- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
Mtendaji Mkuu
wa TBA, Elius Mwakalinga
Na Sophia Mwambe
WAKALA wa
Majengo Tanzania (TBA) umechukua hatua za haraka, kwa kumuondoa kwenye nafasi
yake Meneja wa Mkoa wa Simiyu, Michael Semfuko na kumrejesha Makao Makuu Dar es
Salaam kupisha uchunguzi.
Hatua hiyo
imechukuliwa baada ya Rais John Magufuli kukataa kukubaliana na gharama ya Sh
bilioni 46 ya kujenga Hospitali ya Mkoa wa Simiyu.
Aidha, TBA
imeunda kamati ya wataalamu kwenda Simiyu kuchunguza kujua uwiano wa mradi huo
na gharama iliyoelezwa na meneja huyo kwa Rais akiwa kwenye ziara huko.
Rais
Magufuli akiwa ziarani Simiyu wiki iliyopita, aliweka jiwe la msingi kwa ajili
ya ujenzi wa hospitali hiyo, lakini hakukubaliana na gharama ya Sh bilioni 46
iliyotajwa ili kukamilisha mradi huo badala yake alitaka ijengwe kwa Sh bilioni
10.
Uamuzi wa
kumng’oa meneja huyo wa mkoa, uliwekwa wazi Dar es Salaam jana na Mtendaji Mkuu
wa TBA, Elius Mwakalinga wakati wa ziara ya Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa
wa Simiyu, kuzungumzia mradi huo pamoja na kutembelea miradi inayosimamiwa na
TBA, ikiwa ni agizo alilopewa Mkuu wa Mkoa, Antony Mtaka na Rais.
“Kisheria
miradi yote ya ujenzi kwenye mikoa yote huwa inasajiliwa TBA, lakini cha
kushangaza mradi huu haukuwa umesajiliwa na sielewi, lakini sitaki kusemea
tutakapofika huko tutajua ni kwa nini imekuwa hivyo,” alisema Mwakalinga.
Aliongeza
kuwa meneja huyo atatakiwa kutoa maelezo, ikiwa ni utaratibu wa serikali aeleze
kwa nini alifikia hatua ya kuzungumzia, mradi ambao haujasajiliwa.
“Inawezekana
meneja alipewa mradi siku hiyo au alikuwa anaupitia ili aulete kwetu, yote hayo
tutayajua baada ya maelezo yake,” alieleza mtendaji huyo.
Akizungumzia
zaidi mradi huo wa Simiyu, alisema wameunda kamati kwa ajili ya kupitia upya
mchoro uliokuwepo na kuandaa utaratibu ili kuanza mchakato ya ujenzi kwa kuwa
tayari Rais alishazungumza hivyo unapaswa kutekelezwa.
Kwa upande
wake, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mtaka alipongeza juhudi za TBA kwa miradi
mbalimbali wanayoisimamia ikiwemo mradi wa ujenzi wa hosteli za wanafunzi wa
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).
Mtaka
alisema kwa upande wake hakuridhishwa na gharama za mradi huo, kwa kuwa thamani
ya mradi haikuendana na thamani ya fedha iliyotajwa.
“Gharama
iliyotajwa ni kubwa, niliamua kuwasiliana na viongozi wengine mkoani, lakini
nashukuru Rais alikuja na yeye hakuridhishwa na gharama hiyo ndipo alitutaka
tuje TBA Dar es Salaam kuangalia miradi pamoja na kufanya mazungumzo ya jinsi
ya kutekeleza mradi wa ujenzi wa hospitali kwa gharama ya Sh bilioni 10 ambayo
ameahidi kuitoa,” alisema Mtaka.
Aidha,
alishauri taasisi za serikali zinazohusika na mambo ya ujenzi kuwa wabunifu na
kuifanya nchi kuwa na mfumo wake wa ujenzi ambao utakuwa sio wa kuiga kutoka
katika mataifa mengine.
“Tunataka
tujenge mkoa mpya wa kiuchumi, hatuwezi kusema tunakwenda kwenye uchumi wa kati
wakati hatuna mikoa iliyoandaliwa, tunaamini Rais akituunga mkono kwenye ujenzi
wa hospitali yetu na tukathubutu kufanya ujenzi huo tutakuwa tumemsaidia Rais
pamoja na kufanya na mikoa mingine ambayo haina hospitali za rufaa kuiga,”
alisema Mtaka.
CHANZO: HABARILEO
Comments
Post a Comment