- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
Waziri wa Fedha na
Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (kushoto), akiwa katika mazungumzo na mgeni
wake ambaye ni Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Fedha Duniani-IMF,
Bw. Bhaswar Mukhopadhway, walipokutana Makao Makuu ya Wizara hiyo Jijini Dar es
salaam.
Waziri wa Fedha na
Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (katikati) pamoja na maafisa waandamizi wa
Wizara hiyo wakiwa katika mazungumzo na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la
Kimataifa la Fedha Duniani-IMF, Bw. Bhaswar Mukhopadhway, Makao Makuu ya Wizara
hiyo Jijini Dar es salaam.
Mwakilishi Mkazi wa
Shirika la Kimataifa la Fedha Duniani-IMF, Bw. Bhaswar Mukhopadhway, (kulia)
akisikiliza kwa makini maelezo yaliyokuwa yakitolewa na Waziri wa Fedha na
Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (hayupo pichani) wakati wa mazungumzo kati yao
yaliyofanyika Makao Makuu ya Wizara hiyo Jijini Dares salaam ambapo IMF
imeipongeza Tanzania kwa kusimamia vizuri ukuaji wake wa uchumi.
Ujumbe wa Tanzania
na Shirika la Kimataifa la Fedha Duniani-IMF wakiwa katika mazungumzo Makao
Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es salaam, ambapo Shirika hilo
limeahidi kuendelea kushirikiana na Tanzania ili kufikia maendeleo
inayoyatarajia kwa manufaa ya Taifa na wananchi wake kiuchumi na kijamii.
Mwakilishi Mkazi wa
Shirika la Kimataifa la Fedha Duniani-IMF, Bw. Bhaswar Mukhopadhway, (kulia)
akisisitiza jambo wakati wa mkutano wake na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe.
Dkt. Philip Mpango (hayupo pichani), Makao Makuu ya Wizara hiyo Jijini Dares
salaam ambapo IMF imeipongeza Tanzania kwa kusimamia kikamilifu ukuaji wake wa
uchumi.
Mkurugenzi wa Idara
ya Sera wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Ollal, akisisitiza jambo wakati wa
mkutano kati ya Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango na
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Fedha Duniani-IMF, Bw. Bhaswar
Mukhopadhway, walipokutana Makao Makuu ya Wizara hiyo, Jijini Dar es salaam.
Waziri wa Fedha na
Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango, akizungumza jambo na mgeni wake ambaye ni
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Fedha Duniani-IMF, Bw. Bhaswar
Mukhopadhway, (hayupo pichani), Makao Makuu ya Wizara hiyo Jijini Dar es
salaam.
Waziri wa Fedha na
Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango, akizungumza jambo na mgeni wake ambaye ni
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Fedha Duniani-IMF, Bw. Bhaswar
Mukhopadhway, (hayupo pichani), Makao Makuu ya Wizara hiyo Jijini Dar es
salaam.
Waziri wa Fedha na
Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (kushoto), akiagana na mgeni wake ambaye ni
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Fedha Duniani-IMF, Bw. Bhaswar Mukhopadhway,
baada ya kumalizika kwa mazungumzo kati yao yaliyofanyika Makao Makuu ya Wizara
hiyo Jijini Dar es salaam, ambapo IMF, imesifu jitihada za Serikali ya Awamu ya
Tano, katika kusimamia na kukuza uchumi wa Taifa.
Benny Mwaipaja
WFM-Dar es salaam
SERIKALI imesema
kuwa inatambua mchango mkubwa wa sekta binafsi katika kukuza uchumi wa nchi na
kuahidi kuendelea kuimarisha ushirikiano na sekta hiyo ili kuharakisha
maendeleo ya wananchi kupitia sekta ya viwanda na biashara.
Hayo yamesema na
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, alipokutana na kufanya
mazungumzo na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Fedha Duniani-IMF,
Bw. Bhaswar Mukhopadhway, Makao Makuu ya Wizara hiyo Jijini Dar es salaam.
Amesema kuwa uchumi
wa nchi unategemea sana sekta binafsi yenye nguvu na yenye utulivu ambayo
itachangia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya nchi kwa njia ya uwekezaji na ulipaji
kodi.
Kwa upande wake
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Fedha Duniani-IMF, Bw. Bhaswar
Mukhopadhway, amesema kuwa Shirika lake limeridhika na kiwango kikubwa cha
ukuaji wa uchumi wa Tanzania miongoni mwa nchi za Afrika na kwamba wanatarajia
kuona uchumi huo ukiendelea kukua zaidi kwa ushirikiano na sekta binafsi.
Ametaja sifa za
ukuaji huo kuwa ni pamoja na kuimarishwa kwa ukusanyaji wa kodi, udhibiti wa
mfumuko wa bei na thamani ya shilingi, uwajibikaji na pamambano dhidi ya
rushwa, ufisadi, na utekelezaji mzuri wa Bajeti ya serikali.
Hivi karibuni Bodi
ya Wakurugenzi ya IMF ilitoa taarifa yake ya mapitio ya mwenendo wa uchumi wa
Tanzania na kueleza kuridhika kwake na uimara wa uchumi huo baada ya kutoyumba
katika nusu ya kwanza ya mwaka 2016 na kueleza kuwa utaendelea kukua kwa
wastani wa asilimia 7 kama ilivyopangwa.
Shirika la
Kimataifa la Fedha Duniani ni chombo cha kimataifa kinachosaidia ukuaji wa
uchumi wa nchi wanachama wake kwa kuweka mikakati na kuzikopesha fedha kwaajili
ya shughuli mbalimbali za maendeleo ya kiuchmi na kijamii ikiwemo, elimu, afya,
miundombinu, nishati na miradi mingine kadha wa kadha.
Mwisho
Comments
Post a Comment