- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
Mbunge
mmoja ametoa wito kwa wanawake waliopo katika maeneo yenye wafuasi wengi wa
upinzani nchini Kenya kutofanya mapenzi na waume zao ambao hawajajisajili kama
wapiga kura.
Kwa mujibu
wa gazeti la The Standard nchini humo, mwakilishi wa wanawake mjini Mombasa
Mishi Mboko amewataka wanawake nchini humo kuwanyima wanaume zao haki zao za
kindoa ili kuwashinikiza waende kujisajili kama wapiga kura ili kujiandaa kwa
uchaguzi wa mkuu ujo unaofanyika tarehe 8 mwezi Agosti.
Akiongea
katika uwanja wa maonyesho ya kilimo katika eneo la Mkomani Bi Mboko alisema
kuwa ngono ni kifaa kizuri kinachoweza kuwashinikiza wanaume kukimbilia
kujisajili katika shughuli hiyo ilionza siku ya Jumatatu.
Kulingana
na gazeti hilo hata hivyo, mumewe Mboko hatonyimwa haki hiyo ya ndoa kwa kuwa
tayari amejisajili kama mpiga kura.
“Wanawake
huu ndio mpango munaofaa kuutumia.Ni mpango muziri sana.Wanyimeni haki yao ya
kufanya mapenzi hadi pale watakapowaonyesha cheti cha kupiga kura”, alisema.
Mboko
aliongezea kwamba imefikia wakati ambapo wanawake wanafaa kutumia ngono kuwalazimisha
waume zao kuchukulia shughuli ya usajili wa wapiga kura na umuhimu mkubwa.
Source: BBC
Comments
Post a Comment