- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe. Dkt. Rehema Nchimbi akipanda viazi lishe katika
shamba la Mkulima wa viazi katika kijiji cha Nkungi Wilayani Mkalama katika
ziara yake wilayani humo.
Mkuu wa
Wilaya ya Mkalama Mhe. Jakson Masaka akishiri kupanda viazi lishe katika shamba
la Mkulima katika kijiji cha Nkungi Wilayani humo.
Katibu
Tawala Mkoa wa Singida Dkt. Angelina Mageni Lutambi akipanda viazi lishe
katika shamba la Mkulima wa viazi katika kijiji cha Nkungi Wilayani Mkalama.
Mkurugenzi
wa Halmashauri ya Mkalama Mhandisi Geofrey Sanga akipanda viazi lishe katika
shamba la Mkulima wa viazi katika kijiji cha Nkungi Wilayani Mkalama.
Katibu
Tawala Mkoa wa Singida Dkt. Angelina Mageni Lutambi akisadiniana na mkulima
kuandaa matuta kwa ajili ya kupanda viazi lishe katika shamba la Mkulima wa
viazi katika kijiji cha Nkungi Wilayani Mkalama.
Baadhi ya
watumishi wa halmashauri ya Mklama wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Singida (hayupo
pichani) alipokuwa akizungumza nao juu ya uadilifu na kufanya kazi kwa bidii
ili kuendana na kasi ya hapa kazi tu.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe. Dkt.
Rehema Nchimbi au “mama Nchimbi” kama anavyojulikana jana amefanya ziara ya
kikazi Wilaya ya Mkalama na kuagiza watendaji kusimamia miradi kwa umakini
kwakuwa hataki kusikia mradi wowote uko chini ya kiwango.
Dkt. Nchimbi amesema msamiati chini
ya kiwango hataki kuusikia kwakuwa umekua ukifanya watendaji kuwa wazembe na
kuongeza kuwa hatua kali zitachukulkiwa kwa viongozi wote ambao hawatasimamia
ipasavyo utekelezaji wa maelekezo hayo.
Ameongeza kuwa watendaji wamekuwa
wakiilalamikia serikali na kuirudisha nyuma kwa kutotekeleza majukumu yao
ipasavyo na hivyo kupelekea wananchi kuona serikali haifanyi chochote wakati
inaleta pesa nyingi za miradi mbalimbali ambapo jukumu la watumishi ni
kusimamia miradi ili ifanye kazi ipasavyo.
Dkt. Nchimbi amesema viongozi wote
kabla ya kusaini mikataba yoyote ya halmashauri wanapaswa kukiri thamani ya
mali zao zinazohamishika na zisizohamishika ili kama mradi utatekelezwa chini
ya kiwango, mali zao zitumike kufidia pesa ya serikali iliyopotea.
“Mradi wakati unajengwa Mkurugenzi,
Mwenyekiti wa halmashauri na wataalam wanauangalia bila kusema chochote,
ukikamilika ndio wanakuambia umejengwa chini ya kiwango, kuanzia sasa sitaki
kusikia msamiati wa ‘chini ya kiwango’ na endapo ikitokea chini ya kiwango
tutahakikisha fedha ya serikali inarudi", amesema Dkt. Nchimbi.
Aidha katika kikao hicho na watumishi
wote wa halmashauri hiyo amewaagiza wakuu wote wa shule za msingi na sekondari
kuwaruhusu wanafunzi ambao hawana sare kuanza masomo huku utaratibu wa
kuwafuatilia wazazi watimize majukumu yao ukiendelea.
“ Baada ya elimu kuanza
kutolewa bure, changamoto nyingine iliyobakia kwa baadhi ya wazazi ni uwezo wa
kuwashonea watoto wao sare za shule, sasa ninaagiza wakuu wa shule za sekondari
na Msingi wote Wilayani hapa kuwaruhusu watoto hao waingine madarasani hata
kama hawajavaa sare za shule ili wasikose haki yao ya msingi kwa sababu ya sare
tu”, ameagiza Dkt. Nchimbi.
Awali kabla ya kuzungumza na
watumishi Dkt. Nchimbi alifanya ziara katika mashamba ya wakulima ili kujionea
na kushiriki na wananchi shughuli za kilimo hasa mashamba ya viazi katika
kijiji cha Nkungi na mashamba ya mtama katika kijiji cha Ilunda wilayani humo.
Dkt. Nchimbi akiwa katika shamba la
mkulima wa viazi lishe katika kijiji cha Nkungi alipanda viazi na kuhamasisha
wananchi wengine walime mazao ambayo yanatumia maji kwa ufanisi kama vile
viazi, mihogo, matama na uwele kutoka na mabadilike ya tabia nchini ili
kujihakikishia uwepo wa chakula.
Amewataka watendaji hasa wa kada za
kilimo na ufugaji kuacha kufanya kazi kwa mazoea hasa kuandaa taarifa za
makaratasi bali wawatembelee wakulima na wafugaji katika maeneo wanayofanya
shughuli zao ili waweze kutoa ushauri kwa kupata picha halisi.
“Sipendi kiongozi anayesema yupo
karibu na wananchi kwa sababu hatuwezi kupima ukaribu uliopo hivyo ni vyema
kuanzia sasa tuache kuwa karibu na badala yake tuwe pamoja nao”, amesema Dkt.
Nchimbi.
Comments
Post a Comment