sio rahisi kuyabaini haraka.
Uzinduzi huo ambao
ni utekelezaji wa agizo la makamu wa Rais aliyetaka kuwe na kampeni ya
kitaifa ya kudhibiti magonjwa yasioambukiza na yanayozuilika kupitia
michezo uliandaliwa na ofisi ya mkuu huyo wa wilaya ya Nachingwea Ambapo
michezo mbalimbali ilichezwa, sambamba na upimaji wa afya na
uchangiaji damu kwa hiari.
Comments
Post a Comment